format na maanisha bwana HEKIMA na GKM
Okay format yake huwa kama hivi ifuatavyo. Nitaweka namba kuashiri ndio kinachoanza mpaka mwisho na natumai itakuwa msaada kwako kaka mkuu.
1. Utaanza na anuani yako (adddress) ambayo hii itakaa upande wa kuliwa wa karatasi yako ya barua ya kazi. Na vitu vya kuzingatia ni jin lako kamili, sanduku la posta, mjini, nchi, na utamaliza na namba zako za simu pamoja na barua pepe kama utakuwa nayo.
2. Utaandika anuani ya sehemu unayopeleka hiyo barua yako. Kwa mfuatano kama wa namba 1 ila kumbuka tu kuwa hapo utaiandika barua inaenda kwa nani kwa kuandika cheo chake HR, GM, CEO nk. NB: hii itakaa upande wa kushoto
3. Utafungua barua kwa kuandika Dear sir/ madam / ambayo utaandika chini ya anuani ya ofisi chini japo ruka mstari mmoja.
4. Kichwa cha habari ambayo inakuwa na YAH: au ref: kwa lugha ya kiingereza na utaandika dhumuni lako katika kichwa hicho cha habari.
5. Utaandika barua yenyewe chini ya kichwa cha habari. Kumbuka kuanza kwa aya kwa kila jambo lenye uzito aidha unaelezea sifa yako au elimu au jambo lolote lile.
6. Ni Saini yako ambayo itakaa upande wa kushoto wa aratasi yako
Nadhani kwa uchache utakuwa na official letter nit and clear kwa maudhui uliyolenga. Hope itakiwa msaada japo kwa uchache. Asante.