Naomba Mchango wa Mawazo, Nahisi Hatukutendewa Haki!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Mchango wa Mawazo, Nahisi Hatukutendewa Haki!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by NasDaz, Mar 28, 2012.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Nina mdogo wangu wa kiume ambaye amemaliza kidato cha nne 2011. Hata hiivyo, nahisi kama hakutendewa haki kutokana na shule ambayo amepangiwa kwa masomo ya kidato cha tano na sita. Pamoja na kufanya vizuri mtihani wa kidato cha nne kwa kupata Division I Point 16, huku akiwa na Physics C, Chemistry A, Mathematics A na Biology C; bado kwa masomo ya kidato cha tano amechaguliwa kwenda shule ya “kata” (Chang’ombe Day) kwenda kusoma PCB!! Dogo, ambae hata miaka 18 hajafika (anatimiza August) amekuwa very disappointed hasa akizingatia wenzake ambao ama wamefanya vizuri sawa nay eye na hata waliofanya vibaya kuliko yeye wakiwa wamechaguliwa shule mzuri (angalau kwa majina)!! Mbaya zaidi, kwa zaidi ya miezi miwili sasa, tayari ameshapiga tution za Advanced Mathematics na Physics kwavile alitarajia kwenda PCM Boarding School! Leo hii anaambiwa aende PCB. Binafsi, sina matatizo na PCB na tangu zamani nilikuwa namshawishi sana asome PCB lakini alikuwa anakataa katakata na kutamka bayana kwamba ana “mahaba ya dhati” na Maths!

  Kwa jinsi ilivyo nafahamu itatuwea ngumu kumwamisha toka Chang’ombe kwenda Boarding School au shule yoyote iliyo nafuu kuliko Chang’ombe ambayo kwa matokeo ya mwaka jana (A-Level), hawakuwa na One hata moja, bali TWO chache. Division III, IV na Zero ndizo zilitapakaa pamoja na shule hiyo kuwapo kilipo Chuo Kikuu cha Ualimu!!! Mbaya zaidi, hakuna pesa ya kumpeleka Private School. Hivyo basi, ushauri ninaoomba kwa wadau, je nini nafuu kati ya kumwacha hapo hapo Chang’ombe au kumpeleka DIT ( Dar Tech)?! Binafsi, nilikuwa nafikiria kufanya mpango wa kumtoa Advanced School (Chang’ombe) na badala yake aende Dar Tech ili akamilishe ndoto zake za kusoma ama Computer au Telecommunication.

  NAWAKILISHA!
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa kama shule za boarding zimejaa wangemuweka wapi?

  Nyie kama mnaona kwa kumhamisha mtakua mmemsaidia kufanya kile anachopenda yeye ni vizuri mkafanya hivyo ili asije akapoteze interest darasani kwa kusoma mambo ambayo binafsi hayajamkaa moyoni.
   
 3. d

  dr chris Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwakweli inasikitisha sana na sidhani kama shule aliyopangiwa hata ilikuwepo kwenye uchaguzi wake hata hivyo mi nadhan kwenda adva.ni bora kinachobaki ni jitihada binafs itatakiwa.kwa ushauri zaidi nakushauli peleka hoja hi kwenye jukwaa la elimu kwani naamini kule kuna wadau wenye uzoefu na wamejaliwa hekima ktk kushauli mambo.
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  muulizen vizuri alijazaje sel form zake huenda amapangiwa kutokana na machaguo yake na si vinginevyo
   
 5. k

  kamili JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Kuna vitu vimejificha hapo. Maana nimejionea walifauli chini ya hapo wamepata shule nzuri tu za Boarding. Hebu naomba jina lake liweke wazi.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,130
  Likes Received: 6,615
  Trophy Points: 280
  Mwache aende kuripot aone walimu hakuna umfanyie uhamisho. kosa lako umehamaki kitu ambacho hata kwake ataona kama ni kibaya.
   
