Mtu hujikuna anapopafikia!
Tajiri hakusanyi michango ya harusi. Huwezi kusikia Jay Z anaomba mchango wa harusi.
Kijijini mzee mwenye uwezo wake akifanya shughuli ya mwanawe kijiji kizima kitatingishika lakini haombi mchango wa harusi.
Ngoma iko kwa makabwela wa mjini. Holi la harusi milioni kumi. Bwana harusi elfu kumi benki hana.
Hapo ni mwendo wa michango. Yaani michango kiasi utamkuta mtu anakuhesabia michango ya harusi ni sehemu ya matumizi yake ya mshahara.
Ujinga tuache. Una milioni 30 yako unataka kuitumbua siku moja kwenye harusi. Fanya harusi alika watu waje na zawadi tu.
Ingekuwa la maana mtu akikwama ada ya shule mwaka wa mwisho achapishe kadi kwa ndugu na jamaa wamsaidie. Na anaweza kupanga siku watu wakaja na michango yao kukawa na tafrija ndogo na vinywaji watu wakafurahi.
Si tunaiga wazungu? Wenzetu wana rent party. Mtu akikosa kodi akiwa karibu kufukuzwa kwenye nyumba wanafanya pati michango inakusanywa mwenye shida anasaidiwa.
Utafikiri wabongo sio wabunifu. Ni wabunifu mno ila kwenye vitu vya hovyo hovyo. Utakuta bwana harusi kavalishwa gagulo la mtemi Mirambo, kilemba cha Tippu Tip bado gobore tu afanane na muuza watumwa. Wengine wanavaa makoti ya kuendeshea meli yaani tafarani mtindo mmoja. Kesho asubuhi bwana na bibi harusi wana madeni na kodi ya nyumba hawana.
Ushauri wa bure tufanyeni harusi ndogo halafu tuwe na utaratibu wa kuwakabidhi maharusi zile pesa za michango ili ziwasaidie kuanza maisha.