Nimekumbuka wimbo wa Ferouz, soma wenyewe muone barua hii;
Angalia walichoindicate kuhusu ISBN
Kisha nenda kwenye references
unakutana na hii, mwanawane;
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (2005). Mtaala wa Elimu ya Awali (Andiko lisilochapishwa)
TAASISI YA ELIMU TANZANIA
MTAALA WA ELIMU YA AWALI
TANZANIA BARA
TAASISI YA ELIMU TANZANIA
MTAALA WA ELIMU YA AWALI
TANZANIA BARA
© Taasisi ya Elimu Tanzania, 2010 Chapa ya kwanza 2012ISBN……………..……
Mtaala huu umebuniwa na kutayarishwa na:Taasisi ya Elimu TanzaniaKitalu na. 686, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi,S.L.P 35094Dar es Salaam.Simu: 255 22 2773005Nukushi: 255 22 2774420
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupigisha chapa au kutoa andiko hili kwa jinsi yoyote ile bila idhini ya Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania.
YALIYOMO
Dibaji……………………………………………………………… iv1.0 Utangulizi…………………………………………………………. 1 1.1 Muktadha wa sasa wa kijamii na kiuchumi……………… 12.0 Matamko Ya Sera.....……………..................................................... 12.1 Sera za Kimatai….......…………………….................................. 22.2 Sera za Kitaifa……………………………................................... 23.0 Dira, Dhamira, Malengo na Ujuzi wa Elimu ya Awali.................. 2
3.1 Dira …………………………………………. .............................. 23.2 Dhamira…………………………………….................................. 23.3 Malengo…………………………………….................................. 23.4 Ujuzi wa jumla wa Elimu ya Awali…………................................ 54.0 Muundo Wa Elimu……………......................................................... 54.1 Muda wa kusoma……………………………................................ 54.2 Idadi ya vipindi……………..………………................................. 65.0 Maudhui ya Mtaala wa Elimu ya Awali…………............................. 6
5.1 Lugha ………………………………………................................... 65.2 Sayansi…… ………………………………................................ ..... 65.3 Hisabati……………… .......………………................................... 65.4 Elimu ya Jamii………………… ………........................................ 75.5 Maadili na Imani………………… …………..................................... 76.0 Viwango vya Rasilimali Kwa Ajili ya Utekelezaji wa Mtaala………... 86.1. Rasilimali watu………………………………………..................... 86.2.Rasilimali vitu..................................................................................... 87.0 Njia Za Kufundishia Na Kujifunzia..................................................... 108.0 Ufuatiliaji Wa Maendeleo Ya Mtoto.................................................... 11
9.0 Ukaguzi Na Usimamizi Wa Utekelezaji Wa Mtaala.......................... 12
REJEA........................................................................................................ 13
DIBAJI
Mtaala wa Elimu ya Awali umeandaliwa ili kukidhi mahitaji ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, falsafa ya elimu ya kujitegemea ya mwaka 1967, Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu 1999- 2009 na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025. Aidha mtaala umezingatia mahitaji ya jamii ya kisayansi na kiteknolojia, na mtazamo mpya kuhusu ufundishaji na ujifunzaji. Vile vile mtaala huu umezingatia mapendekezo ya tafiti anuai za kielimu na maoni ya wadau wa elimu. Mtaala huu umejengeka kwenye misingi muhimu ya kielimu. Sehemu ya misingi hiyo inaonesha kwamba mtaala unamlenga mtoto, unakuza matumizi ya maarifa, unazingatia njia zinazomshirikisha mtoto, unabeba masuala mtambuko na umezingatia ujenzi wa stadi za maisha. Mtaala pia umezingatia ujuzi unaotakiwa katika dunia ya leo.Katika mtaala huu, jumla ya vitendo vya masomo sita (6) pamoja na dini vitafundishwa. Vitendo hivyo ni: Vitendo vya Kiswahili, English Learning Activities, Vitendo vya Hisabati, Vitendo vya Sayansi, Vitendo vya Haiba na Michezo na Vitendo vya Sanaa. Vitendo hivi ndivyo vilivyounda muhtasari wa Elimu ya Awali. Aidha sifa za walimu Mkuu wa elimu ya awali, Mwalimu wa elimu ya awali na Wasaidizi wao zimebainishwa.Njia shirikishi, vifaa na zana za kufundishia na kujifunzia zimebainishwa na kuwekewa mkazo. Mtaala pia umeelezea umuhimu wa kufuatilia maendeleo ya mtoto na kubainisha zana za upimaji zitakazotumika katika ufuatiliaji huo. Aidha, mtaala umeelezea jinsi ukaguzi na usimamizi wa mtaala wa elimu ya awali utakavyofanyika.Dkt. Paul S. D. MushiMkurugenzi MkuuTaasisi ya Elimu Tanzania
