Naomba mawazo yenu, sielewi hatma ya maisha yangu

Naomba mawazo yenu, sielewi hatma ya maisha yangu

beny jr

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2018
Posts
864
Reaction score
1,182
Naomba niende kwenye mada moja kwa moja mimi ni mtoto wa mwisho katika familia yetu nimezaliwa mwaka 1994 lakini maisha yangu sielewi nakosea wapi mpaka umri huu (utapiga heaabu nimekutajia mwaka niliozaliwa) bado ramani ya maisha yangu siijui story ipo hivi mimi ni mtoto wa mwisho kwenye familia yetu mama yangu alipoteza maisha baada ya kujifungua mimi.

Kwa taatifa zilizopo ni kuwa alipata kifafa cha uzazi sina uhakika na hilo ila sijamuona mama yangu nililelewa na bibi na bibi alinambia alikua ananipa nyonyo lake alinikuza mpaka miaka mitano ndo akanipeleka kwa baba, baba yangu alikua mfanyabiashara mkubwa uhindini iringa ingawa mimi nimezaliwa tukuyu mbeya na nimekulia huko mpaka miaka yangu hiyo mitano baada ya kuja kumjua baba iringa baba alinipenda sana ingawa alikua ameoa mke mwingine ilibidi niendelee kukaa na bibi kwakua mama wa kama kule upande wababa nadhan baba alimdanganya hana watoto so ilikua ngumu kuishi kule na baba alikua anakuja mlandege kuniona na kunipa mahitaji yote bila shida ila mwaka 2000 aliaga dunia nae (R.I.P dad).

Bibi alinilea mpaka umri wa kujitambua ila cha kushangaza bibi alikuja kunichukia balaa sababu ni sizijui ila kuna story bibi aliachana na babu akampata mwanaume mwingine ambaye alikua mtumishi wa bank ya posta na hakumwambia kama anawatoto nje kumbuka bibi yangu alikua amefanikiwa kupata watoto wanne na babu yangu Mr Joseph bukuku ambaye amefariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 102 na hao ni mama yangu na wajomba watatu sababu ya kunichukia ni kuwa ilikua haiepukiki kuniacha mimi kwaka ndugu walisema mimi ni lazima nilelewe na yeye sasa akanichukua inavyoknekana nilileta mgogoro mkubwa kwa mwanaume wake mpya ambae alifanikiwa kuapata watoto wa wili wakike ambao majina yao nayahifadhi sasa wakawa mama zangu wadogo.

Maisha yaliendelea huyu mzee akahamishiwa mafinga posta kwa hiyo tukahamia wote ndipo nilipoanza darasa ya kwanza katika shule ya msingi mkombwe mafinga kumbuka shule walipewa kipaumbele watoto wa mama zangu wadogo mimi niliachwa nyumban lakini kwakua nilikua mnene sana nakuonekana naumbile kubwa sikupenda nishinde nyumbani nikawa naenda mkombwe kuangalia wanafunzi wenzangu ndipo mwalimu mmoja namkumbukaga sana ambae ndiye alibadirisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa mnoo story ya huyu mwalimu ni ya kusisismua sana anaitwa mwalimu mgitu.

Nikaanza kuingia darasan bila hata kusajiliwa siku moja wanafunzi wanaitwa waliosajiliwa jina langu halipo ndipo huyu mwalimu akanihoji ikabidi aniandikishe hapo hapo jina nililosajiriwa linanitesa mpaka kwenye cheti changu cha kuzaliwa na other academic certificate.

Maendeleo yangu ya kitaaluma yalikuwa mabovu sana tena sana kati ya wanafunzi 198 mimi nilikua nashika namba 196 au 197 wa mwisho alikua kijana mmoja ambae ana pesa sana mafinga pale anaitwa Joshua (sio jina halisi) ambaye sasa anahela vibaya mno na mtu aliyekua anatuongoza anaitwa janet huyu ni CPA holder na ni mhadhili chuo cha Ardhi maendelo ya kitaaaluma yalianza kuonekana darasa la sita nimeandika.

Hili kuomba ushauri story yangu ni nzito sana nilipo sasa na mafanikio yangu hayaendani kabisa na umri wangu story hii itaendelea, mambo yatakayozngumziwa baadae ELIMU NILIYOFIKIA SASA JE NILIFANIKIWA KUFIKA CHUO KIKUU? AU LA JE JOSHUA NA MIMI NA JANETH TUPO KATIKA LEVEL SAWA NTAKUJA KUELEZA YOOTE subscribe story yangu utajifunza na kunipa ushauri kuna mahali nilikosea kama binadamu ila sijui narudije kwenye mstari
 
Pole sana, japo nami sio mwandishi mzuri ila we umezidi.

Umeacha kusimulia kilichokutokea baada ya baba kufariki, kuishi na bibi ilikuaje?kwanini bibi alikuchukia nini kilitokea? Hauwezi kuwa haujui labda kama hautaki kusema inawezekana wewe ndio mkosaji.

Umerukia kuandika maisha ya watu

Pole kwa uliyopitia.
 
Nenda machimboni ukachimbe Tanzanite huko unaweza kulala masikini na kuamka tajiri
 
Pole sana, japo nami sio mwandishi mzuri ila we umezidi.

Umeacha kusimulia kilichokutokea baada ya baba kufariki, kuishi na bibi ilikuaje?kwanini bibi alikuchukia nini kilitokea? Hauwezi kuwa haujui labda kama hautaki kusema inawezekana wewe ndio mkosaji.

Umerukia kuandika maisha ya watu

Pole kwa uliyopitia.
Stay tuned kuna jambo mbele mkuu
 
Pole sana, japo nami sio mwandishi mzuri ila we umezidi....

Umeacha kusimulia kilichokutokea baada ya baba kufariki, kuishi na bibi ilikuaje?kwanini bibi alikuchukia nini kilitokea? Hauwezi kuwa haujui labda kama hautaki kusema inawezekana wewe ndio mkosaji.
Umerukia kuandika maisha ya watu
Pole kwa uliyopitia.
mleta mada pamoja na kutaka kutupia lawama wengine ila inaonekana yeye mwenyewe kwanza ana matatizo
 
Watoto wanne ukadanganye mwanaume haujawahi kuzaa?!

Wanawake wengine wana guts za ajabu mno
 
Hatma ya maisha yangu sielewi naomba msaada wa mawazo yenu JF
Mdogo wangu, hatma ya maisha yako ipo mikononi mwa Mungu. Humu JF kuna watu wana mitihani ya kutisha sana.

Mimi ninapitia mambo mazito sana katika maisha yangu sasa hivi lakini I LOOK NORMAL on the outside. Ninapambana nikijua haya yatapita tu kwa nguvu za Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom