Natanguliza kusema kuwa mimi si mmoja wa waathirika wa magonjwa hayo.
Baada ya kusema hivyo, natamani kuiuliza serekali yangu hii tukufu inayoongozwa na mh JPM. Hivi inakuwaje wagonjwa wa Kisukari wanajitibu wenyewe tena kwa gharama kubwa (No subsidy) kwa dawa zao wala vifaa tiba vyao wakati HIV wanapewa matibabu ya hali ya juu bure?
Kisukari ni ugonjwa unaompata mtu yeyote bila hata taarifa wakati HIV huambukizwa kutokana na, naomba kumnukuu rais wetu mstaafu, Mh. JK; Kutokana na kiherehere chako. Mtu umegawiwa na zana za kinga hotelini bure, unatangaziwa kila siku kuwa uwe mwangalifu Ukimwi upo. Lakini kutokana na viherehere vyao watu wanajitumbukiza peku peku na kuupata huo ugonjwa. Serekali inatumia mamilioni kuwanunulia dawa za kuufubaza.
Hamuoni kuwa kama serekali hamtendi haki kumuachia jukumu hili mgonjwa wa Kisukari ajitibu peke yake bila msaada wa serekali?
Ni mawazo yangu tu lakini, kama kuna mhusika anieleze tu kuwa tatizo liko wapi kwani nadhani kutoka malaria, kisukari ndio kinachukua maisha yetu zaidi tena kwa uchungu mkubwa.