1.0 UTANGULIZI1.
1 Muktadha wa Elimu ya Awali TanzaniaElimu ya awali ni ngazi ya kwanza katika mfumo wa elimu ya Tanzania ambayo hutolewa kwa watoto wadogo kabla ya kujiunga na elimu ya msingi. Elimu hii hutolewa kwa watoto kuanzia miaka 5 mpaka 6 kwa lengo la kuwapa maarifa, stadi na mielekeo ambayo itawasaidia kupambana na maisha yao ya kila siku na pia kuwaandaa kwa elimu ya msingi. Ili kutoa elimu hii kikamilifu, mtaala wa elimu ya awali umeandaliwa kwa kuzingatia mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika nchi ya Tanzania na dunia kwa ujumla. Mahitaji mbalimbali yamezingatiwa katika maandalizi ya mtaala huu kama ifuatavyo:
1.1.1 Mahitaji ya KijamiiMtaala wa elimu ya awali umezingatia masuala mbalimbali ya kijamii ambayo huchochea ukuaji wa mtoto katika nyanja zote. Mambo hayo ni pamoja na lishe bora, afya bora, uangalizi, mahusiano ndani ya familia, vifaa na viwanja vya michezo na mila na desturi. Vile vile mtaala huu umezingatia haki za mtoto, stadi za maisha, utamaduni na ujenzi wa haiba inayokubalika kwa jamii ya Kitanzania.
1.1.2 Mahitaji ya KiuchumiMtaala wa elimu ya awali umekusudia kumwezesha mtoto kujitegemea zaidi yeye mwenyewe kwa kutumia maudhui yatakayomwezesha kukua kiakili, kitabia na kifikra ili anapojiunga na elimu ya msingi angewe uwezo wa kuwa mbunifu na mgunduzi na kutumia mazingira yake ili kupata mahitaji ya msingi na kutatua matatizo kwa kiwango cha makuzi yake. Kwa kuwa Tanzania ni nchi inayofuata falsafa ya elimu ya kujitegemea, mtaala huu umekusudiwa kumwandaa mtoto ili aweze kujitegemea kwa kumpatia maarifa na stadi sahihi ambazo zitamwezesha kujenga misingi ya kujitegemea. .
2.0 MATAMKO YA SERA
Katika uandaaji wa mtaala huu, sera mbalimbali za kimataifa na kitaifa zimezingatiwa ili kumwandaa mtoto kikamilifu kupata elimu bora. Sera hizo ni kama ifuatavyo :
2.1 Sera za Kimataifa
Ili kukidhi haja ya utoaji wa elimu bora kwa watoto, mtaala pia umeridhia Mikataba ya Kimataifa Kuhusu Haki za Mtoto ya mwaka 1989, Sera ya Elimu kwa Wote ya mwaka 1990 na Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya mwaka 2002 yamezingatiwa.
