Naomba kujuzwa taratibu za kuoa Kibosho

Diaryjr

Senior Member
Jun 15, 2015
190
131
Habari zenu wakuu.

Naomba kwa wajuzi wa Kabila tajwa hapo juu wanijuze utaratibu wa kuoa Kibosho. Vitu kama mahari vinakuwaje ili angalau nipate mwanga kidogo.

Asanteni sana




Mrejesho


..................................................
Niliulizia kuhusu mahari lakini wadau wakaja na ushauri na maoni ambayo nilijitahidi kuyafanyia kazi.

Katika mambo ambayo wadau wengi waliyaongelea na nineyaona kwa huyu wangu ni kiburi.
Ana kiburi fulani hivi ambacho hata kama amekosea yeye hajuti wala kuomba msamaha. Yaani ni kama anajiona kuwa yeye si mtu wa kufanya makosa kabisa.

Hasira. Ana hasira za karibu sana. Unaweza ukafanya kosa dogo lakini yeye akapaick vibaya sana mpaka unabaki unajiuliza hii ni nini?

Kususa.
Ni mtu wa kususa sana. Ukimkosea kuna mawili, apanick au asuse na kuondoka bila kusema chochote
Uongo. Kwa hapa ninegundua kuwa kuna dalili kidogo ya uongo na kujikuza. Hili bado nalifanyia kazi.


Sasa basi nimejaribu kukaa nae na kuongea nae kwa namna fulani kuhusu hizi kasoro. Nimeamua kusogeza harakati zangu za ndoa mbele kidogo ili nijipe muda wa kumuangalia zaidi.


Nashukuru sana kwa ushauri wenu.

Nategemea kupata mengi zaidi kutoka kwenu.

Asanteni
 
Back
Top Bottom