Naomba kutoa hoja, wabunge hawa wajiandae kugombea majimboni 2015

Nyahende Thomas

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
211
104
Ndugu wadau wa JF,

Wakati huu tunapojipongeza kwa kufanikiwa kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni, hususani chama mbadala CHADEMA, na baada ya kufahamu wabunge wateule wa viti maalum, basi naomba tuangalie mbele zaidi kwa kuutazama uchaguzi mkuu wa 2015 kwakuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, maandalizi ya uchaguzi wa 2015 ndio yamekwishaanza.

Baada ya kupitia majina ya wateule wa viti maalum, na kwa kuzingatia ujasiri na mfano wa kuigwa ulioonyeshwa na binti imara na jasiri mh.Halima Mdee, ninaomba kutoa hoja kwamba chadema iendelee kuwa mfano kwa vyama vingine na kwahiyo kujitofautisha navyo. Ushindi wa Halima Mdee kwa kiasi kikubwa umetoa hamasa ya kipekee si kwa wanawake au akina mama watu wazima tu, bali pia kwa wasichana wadogo kwamba nao wanaweza, kwani amekuwa ni mwanamke wa kwanza kushinda kiti cha ubunge kutoka chama cha upinzani kutokea jimboni.

Ni hamasa ya kipekee kwa wanawake kuweza kushiriki siasa si kwa kutegemea nafasi za kupewa ama kuteuliwa bali pia kwa kugombea majimboni na wanaweza kushinda na hata wasiposhinda lakini uwezo wao utakuwa umeonekana na kutambulika kama ilivyokuwa kwa Mh. Regia Mtema, alipambana kiasi cha kutosha hadi chama kimemuamini na kumpa nafasi kupitia viti maalum.

Kwa muktadha huo, ningependa kutoa ushauri kwa chadema au wabunge hawa wa viti maalum ambao wamekuwa wawakilishi wa wananchi kwa viti maalum kupitia chadema kwa muda wa miaka 5 na zaidi kuwa na mpango mkakati wa kujitokeza majimboni mwaka 2015 ili kuhakikisha kwamba chama kinakuwa na wagombea katika majibo yote nchini.

Kwa uzoefu walioupata na watakaoendelea kuupata, naamini kabisa wataweza kuwa ni chachu ya kipekee katika siasa za Tanzania na hatimaye chama chetu kitapata ushindi mkubwa zaidi kwa kuwa tunayo nafasi kubwa zaidi ya kuchukua uongozi wa nchi hii 2015.

Kwa heshima kabisa nawaomba waheshimiwa hawa wajiandae kwenda kugombea majimboni uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
1. Mh. Lucy Owenya
2. Mh. Suzan Lyimo
3. Mh. Grace Kiwelu
4. Mh.Muhonga Ruhwanya

Karibuni wadau kwa mawazo yenu,

Naomba kutoa hoja.
 
Na wengine woote wasaidiwe zaidi, na zaidi sana tuanzae mapeeeema kuwaandaa watu watakaong'oa wajeuri wote kutoka CCM

Anyway kwa kifupi wakati CCM wakishangilia wizi wao, Chadema tuanze kupanga mashambulizi ya mwaka ujao wa uchaguzi.
Kwa kifupi tu, Nimegundua kuwa Vijana wooooote na wenye uelewa sawasawa na wasiowanafiki wanaunga mkono chadema.

Hivyo ni kazi kwa Viongozi wetu kutuunganisha na kujenga safu bora ya ulinzi wa vijana hawa walio nyuma ya Chadema.
Umakini uchukuliwe tusije kuwa kama NCCR mwaka huo.

Ni kwamba kwa sasa Chadema ndo kinashikilia nchi kwa sababu wasomi, vijana wote wanaunga mkono. Je tuseme CCM bado ipo na wazee wake, pamoja na hao wachache wanafiki waliobaki. A BIG NO!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wapiga kura wengi uchaguzi mkuu ujao watakuwa ni vijana waliozaliwa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi vya siasa na wameshuhudia namna chadema ilivyosimamia hoja zenye maslahi kwa taifa hili na kwa kuwa ccm haina agenda inayowagusa vijana basi chadema ndipo inapata nafasi kubwa ya uungwaji mkono. Nakubaliana nawewe kwamba chama kiandae mikakati ya kuandaa vijana wengi zaidi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi hii kuanzia serikali za mitaa 2014. Baada ya hapo tutaingia kwenye uchaguzi mkuu 2015 kwa kishindo kikubwa na kuondoka na ushindi mnono, watanzania wameipokea vizuri chadema, wameanza kuiamini na watendelea kuiunga mkono.

