Naomba kuuliza, cement huharibika baada ya muda gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba kuuliza, cement huharibika baada ya muda gani?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tuko, Jun 17, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kama ikihifadhiwa vizuri bila kufunguliwa, cement inaweza kuwa useful kwa mda gani? Naomba wataalamu wanijulishe..
   
 2. NEGLIGIBLE

  NEGLIGIBLE JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Inategemea na mtengenezaji,jibu sahihi utalipata baada ya kusoma kwenye mfuko wa cement husika kwani ni lazima itaonyesha tarehe ya mwisho wa matumizi.........................kuharibika kwa cement sio kuganda tu,kwani inaweza ikawa haijaganda lakini isifae kwa matumizi kwani ubora wake utakuwa umepungua.............cement nyingi nadhani hudumu kwa miezi sita toka itengenezwe kama itahifadhiwa vizuri.
   
 3. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,808
  Likes Received: 2,583
  Trophy Points: 280
  Kwa hali ya kawaida utafiti umeonyesha:
  baada miezi 3 nguvu hupungua asilimia 20 hadi 30.8aada miezi 6 ni asilimia 30 hadi 40.Baada ya mwaka nguvu itapungua kwa asilimia 40 hadi 50.
  Ni muhimu kuhifadhi saruji pasipo unyevu wa aina yeyote unaotoka sakafuni,ukatani,bati au kutoka kwenye hewa.Nguvu ya zege hutegemea mambo kadha pamoja na nguvu ya saraji./wingi wa saruji katika mchanganyiko,usafi na wingi wa maji,kiwango cha mchanga na kokoto,ukorogaji na umiminaji,ukuzaji(curing) baada ya kumimina
   
Loading...