2.2 Sera za KitaifaMtaala pia umeazimia kutekeleza azma ya Dira ya Maendeleo ya Taifa la Tanzania kufikia Mwaka 2025 kuhusu mtoto, Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) 2005-2010, Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu. Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu wa 1999- 2009 umeandaliwa chini ya sera ya Elimu na mafunzo (1995) kwa madhumuni ya kukuza ushiriki wa wadau katika elimu, kuimarisha uwazi miongoni mwa watendaji, matumizi ya rasilimali, uwekaji wa mipango, usimamizi, tathmini na utekelezaji wake na kuanzisha mahitaji ya utekelezaji wa malengo ya sekta ndogo za elimu yaani msingi, sekondari, ualimu, elimu ya ufundi na elimu ya juu.Dira ya Maendeleo ya Tanzania kufikia mwaka 2025 imelenga kukuza maendeleo ya jamii, hususani kutoa elimu bora kwa lengo la kuendeleza walengwa katika ubunifu, ugunduzi/uvumbuzi, maarifa na stadi mbalimbali, kutoa wataalamu wenye uwezo wa kutatua matatizo ya jamii nchini, utumiaji wa sayansi na teknolojia na vitendo katika ngazi zote za elimu na kuwa na jamii iliyoelimika vyema ifikapo mwaka 2025.Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) 2000-2006 unalenga katikakuwa na mtaala bora wenye muundo unaotekelezeka na kukidhi mahitaji ya wadau wa elimu ikiwa ni pamoja na kuufanya umlenge mtoto zaidi, kuufanya mtaala ulenge kwenye ujuzi badala ya maudhui, kuingiza masuala mtambuko na stadi za maisha katika mtaala, kuboresha ufundishaji kwa walimu na ujifunzaji wa wanafunzi na kuboresha upimaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya mwanafunzi ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu iliyo bora wakati wote.Mkakati wa Taifa wa Kuinua Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA)umelenga
kuwa na mtaala wa elimu ya msingi utakaowapa walengwa maarifa, stadi na mielekeo
chanya ya kushiriki vyema katika kujiletea maendeleo yao wenyewe. Hivyo Taifa
litaweza kuongeza uzalishaji mali na kupunguza umaskini.
Kwa mujibu wa sera ya elimu, lugha rasmi ya kufundishia Elimu ya Msingi itakuwa ni Kiswahili. Lugha ya Kiingereza itafundishwa kama somo la lazima. Shule zinazotumia lugha ya kiingereza kufundishia, somo la Kiswahili litafundishwa kama somo la lazima.
3.0 DIRA, DHAMIRA, MALENGO NA UJUZI WA ELIMU YA AWALI
3.1. Dira
Ni kuwa na watoto wenye misingi bora katika stadi za awali za kusikiliza, kuzungumza, kusoma, kuandika, kuhesabu na mielekeo iliyo bora.3.2 DhamiraNi kutoa elimu ya awali iliyo bora kwa usawa kwa watoto wote wenye umri wa miaka mitano (5) na sita (6) na kuhakikisha kuwepo kwa mazingira rafiki ya mtoto yanayokidhi mahitaji ya ufundishaji na ujifunzaji wenye manufaa katika nyanja zote kuu tatu za elimu.
3.3 Malengo
3.3.1 Malengo ya Elimu Nchini Tanzania
Malengo ya jumla ya Elimu Tanzania kama yalivyotolewa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ni haya yafuatayo:
(a) Kujenga na kudumisha stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma, kuandika, kuhesabu, ubunifu na kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za kigeni.(b) Kukuza na kuendeleza mila, desturi na utamaduni wa jamii ya Watanzania.(c) Kurithisha, kuendeleza na kutumia maarifa, stadi na mielekeo itokanayo na maandishi anuai, sayansi ya jamii, sayansi ya asili, teknolojia na mafunzo ya kazi kuendeleza jamii anamoishi.(d) Kukuza na kuendeleza moyo wa kujiamini, kudadisi, kutathmini, kufikiri kiyakinifu na kufanya uamuzi wa busara, kuheshimu utu, haki za binadamu na kuchochea utayari wa kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo binafsi nay a Taifa.(e) Kujenga uwezo na ari ya kujielimisha na utashi wa kuendelea kutafuta maarifa na stadi za kiutendaji.(f) Kujenga na kuendeleza heshima kwa Katiba ya nchi, kuthamini utawala wa sheria na haki za binadamu.(g) Kujenga uwezo na misingi ya kutambua, kuheshimu na kupenda kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi.(h) Kukuza ari ya kuyatambua na kuyahifadhi mazingira. (i) Kujenga na kudumisha misingi ya kuthamini umoja, amani na ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.(j) Kujenga misingi na ari ya kutambua na kuthamini mchango wa sayansi na teknolojia katika maendeleo ya taifa.
