Naomba kupata Experience kidogo kwa wale waliowahi kufanya matangazo either ya redio ama mtandaoni?

Shomary47

JF-Expert Member
Feb 12, 2021
224
348
Habari wafanyabishara,

Naomba kupata Experience kidogo kwa wale waliowahi kufanya matangazo either ya redio ama mtandaoni.

Kipi Bora na kinaleta matokeo ya haraka, Kutangaza Biashara mtandaoni kwa kulipia ama Kutumia Local radio kutangaza biashara yako.

Chukua mfano una bajet ya Laki tano 500,000 kwa mwezi, Kipi kitaleta matokeo ya Haraka Yaani upate mauzo mengi ndani ya mwezi mmoja. Ulipie mtandao ukutangazie ama Ulipie Radio ukutangazie. ??
 
Tuanze na wewe.

Ukisikia tangazo kwenye radio uwa unalisikiliza? Au ndio muda wa kufanya mambo mengine ili tangazo lipite?

Kwenye FB je?

Kwa budget ya 500k kwenye FB unaweza tangaza ata mwezi mzima. Ila kwenye Radio haifiki week.
Kwa mtazamo wangu naona kwenye Redio kunakuza jina, Japo unapata wateja sawa.

ila mtandaoni inapata wateja wengi zaidi. Kwa experience ndogo nilio nayo
 
Swali lako lilitakiwa liambatane na uko wilaya gani na unafanya biashara gani hasa.

Advertising inatofautiana kulingana na sehemu ulipo na biashara unayofanya na target audience yako ni ipi ina age gani, jinsia gani, imani gani. Shule za dini unahisi kwanini zinabanana redio gani ile ya dini yenye matangazo nusu saa nzima.
Ukiwa unauza electronics mjini Dar es Salaam utalipia Instagram zaidi.
Ukiwa unamiliki chuo utatumia TV na redio, ukiwa unauza viwanja au real estate nzima utatumia hata magazeti ingawa siku hizi wengi hawasomi. Huwezi tumia magazeti kutangaza biashara ya electronics.

Ukiwa unatoa services kama clinic utatumia redio ya wilaya husika. Kwa bidhaa za wakulima na wafugaji kama wa ng'ombe na mbuzi utatumia redio na Facebook tu ila kwa wafugaji wa kuku utatumia Instagram.

Wateja wa Facebook njaa kali ila wanakuja faster alafu wanatapeliwa sana kwa tamaa za bei zisizowezekana, wa Instagram hawajilizi sana ila wanachelewa kuja. Kuna classmate aligraduate diploma ya mifugo akaenda Karagwe akalipia tangazo redioni kwa miezi kadhaa na hela ilikuwa ndogo. Wateja walimzidi uwezo.

Uzuri wa kijijini ukienda unanyoosha Kiswahili alafu unajiita dokta hata kama form four failure, na hiyo redio umenunua kipindi au unaitwa kama mtaalamu au mshauri wa hiyo sekta yako utakusanya kijiji. Ile mfano "tuko na mtaalamu wetu Dokta Mayunga" huyo Mayunga anaweza kuwa mhuni tu.

Hata mjini kina Dokta Ndondi na Grace Products mbona walikula hela zenu wenye vitambi na mapunye.
 
Habari wafanyabishara,

Naomba kupata Experience kidogo kwa wale waliowahi kufanya matangazo either ya redio ama mtandaoni.

Kipi Bora na kinaleta matokeo ya haraka, Kutangaza Biashara mtandaoni kwa kulipia ama Kutumia Local radio kutangaza biashara yako.

Chukua mfano una bajet ya Laki tano 500,000 kwa mwezi, Kipi kitaleta matokeo ya Haraka Yaani upate mauzo mengi ndani ya mwezi mmoja. Ulipie mtandao ukutangazie ama Ulipie Radio ukutangazie. ??
kwanza inabidi ueleze aina ya biashara ili upate ushauri mzuri
 
Achana na Redio.