Lakini tusisahau kuwatumia vizuri wabunge tulionao ili kuzidi kujiimarisha na hususan kwa akina mama. Wanawake wengi wanaonekana kuangukia kwa ccm, hivyo basi tuwatumie vizuri wabunge wetu wanawake na hususan hawa wa viti maalum kuwafikia wanawake wengi ili wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono chadema na wagombea wake.
 
Kwa kweli hilo ni jambo la msingi sana,nawasihi wawe na utulivu watumie hekima zaidi ya mabavu,ruzuku itakayoongezeka ikiue chama bali ikiimarishe uchaguzi ujao kipate wabunge 100 na rais atoke upinzani
 
Ndugu wadau wa JF,

Wakati huu tunapojipongeza kwa kufanikiwa kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni, hususani chama mbadala CHADEMA, na baada ya kufahamu wabunge wateule wa viti maalum, basi naomba tuangalie mbele zaidi kwa kuutazama uchaguzi mkuu wa 2015 kwakuwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, maandalizi ya uchaguzi wa 2015 ndio yamekwishaanza.

Baada ya kupitia majina ya wateule wa viti maalum, na kwa kuzingatia ujasiri na mfano wa kuigwa ulioonyeshwa na binti imara na jasiri mh.Halima Mdee, ninaomba kutoa hoja kwamba chadema iendelee kuwa mfano kwa vyama vingine na kwahiyo kujitofautisha navyo. Ushindi wa Halima Mdee kwa kiasi kikubwa umetoa hamasa ya kipekee si kwa wanawake au akina mama watu wazima tu, bali pia kwa wasichana wadogo kwamba nao wanaweza, kwani amekuwa ni mwanamke wa kwanza kushinda kiti cha ubunge kutoka chama cha upinzani kutokea jimboni.

Ni hamasa ya kipekee kwa wanawake kuweza kushiriki siasa si kwa kutegemea nafasi za kupewa ama kuteuliwa bali pia kwa kugombea majimboni na wanaweza kushinda na hata wasiposhinda lakini uwezo wao utakuwa umeonekana na kutambulika kama ilivyokuwa kwa Mh. Regia Mtema, alipambana kiasi cha kutosha hadi chama kimemuamini na kumpa nafasi kupitia viti maalum.

Kwa muktadha huo, ningependa kutoa ushauri kwa chadema au wabunge hawa wa viti maalum ambao wamekuwa wawakilishi wa wananchi kwa viti maalum kupitia chadema kwa muda wa miaka 5 na zaidi kuwa na mpango mkakati wa kujitokeza majimboni mwaka 2015 ili kuhakikisha kwamba chama kinakuwa na wagombea katika majibo yote nchini.

Kwa uzoefu walioupata na watakaoendelea kuupata, naamini kabisa wataweza kuwa ni chachu ya kipekee katika siasa za Tanzania na hatimaye chama chetu kitapata ushindi mkubwa zaidi kwa kuwa tunayo nafasi kubwa zaidi ya kuchukua uongozi wa nchi hii 2015.

Kwa heshima kabisa nawaomba waheshimiwa hawa wajiandae kwenda kugombea majimboni uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
1. Mh. Lucy Owenya
2. Mh. Suzan Lyimo
3. Mh. Grace Kiwelu
4. Mh.Muhonga Ruhwanya

Karibuni wadau kwa mawazo yenu,

Naomba kutoa hoja.

Ni kweli kabisa; viti maalum viwe ni transition ya kupata jimbo na waanze mkakati huo kwa sasa. Halima Mdee alikuwa akitoa mchango wake kwa wananchi wa Kawe, mfano, kusaidia kutatua matatizo kama ya ardhi kisheria. Pia wajitahidi wawe public figures kwa maana ya kuwa wageni rasmi kwenye shughuli za wananchi; watoe michango bungeni bila woga kwa maslahi ya jamii; waangalie matatizo ya sehemu wanazoishi na aidha kushirikiana na wabunge wa Chadema wa majimbo katika kupigania haki na kuiwajibisha serikali. Ili 2015 hivyo viti wawaachie wengine kwani watakuwa wamekomaa vya kutosha.
 
Back
Top Bottom