3.3.2 Malengo ya Elimu ya Awali
Malengo ya elimu ya awali nchini yameainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ambapo haki za mtoto zimezingatiwa. Malengo hayo ni:i) Kuhimiza na kukuza maendeleo yanayojumlisha ukuaji wa haiba na uwezo wa mtoto kimwili, kiakili, kimaadili na kiroho.i) Kuwatambua watoto wenye matatizo na wale wenye uwezo na vipaji vya pekee ili kuweza kubuni mbinu na mipango maalum ya kuwasaidia kukua kwao kielimu kiuchumi na kijamii.ii) Kumjengea mtoto tabia na kumwezesha kupenda kujifunza desturi za kijamii zinazokubalika.iii) Kumsaidia mtoto kujifunza, kuthamini, kuheshimu familia, pia utamaduni, mila na desturi za kijamii, zinazokubalika kitaifa pamoja na kujivunia maadili na utambulisho wa kitaifa.iv) Kumpa mtoto fursa ya kujifunza na kukuza stadi za mawasiliano, numerali na utendaji.v) Kumwandaa mtoto kwa elimu ya msingi.
3.4 Ujuzi wa Jumla wa Elimu ya Awali
Mtaala huu unatarajiwa kumwezesha mwanafunzi kupata ujuzi mbalimbali kufuatana na kiwango cha makuzi yao kama ifuatavyo:i) Kuthamini imani ya kiroho, kuheshimu familia, utamaduni, mila, desturi na maadili yanayokubalika katika jamii na utambulisho wa kitaifa.ii) Kuwasiliana, kutambua numerali na kutenda kwa usahihi.iii) Kuchunguza, kutambua na kutafsiri vitu mbalimbali vilivyo katika mazingira yanayomzunguka.iv) Kuhesabu, kutambua maumbo na vipimo kwa kulinganisha na kutofautisha. v) Kuimba na kucheza michezo. vi) Kufanya majaribio rahisi ya sayansi. vii) Kubuni, kuunda na kutumia fikra yakinifu katika kutatua matatizo.viii) Kujitegemea na kujiendeleza.
4.0 MUUNDO WA ELIMU
Mfumo wa elimu nchini Tanzania kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ni 2-7-4-2-3+, yaani miaka 2 ya elimu ya awali, miaka 7 ya elimu ya msingi, miaka 4 elimu ya kawaida sekondari kidato cha nne, miaka 2 elimu ya sekondari kidato cha sita na miaka 3 au zaidi ya chuo kikuu.
4.1 Muda wa Kusoma
Elimu ya awali itachukua muda wa miaka miwili kukamilika. Mwaka wa kwanza ni kwa watoto wa umri wa miaka 5 na mwaka wa pili ni kwa wale wa miaka 6. Kila mwaka wa masomo utakuwa na siku 194 na mihula miwili yenye majuma 21 kwa kila mhula
.4.2.1 Idadi ya Vipindi
Kila siku kutakuwa na vipindi 5 vya dakika 20 kila kimoja. Kutakuwa na jumla ya vipindi 25 kwa wiki
.5.0 MAUDHUI YA MTAALA WA ELIMU YA AWALI
Mtaala wa elimu ya awali unalenga kumuandaa mtoto kwa ajili ya elimu ya msingi. Maudhui mbalimbali yamezingatiwa ambayo yamegawanywa katika vitendo mbalimbali vya masomo kama ilivyobainishwa katika maeneo ya kujifunza hapa chini. Maeneo ya kujifunza yametokana na malengo ya jumla ya elimu kama ifuatavyo:
5.1.1 Lugha
Eneo la lugha linahusisha maendeleo ya stadi za mawasiliano katika maisha ya kila siku. Stadi hizo ni kusikiliza, kuzungumza, kuandika na kusoma. Mtoto atakapojenga misingi mizuri katika stadi hizo ataweza kukuza uwezo wake katika kuwasiliana kwa lugha ya kiswahili na kiingereza. Aidha ataweza kuthamini Kiswahili kama lugha ya taifa na kumjengea misingi imara katika ujifunzaji wa lugha mbalimbali na maeneo mengine ya vitendo vya masomo. Vitendo vya masomo katika eneo hili vitakuwa ni:i) Vitendo vya Kiswahiliii) English Learning activities
5.1.2 Sayansi
Eneo hili linahusisha kuwapa watoto misingi katika uelewa wa ulimwengu halisi ambamo wanaishi. Watoto watapata pia misingi ya dhana, stadi na michakato katika kufanya majaribio rahisi kwa kutumia vitu vilivyopo katika mazingira yanayowazunguka. Stadi za sayansi zitawasaidia watoto kukuza mtazamo chanya wa masomo ya sayansi na kutumia misingi ya sayansi katika maisha yao ya kila siku. Vitendo vya masomo katika eneo hili vitakuwa ni Vitendo vya Sayansi
5.1.3 Hisabati