Mtandaoni sio tu kwamba inakupa wateja wengi. vile vile itakuletes wafuasi ambao kesho utawahiji tena bila matangazo.

Alafu itakuonyesha lipi tangazo pendwa, wateja wako ni jinsia gani ns wanatokea wapi muda gani.

Utakuwa na taarifa sahihi ya mwenendo wa biashara yako N.K….
 
Asante kwa Maoni yako kaka,
 
Asante sanaa kaka ubarikiwe
 
Asante kwa Maoni yako kaka,
Hauko serious 😂😂😂

Binafsi nishafanya Sana Facebook na Instagram marketing.

Pia kwa uchache nishawahi kufanya kwa redio japo biashara tofauti

Nilikuuliza hivyo ili nikupe ushauri kutokana na nature ya biashara

Kila biashara Ina Aina yake ya utangazaji

Hata huko Facebook Kuna ujuzi wake wa kutangaza na kuuza unless Ni matumizi mabaya ya dollars kwa kulipia matangazo yasiyo na faida
 
Habari wafanyabishara,

Naomba kupata Experience kidogo kwa wale waliowahi kufanya matangazo either ya redio ama mtandaoni.

Kipi Bora na kinaleta matokeo ya haraka, Kutangaza Biashara mtandaoni kwa kulipia ama Kutumia Local radio kutangaza biashara yako.

Chukua mfano una bajet ya Laki tano 500,000 kwa mwezi, Kipi kitaleta matokeo ya Haraka Yaani upate mauzo mengi ndani ya mwezi mmoja. Ulipie mtandao ukutangazie ama Ulipie Radio ukutangazie. ??
To whom the message should be sent?.
Unataka kuwafikia customer wako ambayo ni potential au unataka kwenda viral tu?
 
Kwa mtazamo wangu naona kwenye Redio kunakuza jina, Japo unapata wateja sawa.

ila mtandaoni inapata wateja wengi zaidi. Kwa experience ndogo nilio nayo
Huyu wateja wake ni watu gani? Mana hili ndo linatoa picha nzima ya marketing plan. Anauza nn?
 
Kwa mtazamo wangu naona kwenye Redio kunakuza jina, Japo unapata wateja sawa.

ila mtandaoni inapata wateja wengi zaidi. Kwa experience ndogo nilio nayo
Idadi kubwa ya watu kwasasa imekimbilia mtandaoni (Twiter, Insta, Facebook) huku utakutana na makundi mbalimbali ya watu ambao ndio wanunuzi wazuri wa bidhaa mbalimbali na kuna kuwa urahisi wa wateja kukufikia kupitia links na namba kwasababu mteja atahitaji kubonyeza tu ili kukufikia, tofauti na kwenye redio ambako atalazimikia kutafuta kalamu na karatasi au kukumbuka alichokisikia. Lakini pia, idadi ya watu wanaosikiliza redio sikuhizi ni ndogo sana, tena kundi kubwa ni la wazee.

Ungesema kwenye Tv ningekuelewa, tena inapendeza tangazo lako likawekwa wakati wa vipindi vya usiku kwasababu huu muda watu wengi ambao ndio watafutaji wenyewe (wenye pesa) wanakua majumbani, ila kwa hiyo budget yako ya kwa mwezi, haiwezi kutosha.

Kwa ushauri wangu, jikite kwenye mitando kwanza na uhakikisha matangazo yako yanakuwa na ubunifu.
 
Asante sana kaka, Noted. Tangazo mtandaoni ukipatia kuliseti basi utachekelea tu matokeo yake maana wateja watakua wanamiminika tu, na bajeti inakua reasonable sana.
 
Pia kama unaweza tangaza kulingana na niche uliyoilenga, mfano kama ni wajasiriamali basi upo mtandao maalumu kwa ajili yao.

Tenaa una majarida yenye maelezo yote na maelekezo unayohitaji
 
Attachments

  • Jarida la wajasiriamali na biashara zao Sahili Marketplace Network (Toleo 1).pdf
    9.1 MB · Views: 3
Back
Top Bottom