Nimetengeneza profile ya maombi ya NACTE, pia gharama zote nimelipa za maombi. Sasa nahitaji kuomba kozi za ualimu diploma lakini sioni option ya elimu kwenye akaunti yangu.
Napata option moja tu ya health and allied sciences, msaada naombaje kozi za ualimu NACTE?
Kiujumla kupitia nacte application zilianza kwa kozi za afya tu peke yake na kwa kozi zingine application zinafanyika kupitia panel za vyuo husika kwa kila chuo.
Kwa upande wa ngazi ya ualimu application zilikuwa bado hazijaanza rasmi, hivyo unaweza kuvuta subira mpaka kufikia jumatatu ili kama watakuwa wameruhusu rasmi kuomba kwa kozi za ualimu then unaweza ingia kwenye system ya nacte kuangalia kama zitakuwa zimeongezwa nazo au lah.
Nakushauri uvute subira mpaka jumatatu ili kuona kama zitakuwa zimeongezwa, ila kwasasa huna cha kufanya.
Kama zitakuwa hazijaongezwa basi itabidi kuingia gharama ku-apply tena chuo husika moja kwa moja kupitia application panel zao.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.