Eneo hili litawawezesha watoto kupata misingi ya awali ya dhana na stadi za kihisabati. Stadi hizi zitamwezesha mtoto katika kutafsiri numerali, kulinganisha na kutofautisha vipimo na maumbo mbalimbali, kukuza mtazamo chanya wa hisabati na kutumia misingi ya hisabati katika maisha yao ya kila siku. Vitendo vya masomo katika eneo hili vitakuwa ni Vitendo vya hisabati.5.1.4 Elimu ya Jamii
Eneo hili linahusisha misingi ya uelewa wa maarifa, tafsiri ya tabia pamoja na mazoea ya kibinadamu na jinsi yanavyoathiri mazingira yao. Eneo hili pia linahusisha kujifunza stadi mbalimbali za mikono, kuthamini na kuwasiliana kwa kutumia sanaa. Elimu ya sanaa itamjengea mtoto ukakamavu na uvumilivu, kujenga misingi ya ushirikiano na wenzao katika masuala mbalimbali, kupendana na kuheshimiana katika jamii wanamoishi, kuheshimu na kuthamini utamaduni wetu na watu wenye mahitaji maalumu wa jinsia zote. Vitendo vya masomo katika eneo hili vitakuwa Vitendo vya Sanaa.
5.5 Maadili na Imani
Eneo hili ni kwa ajili ya kumuandaa mtoto katika misingi ya maadili na imani ikihusisha kanuni mbalimbali kama uvumilivu, wajibu, uaminifu, haki pamoja na maana na thamani ya maisha. Maadili na imani pia vitamwezesha mtoto kujenga na kujifunza misingi ya tabia njema, kujua na kufuata misingi ya dini zao, kuishi kwa kuwa raia wema na kuheshimu imani za watu wengine. Vitendo vya masomo katika eneo hili vitakuwa:i) Vitendo vya haiba na michezo.ii) DiniJedwali na.1: Eneo la Kujifunza, Vitendo vya Somo na Idadi ya vipindi kwa kila vitendo vya somo.[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
Eneo la Kujifunza
[/TD]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Somo
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
Idadi ya Vipindi
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 198, bgcolor: transparent"]
Lugha
[/TD]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Kiswahili
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
English Learning Activities
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 198, bgcolor: transparent"]
Hisabati
[/TD]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Hisabati
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 198, bgcolor: transparent"]
Sayansi
[/TD]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Sayansi
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 198, bgcolor: transparent"]
Elimu ya Jamii
[/TD]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Sanaa
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 198, bgcolor: transparent"]
Maadili na Imani
[/TD]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Haiba na Michezo
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 217, bgcolor: transparent"]
Vitendo vya Dini
[/TD]
[TD="width: 142, bgcolor: transparent"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
6.0 VIWANGO VYA RASILIMALIKWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MTAALA
6.1 Rasilimali Watu
6.1.1 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali
Mwalimu mkuu wa elimu ya awali anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;a) Awe amehitimu Kidato cha nne kwa kiwango cha daraja la III au zaidi b) Awe amehitimu mafunzo ya ualimu wa elimu ya awali katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.c) Awe na upendo kwa watoto wa aina zote, wakiwemo wenye mahitaji maalum.d) Awe na uzoefu katika kufundisha darasa la elimu ya awali kwa muda usiopungua miaka 5.e) Awe na ari ya kujiendeleza katika eneo hili
.6.1.2 Mwalimu wa Elimu ya Awali
Mwalimu wa elimu ya awali anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:a) Awe amehitimu Kidato cha nne kwa kiwango cha daraja la III au zaidi.b) Awe amehitimu mafunzo ya ualimu wa elimu ya awali ngazi ya cheti, stashahada au shahada katika chuo kinachotambuliwa na serikali.c) Awe na upendo kwa watoto wa aina zote, wakiwemo wenye mahitaji maalum.d) Awe na ari ya kujiendeleza katika eneo hili.
