Naomba kujuzwa juu ya ugonjwa huu

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,647
20,984
Habari za asubuhi waungwana wote hapa, Yupo ndugu yangu ameanza kuwa mweupe katika sehemu mbalimbali za mwili wake, weupe unaofanania kama wa zeruzeru vidoleni na miguuni.

Je, huu ni ugonjwa gani na husababishwa na kitu gani au ukosefu wa madini gani na tiba kamili ni ipi?

#Thanks you.
 
Ni kweli naungana na wenzangu ktk kukushauri kuwa uwende hospital.

Kama ukituuliza sisi hapa tarajia kupata majibu mengi na mengine ni ya kuogopwa kwa mfano moja kati ya dalili inayotaka kufanana na iyo niliwahi kusikia pia wenye tatizo la INI dalili zake huwa ni kutakata yaani kuwa mweupe lkn wapo wengine wanaosema ni upungufu wa madini mwilini.
 
Huo ugonjwa unaitwa Vitiligo.......... umempata hata yule binti anaonekana kwenye wimbo wa Freedom is coming you Msouth.

Aende kuonana na doctor wa ngozi kwa hatua zaidi
 
Ukweli kuna kijana mmoja alianza kubadilika mfano wa jamii ya albino. Wengi wanadai unasababishwa na presha ama Kisukari. Mpe pole sana jaribu kumuona daktari. Kama ni mkeo usimkimbie. Huu ugonjwa anaugua pia dada mmoja alikuwa maarufu sana nchini sasa hivi yupo benki mama nchini.
 
Mkuu, ukweli ni kwamba ngozi inapoteza melanin. Maalbino hawana melanin. So in short, hauna dawa, labda(sijui), kuzuia isiendelee!
 
funguka kwanza hapa visababishi na dalili
Vitiligo husababishwa na upungufu/ukosefu wa pigment inayoitwa Melanin ambayo huzalishwa na cell za ngozi ziitwazo melanocytes (Melanin ndio huipa ngozi yako rangi iliyonayo).

So mtu huanza kupata vitiligo (mabaka meupe kwenye ngozi), pale ambapo cell zake za ngozi melanocytes zimepungukiwa uwezo wa kuzalisha melanin za kutosha kwenye ngozi.
 
Back
Top Bottom