Kwa hapa nchini tunapenda kupanga njia zilizonyooka-hivyo diploma ya IT lazima uanzie certificate (levels 4, halafu 5 na mwisho diploma level 6). Kama unaufaulu mzuri F4-basi waweza piga certificate ya Accountancy, halafu ukatumia cheti hicho hicho cha F4 kuomba certificate ya IT hadi Diploma au Diploma direct (DIT na AT) ambayo wanachanganya level zote 4,5 na 6.
Unaweza pia kufikiria kusoma Certificate na Diploma ya Business Information Technology ya UCC ambayo inachanganya courses za IT, Accounting, Finance na masomo mengine ya biashara.