6.1.3 Msaidizi wa Mwalimu wa Elimu ya Awali
Kutakuwa na msaidizi mmoja wa mwalimu wa elimu ya awali. Msaidizi huyo atakuwa si mwalimu. Msaidizi wa mwalimu waelimu ya awali anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;a) Awe amehitimu kidato cha nne kwa kiwango cha daraja la IV b) Awe amehitimu mafunzo ya malezi ya watoto wa elimu ya awali katika chuo/taasisi inayotambuliwa na serikali.c) Awe na upendo kwa watoto wa aina zote, wakiwemo wenye mahitaji maalum.d) Awe na ari ya kujiendeleza katika eneo hili.
6.1.4 Uwiano wa Mwalimu na Watoto
Katika darasa la Elimu ya Awali, uwiano kati ya mwalimu na watoto utakuwa ni 1:25.
6.1.5 Idadi ya Vipindi kwa Mwalimu.
Mwalimu mmoja atafundisha vipindi vyote kwa darasa husika ambavyo ni 25 kwa wiki.
6.1.5 Rasilimali Vitu6.2.1 Vifaa na Zana za Kufundishia na Kujifunzia
Mtaala wa elimu ya awali utatumia vifaa mbalimbali vikiwemo muhtasari, vitabu vya kiada na ziada, miongozo ya kufundishia na zana mbalimbali za kufundishia na kujifunzia. Vitabu vya kiada na ziada vitakavyotumika ni vile vitakavyokuwa na ithibati ya EMAC. Uchaguzi wa vifaa na zana utazingatia makundi ya watoto wakiwemo wenye mahitaji maalumu kama wasioona vizuri, wenye ulemavu wa akili, viziwi, wanaojifunza polepole na wenye vipaji maalumu.
6.2.2 Kisanduku cha Huduma ya Kwanza
Shule/Darasa la elimu ya awali litakuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza. Huduma ya kwanza itatolewa na mwalimu/msaidizi aliyepata mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa watoto wadogo.
6.2.3 Madarasa, Vyoo na Samania) Madarasa
Katika shule za msingi kutakuwa na madarasa ya elimu ya awali kama sehemu ya shule kimuundo. Hii itajumuisha shule za msingi zilizoanzishwa na zitakazoanzishwa na watu binafsi, taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, mashirika ya dini, mashirika ya umma na mamlaka mbalimbali. Shule zitakazojengwa kama shule za elimu ya awali kwa watoto wenye umri wa miaka mitano (5) na sita (6) zitakuwa na utawala toufauti na ule wa shule za msingi zenye madarasa ya elimu ya awali kama sehemu ya shule. Miundo mbinu ya shule kwa madarasa ya elimu ya awali itakuwa ni ile inayomjali mtoto kwa kuzingatia umri na utimamu wa maumbile. Ukubwa wa madarasa utakuwa ni m 6.0x m 8.0 (wastani wa mita za ukubwa 1.9 kwa mwanafunzi mmoja). Mpango wa darasa uweke nafasi kwa ajili ya kona za vitendo vya masomo na uwajali watoto wenye ulemavu.b) SamaniSamani zitakazotumika ziwe salama na ziaendane na kimo cha watoto. Kwa mfano ukubwa wa madawati, urefu wa makabati na shobaka za kuhifadhia zana na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Mpangilio wa samani utakuwa ni ule utakaowezesha utumikaji wa mbinu shirikishi na kutoa nafasi kwa ajili ya kona za vitendo vya masomo. c) Vyoo Kutakuwa na vyoo safi na salama vinavyomjali mtoto, pia kutakuwa na vyoo maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa viungo.