 7. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Sa kwa points hzo we ulitaka apangwe wapi labda?
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Tangu lini mtu anayehamaki akaomba ushauri?! Au kuhamaki hapo kupo wapi?! Mie nimesema interest yake ilikuwa kusoma PCM na amefaulu vizuri hiyo PCM na tayari ameshapiga tution ya hayo maswali; sasa kuhamaki kupo wapi hapo?! Au kusema hakutendewa haki kwako ni kuhamaki?! Ukweli bado unabaki pale pale kwamba Chang'ombe ni sawa na shule ya kata...mwanafunzi anapopiga book na kufaulu vizuri anatarajia kwenda kwenye shule mzuri....pamoja na mambo mengine, kwake hiyo ni reward ya jitihada zake!
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hebu toa angalizo hapo kwenye red! Ni vitu gani hivyo unavyohisi vimejificha?!
   
 10. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  ushauri wangu mpeleke Dar Tech aanze mapema safari ya kutimiza ndoto zake. Sometimes form 5 na 6 ni mbwembwe na kupoteza muda tu.
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  In short, hakujaza Chang'ombe....!!
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Shule ambazo wenye pass kama zake, tena wengine wenye pass ndogo kuliko yeye wameenda! Shule kama vile Pugu, Minaki, Azania, Moshi Tech and the like....hata kama nazo zimebaki majina; lakini social satsfaction inaweza kumfanya afanye vizuri zaidi. Hata kama zimebaki majina, lakini kukutana na watu wenye uwezo sawa na wake kunaongeza competition!
   
 13. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Pambana umhamishe. Japo utasumbuka sana kutokana na udhalimu wa maafisa elimu, makarani na wakuu wa shule
   
 14. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  uhamisho unawezekana tafta shule yenye nafasi then mkuu wa hyo shule aandike barua kuwa kkuna nafasi nenda shuleni alikopangiwa watakupa barua then maafsa elimu ukiongea na wakuu wa shule mambo yatakuwa rahisi kumbuka mkono mtupu haulambwi lkn
   
 15. +255

  +255 JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Kumuamisha mbona inawezekana, mwache akaripot huku mnashughulikia uhamisho., moja ya sababu ya uhamisho iwe amepangiwa day na dar hana ndugu wa kuishi nae. Kuna mdogo wangu alishawahi kuhama kwa mtindo huo ila ye ilikuwa O'level
   
 16. M

  Mbundenali Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kufanya vizuri ni jhd ya m2 binafsi. Usibabaike na jina la shule. Hata hizo shule kubwa huwa wanafeli kama kawaida. Na hizo shule za kata huwa wanafaulu. wizara hupanga wnfnz f5 kutokana na mahitaji ya shule mbalimbali nchini. Usidharau hiyo shule mdogo wako akaiona haifai halafu akafeli f6. Mwache apige kitabu hapo hapo
   
 17. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  HAPA KUNA OPTION MBILI YA KWANZA KAMA ANATAKA KUSOMA PCM NI SAWA NA KWA MATOKEO YAKE ASIKATE TAMAA NA KWA VILE MKO DAR HIYO ITAKUWA RAHISI KIASI KWA POINT ZAKE KWENYE PCM =CAA AMBAZO NI 3+1+1=5 kwa matokeo hayo na div aliyopata anastahili kupata shule nzuri walau kwa maijna hapa nadhani ulikuwa unataka kusema shule kama PUGU,MINAKI, AZANIA,TOSAMAGANGA ,TANGA TECH, MOSHI TECH, OLD MOSHI NK.. na hapa naungana na wewe ukitazama ufaulu na cutoff point ambazo wamechukua kwa mfano kwa combination ya PCM MINIMUM NI POINTS KUMI =10 KWA MAANA YA MTU MWENYE CCD ANAPATA SHULE ... SASA CHAKUFANYA YEYE ANAWEZA AKAANZA HAPO CHANG'OMBE AMA UKAANZA KUFUATILIA UHAMISHO KWENYE HIZO SHULE NILIZOKUTAJIA KWA KUWA ATLEAST HUWA ZINA MATOKEO MAZURI KIASI KWENYE COMB ZA SCIENCE ... KWANI UKITAZAMA WAZAZI WENGI AMBAO WATOTO WAO WALISOMA SHULE ZA PRIVATE AMBAO WATOTO WAO WENYE MATOKEO KAMA MDOGO WAKO HUWA WANAWARUDISHA PRIVATE SCHOOLS KUTOKANA NA HALI HALISI SHULE ZETU ZA SERIKALI KWA HIYO UNAWEZA TUMIA HUU MWANYA KWA MDOGO WAKO KWENDA HIZI SHULE kwa kufill haya magap ambayo wanafunzi huwa hawarepoti mashuleni
  LA PILI LA KUMPELEKA DIT INABIDI MSHIRIKISHE NA YEYE UONE MTAZAMO WAKE
  asikate tamaa nafasi bado ipo atapata shule tu ana matokeo mazuri inategemea tu upangaji wa shule
  NAWASILISHA .....
   
