Habari zenu wataalam, kwa kifupi Mimi kwa level ya bachelor nilisoma Economics ila napenda sana niwe na CPA na ninataka january nianze kujifua kwa ajili ya mitihani ya mwezi mei. nimeangalia gharama za Review class pale CBE kwa level ya foundation (masomo 5 ) ni Tshs 400,000. wadau nimekuja mbele yenu mnisaidie kuchanganua gharama za NBAA( examination fees ) kwa hayo masomo 5 ni Tsh ngapi? nimejaribu kuangalia website ya NBAA lakini sijapata taarifa iliyojitosheleza. Natanguliza shukrani za dhati kwa ushauri, maoni na kwa ufafanuzi wenu kwa ujumla.