Naomba msaada jinsi ya kujiunga na sim banking

the horticulturist

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2012
Posts
1,959
Reaction score
1,929
Nimejaribu ila kila mara naambiwa nimekosa namba ya siri au namba ya kadi, namba ya kadi ni ipi!? Maana mimi natumia hizi namba 16 ziko mbele ya kadi na bank ni CRDB mtandao ninaotumia ni vodacom, ahsanteni ambae alifanikiwa anijuze tafadhari.
 
Nimejaribu ila kila mara naambiwa nimekosa namba ya siri au namba ya kadi,namba ya kadi ni hipi maana mimi natumia hizi namba 16 ziko mbele ya kadi na bank ni crdb mtandao ninaotumia ni vodacom,ahsanteni ambae alifanikiwa anijuze tafadhari
Kiongozi pole sana. Hata mimi nimekata tamaa, kwani naishia kuliwa salio langu kila nikitaka kujiunga! Nimefanya kama ulivyofanya wewe lakini naambiwa namba siri za ATM au Kadi siyo zenyewe. Nilienda pia tawi la CRDB nikajaza zile fomu zao na kuambiwa nisubiri nitatumiwa SMS, lakini ni wiki ya pili sasa hamna kitu!
 
Hawa jamaa hii huduma yao itakua tu haina maana hapa nimemaliza vocha ya elfu 2 kila cku nahangaika kuunga duh
 
Nachokumbuka, nilitumiwa sms yenye password kutoka CRDB, ikinielekeza kwamba nibonyeze *150*03#. Kisha baada ya hapo nikaingiza namba ya siri niliyotumiwa kwa sms. Then nikapewa usajili wa muda, kwa kuwa sikuwa na kadi muda huo, kwa ajili ya kuchukua zile namba 16. Usajili wa muda unakupa access ya kuangalia salio tu. Usajili wa kudumu unafanyika baada ya kuingiza hizo 16 katika menu namba 3 ambayo inatokea ukibonyeza hizo namba hapo juu.
Hakikisha kwamba namba unayotumia kusajisajili kwenye sim banking ndio hiyo hiyo uliyoisajili CRDB (wanayokutumia taarifa zao)
 
Itanibid nifike kwao kwani mm nilijiunga pasi na kufika kwao ndio nikapata usajili wa muda nahisi nakosa hiyo namba ya siri toka kwao crdb,ahsante ndugu
 
Kiongozi pole sana. Hata mimi nimekata tamaa, kwani naishia kuliwa salio langu kila nikitaka kujiunga! Nimefanya kama ulivyofanya wewe lakini naambiwa namba siri za ATM au Kadi siyo zenyewe. Nilienda pia tawi la CRDB nikajaza zile fomu zao na kuambiwa nisubiri nitatumiwa SMS, lakini ni wiki ya pili sasa hamna kitu!

Ni rahisi mno.

Nenda tawi lolote, jaza form. Haichukui hata dakika tatu.

Within 3 days utapata sms, inatakiwa uwe na ATM card kwa ajili ya kuingiza zile namba (Sio account namba), zipo katikati ya card.

Utapiga hiyo *150*03. Itaingiza utaingiza namba then password, uta change password then confirmation follows.

Mimi nimejiunga last week. Hata NBC mobile imenichukua siku tatu tangu nilipojaza form!
 
Nimeeleza kuwa nimeenda tawi la CRDB hapa kwetu na kujaza hizo fomu, sasa inaingia wiki ya tatu hakuna cha sms wala nini! Kila nikipiga hizo namba ninafuata maelekezo yote, lakini ikifika hatua ya mwisho naambiwa namba ya siri ya ATM au Kadi imekosewa! Kwa taarifa yako ni kwamba nilikuwa natumia huduma hii hapo nyuma hadi nilipo "swap" line yangu. Kurejesha huduma hiyo ndiyo ngolani!
 
Inaelekea we unapenda ligi..............
 
Sasa unapomwambia mtu kwataarifa yako what does it mean na nauliomba usaidiwe, unapewa maelekezo then wewe ndio unakua mjuaji tena. Wakata kumbe hata uzi wako haujitoshelezi kimaelezo. Si kila alie humu ni great thinker so inaweza ikawa na wewe ni mmoja kati yao.
 
Binafsi nilitaka nitoe maelekozo namna nilivyo fanikiwa ila kwakuwa wewe unajua zaidi wacha nipige kimya.
 
Nimeeleza kuwa nimeenda tawi la CRDB hapa kwetu na kujaza hizo fomu, sasa inaingia wiki ya tatu hakuna cha sms wala nini! Kila nikipiga hizo namba ninafuata maelekezo yote, lakini ikifika hatua ya mwisho naambiwa namba ya siri ya ATM au Kadi imekosewa! Kwa taarifa yako ni kwamba nilikuwa natumia huduma hii hapo nyuma hadi nilipo "swap" line yangu. Kurejesha huduma hiyo ndiyo ngolani!
Mkuu lililokupata linafanana na la kwangu. Mimi nawali nilijiunga na Simbanking kupitia laini yangu ya Tigo. Hivi karibuni Tigo wanajua walichofanya kwani laini za watu nyingi tu zilijikuta hazifunguki ikiwemo ya kwangu, mara baada ya SWAP line yangu sasa siwezi kupata huduma ya kuangalia salio kama awali, isipokuwa naweza kupokea taaarifa za miamala niliyofanya tu.

Nilipowapigia CRDB Huduma kwa wateja walinifahamisha vizuri tu kwamba, nyuma ya kadi ya simu 'sim card" kuna namba ambayo kwa kutumia mfumo wao wanaiona kuwa imebadilika. Hivyo walinishauri kwenda kwenye tawi lolote la karibu ili ku-update taarifa zangu tu.
 
Kiongozi nimetoka tawi la CRDB hapa kwetu mkoani na kukutana na kijana ambaye ni mweleweshaji makini na kufanikiwa kujiunga hapo hapo! Nilichokuwa ninakikosea ni ile namba ya ATM kuirudia mara ya pili badala ya kuandika nyingine kabisa. Baada ya kupata menu (*150*03#), namba ya siri ya ATM ni ile ambayo tunatolea pesa kwa kutumia card. Namba ya kadi ni zile namba nyingi ambazo zipo mbele ya kadi. Ukitakiwa kuingiza namba mpya, inabidi uandike namba ya siri tofauti na ile ya ATM. Kisha unathibitisha namba hiyo tena na hapo utapata sms ya kupongezwa kuwa umejiunga na sim banking na unaelekezwa uende kwenye Mtandao wao kwa huduma zingine zaidi! Kwa maana hiyo kunakuwa na namba za siri mbili; moja ya ATM na nyingine kwa ajili ya mobile banking.
 
Mkuu ahsante kwa taarifa...
 
Habari zenu wakuu,

Jamani naomba kuelekwezwa jinsi yakutumia simu bank hasa katika kutoa pesa, kama unajua plz usipite bila kuweka maelezo yako.
 
Back
Top Bottom