Naomba kuongea na Rais Magufuli

Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Dec 17, 2015
795
479
Ndugu zangu wana jamii forum ni muda mrefu nimekuwa nikitamani kuongea kwa simu na Rais wangu mpendwa John Pombe Magufuli ili nimweleze Shida yangu na nitubu makosa yangu kwake maana najua Rais wangu hapendi kudanganywa lakini nimekoswa namna ya kupata namba yake. Hivyo basi naomba mwenye uwezo wa kunisaidia ili niweze kuongea naye tafadhali naomba anisaidie. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Ndugu yangu kupata namba za simu ya Mh Rais ni kazi ngumu, kupata nafasi ya kuongea naye ni Ngumu zaidi.

Ninachokushauri, fuatilia ziara za Mh Rais katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Akifika katika mkoa wako, ninaamini atasimama na kusikiliza kero za wananchi kama ambavyo amekuwa akifanya. Nyoosha mkono na mweleze dukuduku lako. Atakusikiliza na atakusaidia.

Pili, kuna yule maza wa Mirathi alidai kuwa alishaongea na Mh Rais. Basi mtafute huenda ana namba za Mh ila ni ishu sana kuzipata, tupilia mbali kuongea naye.

Tatu, eleza dukuduku lako humu. Kwa inavyoonekana, Mh Rais huwa anatembelea humu na unaweza kubahatika akakusoma. Pia, kuna wateule wake wengi humu wenye nafasi ya kuongea naye hivyo watamfikishia ujumbe wake. Wapo pia wazee wa Kaunda suti, nao watakusaidia.

Nne, andika barua kisha uielekeze kwa Mh Rais. Japo ana majukumu mengi lakini huenda Shida yako ikatatuliwa.

Tano, jenga urafiki na Bashite Daudi. Jamaa huwa anampigia Mh Rais hata kwenye mikutano ya hadhara. Kwa hiyo naamini atakupa hata wewe nafasi ya kuongea naye.

Sita, nenda Clouds Fm. Redio pendwa ya Mkulu. Mwaga povu lako hapo. Tiririka na baada ya siku mbili tatu, Rais atakuwa kakusikia.

Saba, japokuwa najua bangi imepigwa marufuku fanya mbinu uipate. Vuta pafu kadhaa, shusha vitu. Kisha, kama alivyosema Kamishina wa Kupambana na Madawa ya kulevya kuwa inaleta Hallucination, utajikuta unaongea nae na umueleze shida yako.

NAKUTAKIA KILA LA KHERI.
 
Mi ninayo ila sio ile inayotangazwa. Ni personal so ningekupa labda njoo inboz nikupe ya mtoto wake
 
Shida yangu ni ya siri. Na sidhani rais wangu ni mrasimu kiasi hicho naamini ipo siku Mungu atatoa kibali cha mimi kuongea naye.
 
Kama una hoja ya kutumbua jipu sawa lakini kama ni tofauti mi sikupi namba mkuu.
 
Shida yangu ni ya siri. Na sidhani rais wangu ni mrasimu kiasi hicho naamini ipo siku Mungu atatoa kibali cha mimi kuongea naye.
Mtafute Mwigulu Nchemba Pm, mweleze shida yako. Ongea naye vizuri, naye awe middle man baina yako na Mh Rais. Namba ya Rais siyo pipi itolewe hadharani, huwezi kuipata kirahisi.
 
Hapana. Rais wangu si katili kiasi hicho hata ashindwe kuongea na watu wake. Mi mwenyewe nimeshuhudia akiwapigia cm watu wanyonge kabisa bila kujikweza.
Sijasema katili bali ana namna zake rigid jinsi ya kufanya mambo, ina maana ata pale anapodhani lazima asaidie kwa faida ya mtu au kikundi cha watu tayari anajua ni kwa namna gani na mara nyingi sio technical.
 
Mm naona Daud Bashite ndiye mtu pekee awezaye kuku saidia kwa hilo,naomba uonane naye yeye kwanza ila humu ndani una poteza muda.
 
Back
Top Bottom