Naomba kujuzwa mambo haya kuhusu sindano ya testosterone

kwe2tu

Senior Member
Dec 30, 2023
109
173
Hii Halifa ya upungufu wa testosterone kwa wanaume imekuwa kubwa Duniani sasa. Wanasema sababu ni:

1. Uzito mkubwa
2. Vitambi
3. Kutofanya mazoezi
4. Matumizi ya madawa ya kupunguza maumivu. Nk

Ninachotaka kujua kwa ambao wanatumia au walishawahi kutumia sindano ya testosterone.

1. Unachoma mara ngapi kwa mwezi.
2. Inakaa kwa muda gani ndani ya mwili.
3. Unaweza tumia kwa muda gani, na je unaweza tumia mpk miaka kumi?
4. Je, haipo ya kila baada ya miezi sita au mwaka?
5. Je, unaweza jichoma mwenyewe?

Nb: Hili ni tatizo tusaidiane. Km sio lako leo linaweza kuwa lako kesho tunaomba uzoefu kwa ambao wanatumia au wanauzoefu wa watu ambao wanatumia

Asante
 
Sorry, nje ya mada kidogo.. hv ukipungukiwa testosterone unakua na shida gani zaidi??
 
Hii Halifa ya upungufu wa testosterone kwa wanaume imekuwa kubwa Duniani sasa. Wanasema sababu ni:

1. Uzito mkubwa
2. Vitambi
3. Kutofanya mazoezi
4. Matumizi ya madawa ya kupunguza maumivu. Nk

Ninachotaka kujua kwa ambao wanatumia au walishawahi kutumia sindano ya testosterone.

1. Unachoma mara ngapi kwa mwezi.
2. Inakaa kwa muda gani ndani ya mwili.
3. Unaweza tumia kwa muda gani, na je unaweza tumia mpk miaka kumi?
4. Je, haipo ya kila baada ya miezi sita au mwaka?
5. Je, unaweza jichoma mwenyewe?

Nb: Hili ni tatizo tusaidiane. Km sio lako leo linaweza kuwa lako kesho tunaomba uzoefu kwa ambao wanatumia au wanauzoefu wa watu ambao wanatumia

Asante

Maatatizo ya upungufu wa homoni ya testosterone yanaweza kuanza wakati wowote kwenye maisha ya binadamu.

Mnyororo mzima unaweza kuanza wakati wa kutungwa mimba au wakati mtoto amezaliwa au kwenye utu uzima. Hii huusisha matatizo ya kijenetiki na kasoro yoyote inayoweza kujitokeza kati ya tezi la Hypothalamus, Pituitary na Korodani.

Vyanzo ni kama ulivyotaja hapo juu pamoja na: Maambukizi kwenye mifumo hapo juu, matatizo ya kijenetiki, matibabu ya kansa, pia tiba ya kansa itakayohusisha maeneo ya korodani au korodani zenyewe nk.

Madhira ni pamoja na kushindwa kukua kwa ukamilifu kwa maumbile ua kiume pamoja na viashiria vyake pia kushindwa kutenda yampasayo mwanaume kikamilifu. Hii hutegemea na kiasi cha upungufu.

Kwa mujibu wa USA FDA dozi ya kuanzia kwa wanaume wenye hypogonadism/ upungufu wa homoni ya testosterone ni sindano ya mg 50 mpaka mg 400 mg (IM) kwa wiki kila wiki 2 mpaka wiki 4.

Kwa Jumuiya ya watoa tiba za homoni duniani, wanatoa maelekezo au mwingozo wa: testosterone mg 75 mpaka 100 mg (IM) kwa wiki au 150 to 200 mg IM kila wiki 2.

Yote inategemea na kiasi cha upungufu na chanzo cha upungufu. Daktari wako atafanya maamuzi ya nini kifanyike na kwa kiasi gani.

Hii ni dawa inayochomwa kwenye misuli hivyo kufanya suala la kujichoma kuwa gumu kidogo. Ingekuwa ni subcutaneous/ chini kidogo ya ngozi ingekuwa rahisi.

Kupata ya kuchoma mara moja kwa mwezi au miezi kadhaa, hii itategemea uwepo wa slow release injection ya dawa husika sokoni. Ambayo kwa sasa ipo inayoweza kukaa wiki 8-10.

Tatizo husika kama ni la kudumu, ina maana utatakiwa kutumia tiba husika kwa maisha yako yote ili kuepuka madhira ya upungufu wa homoni husika.

Mtizamo wa kuongeza kwa tatizo kunaweza kubebwa na sura hizi:
1: Upatikanaji wa teknolojia ya kugundua tatizo
2: Ongezeko la mwamko wa wagonjwa kujua tatizo
3: Mwenendo wa maisha ambao huleta visababishi husika kwa wingi zaidi miongoni mwetu.
 
Je unaweza tumia sindano hiyo ht kwa miaka kumi au zaidi??? Naomba kusaidiwa hapo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom