Nyahende Thomas
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 211
- 104
Ndugu wadau wa JF,
Wakati huu tunapojipongeza kwa kufanikiwa kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni, hususani chama mbadala CHADEMA, na baada ya kufahamu wabunge wateule wa viti maalum, basi naomba tuangalie mbele zaidi kwa kuutazama uchaguzi mkuu wa 2015 kwakuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, maandalizi ya uchaguzi wa 2015 ndio yamekwishaanza.
Baada ya kupitia majina ya wateule wa viti maalum, na kwa kuzingatia ujasiri na mfano wa kuigwa ulioonyeshwa na binti imara na jasiri mh.Halima Mdee, ninaomba kutoa hoja kwamba chadema iendelee kuwa mfano kwa vyama vingine na kwahiyo kujitofautisha navyo. Ushindi wa Halima Mdee kwa kiasi kikubwa umetoa hamasa ya kipekee si kwa wanawake au akina mama watu wazima tu, bali pia kwa wasichana wadogo kwamba nao wanaweza, kwani amekuwa ni mwanamke wa kwanza kushinda kiti cha ubunge kutoka chama cha upinzani kutokea jimboni.
Ni hamasa ya kipekee kwa wanawake kuweza kushiriki siasa si kwa kutegemea nafasi za kupewa ama kuteuliwa bali pia kwa kugombea majimboni na wanaweza kushinda na hata wasiposhinda lakini uwezo wao utakuwa umeonekana na kutambulika kama ilivyokuwa kwa Mh. Regia Mtema, alipambana kiasi cha kutosha hadi chama kimemuamini na kumpa nafasi kupitia viti maalum.
Kwa muktadha huo, ningependa kutoa ushauri kwa chadema au wabunge hawa wa viti maalum ambao wamekuwa wawakilishi wa wananchi kwa viti maalum kupitia chadema kwa muda wa miaka 5 na zaidi kuwa na mpango mkakati wa kujitokeza majimboni mwaka 2015 ili kuhakikisha kwamba chama kinakuwa na wagombea katika majibo yote nchini.
Kwa uzoefu walioupata na watakaoendelea kuupata, naamini kabisa wataweza kuwa ni chachu ya kipekee katika siasa za Tanzania na hatimaye chama chetu kitapata ushindi mkubwa zaidi kwa kuwa tunayo nafasi kubwa zaidi ya kuchukua uongozi wa nchi hii 2015.
Kwa heshima kabisa nawaomba waheshimiwa hawa wajiandae kwenda kugombea majimboni uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
1. Mh. Lucy Owenya
2. Mh. Suzan Lyimo
3. Mh. Grace Kiwelu
4. Mh.Muhonga Ruhwanya
Karibuni wadau kwa mawazo yenu,
Naomba kutoa hoja.