 18. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,097
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  hii key point sana ndugu yangu tunajua maana ake wengine
   
 19. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kaka mimi binafsi siamini kama shule ni kigezo cha mtu kufanya vizuri katika mitihani sanasana hizi shule za serikali zote ni sawa tofauti ni majengo na maeneo zilipo pia idadi rukuki ya walimu watoro na wasio kuwa na dhamira ya kusaidia wanafunzi.

  Labda niende kwa mifano utanielewa, mfano wa shule zinazofanya vizuri kwa hapa Dar katika masomo ya sayansi ni kama hakuna ila kuna baadhi ya wanafunzi wa sayansi hizo hizo shule za serikali wanafanza vizuri kuwazidi hata wa huko boarding schools, so it all about self commitment. Mwambie dogo ajitume na kwa kuwa ameshasoma hayo masomo ni rahisi kufanya vizur ila zaidi na zaidi asome sana past papers na ajue syllabus ya sasa iko vipi. Pia apende sana kufanya mitihani katika vituo vyenye ushindani kama kwa MANYILIZU na penginepo. Kingine kuama combination ukiwa shule ni kitu kirahisi kwa hilo asiwaze chochote na namshauri asome PCM just the way he wanted.

  Mwisho, ningependa nikushauri na wewe pia kuwa usikariri maisha, kwakuwa umeshazoea kuona shule ina vilaza basi hutaki mabadiliko katika hiyo shule, huyo mdogo wako ndio anaweza kwenda kuweka hiyo heshima katika hiyo shule na akafanya wanafunzi wenzake wenye kujitambua kupata ushindani na wakafanya vizuri wote kwa ujumla. AENDE HAPOHAPO CHANG'OMBE NA USIMPOTEZEE MDA WAKE KUANZA KUFOCUS KWENYE KUHAMA NA KUACHA MAJUKUMU YAKE YA KIMSINGI YA KUSOMA.
   
 20. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Thanx for contribution.....i'll work for it! kuhusu kumshirikisha dogo kwenda DIT; hapo hakuna tatizo sana kwavile tumeshawahi kuyaongea haya mara nyingi sana tangu akiwa kidato cha tatu! In short, huyu ni zaidi ya mdogo, ni rafiki yangu na kila m2 home anafahamu hilo....mie ni mentor wake! Tangu akiwa form III, yeye interest yake ilikuwa kwenda DIT, nikawa najaribu kumwuliza ni kwanini anapenda DIT kuliko A-Level! Alitoa sababu za msingi sana ambazo kwa mzazi mwenye akili hawezi kuzipuuza! Hata hivyo, nilikuwa najaribu kumpa faida na hasara za kwenda DIT/A-Level. Ni baadae sana alibadilisha mawazo na kuamua kutaka kwenda A-Level. Hata hivyo, nitaanza kuufanyia kazi ushauri wako wa awali wa kuanza kufuatilia shule ulizozitaja!
  Thanx mkuu!
   
Loading...