Naomba kujuzwa haya kuhusu leseni ya biashara

X_Khally

Member
Aug 28, 2023
42
46
Habari wa JF,

Samahani nina swali kuhusu upatikanaji wa leseni ya biashara .Iwapo nina TIN number.

Je, ni documents gani natakiwa kuwa nazo ili kukamikisha upatikanaji wa leseni na pia muongozo wa upatikanaji ukoje na inachukua mda gani na gharama zake.

NB: Ni duka la Nguo za Mitumba.
 
JINSI YA KUPATA LESENI YA BIASHARA ONLINE :-

Jina la Biashara
Taarifa ya msajili (Extract from register)
Tin
Tax clearance
Mkataba wa pango
Nida /passport

Jinsi ya kujisajili.

Bofya sehemu iliyo andikwa HUDUMA.
Chagua huduma za Leseni
Hatua ya kwanza JISAJILI.
Rejea sehemu ya huduma.
Huduma za Leseni
Jaza taarifa za maombi ya leseni
Weka documents kwenye mfumo.
Tuma ombi
Thibitisha malipo.
 
Habari wa JF,

Samahani nina swali kuhusu upatikanaji wa leseni ya biashara .Iwapo nina TIN number.

Je, ni documents gani natakiwa kuwa nazo ili kukamikisha upatikanaji wa leseni na pia muongozo wa upatikanaji ukoje na inachukua mda gani na gharama zake.

NB: Ni duka la Nguo za Mitumba.
Tax clearance uharaka utategemea mtandao na halmashaur husika ushapu wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda TRA fungua file, wakukadirie Kodi lipa full wanakupa clearance certificate unapeleka ofisi ya biashara halmashauri huko ndio wanakupa leseni
-Provisional tax
-Withholding tax (Rental)

Hiyo Provisional hata akilipa installment moja na WT anapata clearance anapeleka halmashauri husika, sababu ye ni sole proprietor analipa 75,000 anapewa business license, ingekuwa ni corporate (kampuni) angelipa 150,000 ili kupata leseni.
 
ivi hii mkataba wa pango ni lazima ata kama frem ya biashara iko nyumban kwangu yaani sijapanga.
Kama ni home kwako unaenda na barua ya mwenyekiti yenye mhuri .
Maana hapo kwenye mkataba wanavholenga ni Ile withholding tax yaan rental. Utalipa ela ya mwezi mmoja wa pango pamoja na Kodi
 
-Provisional tax
-Withholding tax (Rental)

Hiyo Provisional hata akilipa installment moja na WT anapata clearance anapeleka halmashauri husika, sababu ye ni sole proprietor analipa 75,000 anapewa business license, ingekuwa ni corporate (kampuni) angelipa 150,000 ili kupata leseni.

Je hii WT na Provisional tax all ni TRA wana clear zote au online pia naweza fanya bila kwenda ofisini?
 
Back
Top Bottom