NAOMBA KWA MH RAIS JUU YA MADEREVA NGAZI YA DARASA LA SABA

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,565
8,427
Awali ya yote napenda kumpa pongezi kubwa Mh Rais kwa kazi nzuri sana anayoifanya hapa nchini,sitazungumza sana mazuri mengi kwa kua sikuja kuyasema hayo kwa leo,nipo hapa kutoa maombi kwake na kwa serikali kwa ujumla juu ya utendaji kazi ktk sekta zake kwa kada ya MADEREVA

1. MH RAIS
Kwanza kabisa kazi ya dereva kubwa ni kuendesha gari husika alilokabidhiwa kazini na kufuata maelekezo tu ya mabosi wake pale wanapomhitaji katika utendaji.

2. MH RAIS
Pamoja na kwamba kuna kazi zinazomhusu dereva pamoja na kuandika report ya gari lake au hata kuongezewa kazi za kukimbizana huku na kule ili shughuli za maendeleo ziweze kwenda lakini bado mala nyingi zitakua kazi za kupeleka bahasha mahala na kukimbia kutoa eidha copy ya makaratasi na kurudisha ofisini,kitu ambacho kimsingi mtu wa darasa la saba anaweza kuifanya

3. MH RAIS
Hawa madereva darasa la saba ni wengi sana na kimsingi siku zote wamekua ni wenye weredi na ujuzi mkubwa sana wa kazi katika maofisi nikiwepo na mimi hapa ninae andika haya.tumekua wazoefu wa kazi za field na kukimbia mikoani huku na kule bila mawaa yoyote,nidhamu utendaji na uoga kwa maboss imekua sehemu ya kuifanya kada hiyo ya madereva iweze kwenda vyema.

4. MH RAIS
Pamoja na kwamba sitaki kuombea mabaya juu ya madereva watakaoingia sasa lakini yamkini kukaibuka ajali na uharibifu wa magari baada ya muda hapo mbele,sababu ni moja tu.tutakua tumeajili kidato cha nne na si weredi na uzoefu mkubwa wa kazi na hofu ya utendaji ambayo imeendelea kufanya mali za serikali yaani hayo magari kua salama pamoja na hizo ajali kadhaa ambazo hua zinatokea kwa sababu mbali mbali lakini si kwa kiwango kikubwa sana cha kutisha.

5.MH RAIS
Ninafikili wazi kwamba,mtu wa darasa la saba na mtu mwenye elimu ya kidato cha nne hawapishani sana kufikiri kwao na hawapishani sana kiutendaji ilihali pia ukizingatia utendaji mkubwa kwao ni kuendesha gari tu,walipaswa kuchanganywa kwa pamoja na idara ziwasaidie wote kupata kozi zinazoweza kujenga ujuzi zaidi na umahili ktk kazi kupitia vyuo vyetu vya taifa VETA na hasa NIT ambazo zimekua msaada sana kwetu madereva.

6. MH RAIS
Sina uzoefu na huko serikalini lakini binafsi nimekua dereva wa shirika lisilo la kiserikali kwa muda wa miaka 7 na nimekua na watu wa darasa la saba hata kama hawajisemi lakini wamekuwepo wengi na utendaji wao sikuwahi kuukosoa hata kidogo,wameendesha magari kwa weredi mkubwa,wamepata mafunzo pale NIT ambayo yalileta matokeo mazuri kabisa,office iliweza kuwapa elimu kidogo ya kutumia laptop na kujiandikia report zao na kumbukumbu zao ktk utendaji wa kila siku na kazi zilikua zikienda vyema.

7. MH RAIS
Kumekuwepo na chuo cha VETA toka miaka mingi hapa nchini kwetu,na lengo kuu yamkini lilikua ni kuwajengea uwezo vijana wote walioishia darasa la saba kwa kuwapa elimu ya kujitegemea kama ufundi na huo udereva.pale waliposoma udereva inawezekana kabisa walisoma ili waje waajiliwe pamoja na kwamba si lazima kusoma ili kutengeneza kuajiliwa tu badala ya kujiajili.lakini ukweli mtu alieenda VETA mala nyingi si mtu anaesoma na kujiajili kwa maana ya kukosa mtaji.wengi wamesoma udereva ili wakiona ofisi zinatangaza nafasi za madereva waweze kuomba kazi maana zimekuwepo siku zote.nje na hivyo pasingekua na umuhimu wa chuo hiki kuweka kozi hizo,isipokua zimekuwepo maana tulijua kuendesha gari hapakuangali elimu ya kidato cha nne au six au diploma na degree.