6.2.4 Viwanja Vya Michezo
Michezo ni muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mtoto. Michezo humsaidia mtoto kujifunza stadi mbalimbali, kuvumbua, na kudadisi mazingira anayoishi kwa kushirikiana na wenzake. Ni muhimu kuwepo na viwanja vya michezo na vifaa kwa ajili ya michezo mbalimbali. Vifaa hivi vinaweza kutengenezwa na mzazi, mlezi, mwalimu au watoto wenyewe kutokana na malighafi zinazopatikana katika mazingira yao.
6.2.5 Vifaa vya Chakula
Mwalimu/msaadizi atazingatia maendeleo ya afya ya mtoto tangu anapojiunga na elimu ya awali. Huduma ya chakula itatolewa kwa kila shule /darasa la elimu ya awali. Mtoto anahitaji chakula chenye virutubisho vyote muhimu ili aweze kukua na kupata uwezo wa kujifunza kikamilifu. Hivyo basi, vyombo vya kupikia na kulia watoto ni muhimu vikawa safi na salama ili kuwakinga watoto na magonjwa yanayotokana na uchafu. Vile vile ili mtoto awe na afya bora. Mtoto pia anahitaji kukaa mahali safi na salama, kupata kinga dhidi ya magonjwa , kupata muda wa kupumzika na kucheza.
7.0 NJIA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Mtaala huu umejikita katika njia shirikishi zenye kumjali mtoto. Njia zitakazotumika ni zile zitakazomshirikisha mtoto kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa mtendaji mkuu katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Baadhi ya njia hizo ni kama vile njia ya vitendo, michezo, onesho mbinu, hadithi, nyimbo, vitendawili, uchunguzi, mashairi ya watoto, ziara na igizo. Mwalimu atakuwa mwezeshaji wa tendo la kujifunza. Njia hizo zitamjenga mtoto kimaarifa, kistadi na kimwelekeo au kihaiba. Watoto wote wamotishwe kupenda kujifunza vitendo vya masomo yote bila kujali jinsia. Mwalimu azingatie ujifunzaji wa watoto wenye matatizo ya kujifunza ili aende nao sambamba sawa na wengine wasio na matatizo hayo. Vichocheo hasi katika kujifunza kama vile kukaripia, kufinya au kuchapa viboko watoto visitumike kabisa kwa watoto.Mamlaka za shule ziwezeshe ufundishaji/ujifunzaji bora kwa kuwapatia walimu mafunzo sahihi ya mara kwa mara, vifaa na zana bora za kutosha za kufundishia na kujifunzia. Mamlaka hizo pia zitahusika na ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu.
8.0 UFUATILIAJI WA MAENDELEO YA MTOTO
Katika elimu ya awali mtoto hatapimwa kwa mitihani ya kuandika bali kwa kuangalia na kurekodi maendeleo yake ya kila siku.Upimaji wa aina hii ni muhimu kwa sababu utamwezesha mwalimu kuona jinsi mtoto anavyobadilika kimwenendo tangu alivyoanza kujifunza katika darasa la awali.Upimaji wa maendeleo ya mtoto wa elimu ya awali uzingatie vigezo mbalimbali vya kuonesha viwango tofauti vya mabadiliko na maendeleo ya mtoto katika kujifunza. Vigezo hivyo ni:-a) Maendeleo ya kujifunza maarifa, staidi na mwelekeo, yaani kujifunza vitendo vya masomo.b) Mabadiliko yake katika tabia.c) Mabadiliko ya afya ya mtoto.Upimaji wa mtoto wa elimu ya awali utakuwa ni wa aina kuu nne ambazo ni upimaji awali, upimaji endelevu, upimaji tatuzi na upimaji tamati. Ni muhimu sana mtoto anapoanza elimu ya awali kupimwa kabla ya kuanza mafunzo ili kujua afya yake na kiwango cha uelewa alichonacho. Uwezo wa mtoto katika kupata maarifa, stadi na mielekeo mbalimbali katika vitendo vya masomo utapimwa kila mara sambamba na ufundishaji na ujifunzaji wa mtoto.Baada ya mafunzo ya miaka miwili ya elimu ya awali, mtoto ataangaliwa maendeleo yake kiafya, kitabia/kimwenendo na kitaaluma ili kujua ni kwa kiasi gani ameweza kumudu mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Zana za upimaji zilizopendekezwa ni pamoja na orodha hakiki, uchunguzi makini, mkoba wa kazi, shajara na fomu inayoonesha taarifa za maendeleo ya motto.