8. MH RAIS
Ushauli wangu ni kwamba (i) Darasa la saba ni raia wa nchi hii na hawana pa kwenda (ii)wanao uwezo wa kuendesha magari na wanajua kusoma na kuandika pia.hivyo basi Mh Rais na idara zote za serikali ningeomba popote muonapo bandiko langu mimi kama mwananchi hulu ninaeipenda Tanzania,waTanzania na Africa kwa ujumla,MUNGU awaongoze kwa hekima kuwatambua watu ambao hawakuendelea na elimu za juu na mimi binafsi ninaomba ladhi badala yao kwa kutoweza kuendelea na masomo pale tu walipomaliza darasa la saba kwa sababu mbali mbali,eidha za uzembe au ukosefu wa wazazi wa kutokujua umuhimu wa elimu au kwa kukosa uwezo wa kifedha na kifikla juu ya watoto wao ambao leo hii ni madereva wa magari na wanategemea kujikwamua kimaisha kupitia kazi hiyo.

MH RAIS
Chonde Chonde: niko chini ya miguu yako badala ya hawa ndugu hata kama hawajanituma lakini ninajua maumivu yao maana ninao mtaani na vijiweni katka kutafuta tonge la watoto,kilio chao kinasikitisha.
Ninaomba uwafikilie kwa upya na wakiomba kazi tena uwapokee lakini pia walau idara hizo hizo zitakazowapokea ziwasaidie kupata elimu ya udereva hata kwa kukopeshwa ada na wakakatwa taratibu ktk mishahara yao.ninaamini kwa kazi hiyo ya kuendesha magari wanaweza kama ambavyo wameweza kwa miaka mingi iliyopita na hata leo.tusaidie mkuu ili tuweze kulea familia zetu,watoto wetu waweze kwenda shule na wasije kukutana na hali ya namna hii kama ya wazazi wao wa sasa.
........AHSANTE.....
Ndimi mwananchi hulu na mpenda maendeleo
.........G F MASSEBU wa Mwanza Tanzania.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Falsafa ya sheria ina kanuni moja ya msingi kabisa inayofuatwa karibu sehemu zote duniani,hususan kwenye mifumo ya "common law" kama kwetu.

Kanuni hiyo kilatini inaitwa "ex post facto". Ina kiini cha msingi kinachosema kwamba, sheria inayotungwa leo, isihukumu watu waliofanya kosa kwa mujibu wa sheria hiyo kabla ya sheria hiyo kukubaliwa.

Kama leo tunatunga sheria kwamba kula Maharage ni kosa la kufungwa miaka 30 jela, tukiweka sheria leo, iwe kwamba anayehukumiwani yule anayekula maharage leo na kuendelea mbele.

Ukimhukumu aliyekula maharage juzi kwa sheria iliyotungwa leo, utakuwa unamuonea, kwa maana hakujua kwamba kula maharage ni kosa, sheriailikuwa haijatungwa bado.

Hawa madereva wa darasa la saba,hizi kanuni za kutaka kuwaondoa zimewekwa lini?

Kamamtu kaendesha gari vizuri miaka kumi kwa elimu yake ya darasa la saba, anakaribia kustaafu, kumfukuza kazi kwa kanuniiliyowekwa jana si kumuonea?

Kamaserikali inataka madereva wasomi, kwa nini isiseme kuanzia sasa kwenda mbele tunataka madereva wote wapya wawe na elimu ya kidato cha nne, ila waliopo tunawaacha kwenye ajira?
 
Mkuu elimu ya kidato cha nne ndiyo kigezo cha ajira serikalini
Nini maana ya elimu ya msingi basi kidato cha nne iwe ndiyo kiwango cha chini cha elimu kwa wote.
Hayo yote ikiwa na vyeti vyeki ni mbinu za kupunguza wafanyakazi na ukiangalia hakuna uwiano kwa waloondolewa na wanaoajiriwa.
 
Ndiyo mkuu, jirani yangu alipata kazi ya upishi hospitali, ilibidi afanye mitihani ya kids to cha nne na wajukuu.
Habari hiyo ni kinyume na katiba, katiba (ibara ya 9 na 11) inasema kila mtu ana haki ya kupata ajira kwa mujibu wa uwezo wake.

Mtu wa darasa la saba mwenye uwezo wa kujua kusoma, kuandika na kuendesha gari vizuri ana uwezo wa kufanya kazi ya udereva.

Ukimuwekea kizingiti cha kidato cha nne kwenye kazi ya serikali ambayo haihitaji elimu hiyo, unamkosesha kuwa na ajira kwa namna ambayo inavunja katiba ya Tanzania.

Kibaya zaidi, ukimuajiri kwa elimuhiyo, akatumikia serikali miaka kibao, kisha ukamfukuza kama mbwa karibu anastaafu ndiyo unaharibu kabisa.

Wanasheria wa Tanzania wamelala. Hii ni kesi unaishitaki serikali mpaka mahakama za juu kabisa.
 
Mkuu elimu ya kidato cha nne ndiyo kigezo cha ajira serikalini
Hiki kigezo kilianza lini?why waliajiliwa awali?hapa hatupo kulajmiana tupo kutoa ushauli na kusaidiana kwamba wenzetu nao wapate ajira maana ni wananchi halali na wenye uwezo juu kazi husika
 
Elimu yenyewe ya Tanzania siku hizi aliyeishia darasa la saba na aliyepata Ph.D ya Kemia Magumashi hawana tofauti.

Wanawafanyia roho mbaya tu.
 
Back
Top Bottom