9.0 UKAGUZI NA USIMAMIZI WA UTEKELEZAJI WA MTAALA
Ukaguzi na usimamizi wa utekelezaji wa mtaala utafanywa na idara ya ukaguzi wa shule kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Wizara. Kazi kubwa ya wakaguzi wa shule itakuwa ni kuhakikisha viwango vya ubora vya elimu yaAwali katika utekelezaji wa mtaala vinazingatiwa kikamilifu. Aidha Taasisi ya Elimu Tanzania itahusika katika kufuatilia utekelezaji wa mtaala.
BIBLIOGRAFIA
Ministry of Education and Culture (MOEC). (1995) Education and Training Policy. MOEC – Dar es Salaam.
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (2005). Mtaala wa Elimu ya Awali (Andiko lisilochapishwa)
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). (2004). Ripoti ya Utafiti wa Kuboresha Mtaala wa Elimu ya Msingi. TET. Dar Es salaam (Kisawidi: Rekebisho la Kwanza); Agosti 2004.
United Republic of Tanzania (URT). (2003). Education Sector Development Plan: Primary Education Development Plan: Designs for the Improvement of Quality of Primary Education. MOEC: Dar es Salaam, April 2003. (Andiko Lisilochapishwa)
URT. (2001). Education Sector Development Plan: Primary Education Development Programme (2002 -–2006),
Basic Education Development Committee (BEDC), July 2001 (Andiko Lisilochapishwa)
MOEC. (2001). A Baseline Survey on Knowledge, Attitudes and Practices (KAP) in Tanzania Mainland. UNFPA: Dar es Salaam.
Barnes, D (1982). Practical Curriculum Study. Routledge and Kegan Paul: London.Kirk. S. A et. al. (2003). Educating Exceptional Children, 10[SUP]th[/SUP] Edition. Houghton Mifflin Co. Boston.
Njabili. F.A. (1993). Practical Guide for Classroom Measurement and Testing. The Basic Essentials: Mture Publishers: Dar es Salaam.
Tanzania Institute of Education. (TIE). (2004). National Curriculum Development Framework (NCDF): Core Document. Dar Es salaam. (Unpublished Document)
TIE. (2004). NCDF: A Guide to Innovative Teaching and Learning. Dar Es salaam. (Unpulished Document)TIE. (2004). NCDF. A Guide to Curriculum Localization. Dar Es salaam. (Unpublished Document).
TIE. (2004). NCDF. A Guide to Assessment and Examination. Dar Es salaam, (Unpublished Document)
TIE. (2004). NCDF. A Guide to Syallabus Development. Dar Es salaam. (Unpublished Document)
TIE. (2004). NCDF. A Curriculum Guide to Special Needs Education. Dar Es salaam. (Unpublished Document)
TIE. (2004). NCDF. A Curriculum Guide to Pre-Primary Education. Dar Es salaam. (Unpublished Document)
Wheeler, D.K (1967). Curriculum Process. Holder and Stouhton Ltd. London
Ysseldyke, S. (2004) Assessment in Special and Inclusive Education. 9[SUP]th[/SUP] Edition Houghton Mifflin Co. Boston.