Naomba kujuzwa Bei za Guitar

Naomba kujuzwa Bei za Guitar

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
Naomba kuuliza bei za Guitar au gitaa Tanzania, za umeme na zisizo tumia umeme, nimeziona huku nilipo katika minada au auction, pengine naweza kufanya hii biashara, nahitaji kufahamu bei zake Tanzania na sina utaalamu nazo, mwenye kuzifahamu anifahamishe.
 
Mmmhhhh, hebu subiri kwanza, nyieeeeeeeeee wakina Ottu,Sikinde, Ally Choki, Banza Stone na Muumini Mwinjuma njooni huku mumpe jibu huyu jamaa/sista
 
Wako wapi?
 
Achana na hilo wazo wewe, nani anataka maused ya guitar? Siku izi bongo si ka zamani
 
Galatone ni kuanzia 50+ . mie nahitaji nipo dar ni pm kama upo serious
 
Mtu anataka kutumia fursa wewe unampotosha.

Uelewe, Kwa uchumi wetu Watanzania kumudu bei ya vifaa vya muziki vipya si kitu rahisi.
Sibishi, vipo ila ni kama mapambo huko madukani kutokana na bei kuwa kubwa sana kulinganisha na uwezo wa wateja ambao ni wasanii.

FAHAMU TU BONGO LICHA YA KUPIGWA MARUFUKU BADO TUNAUZIWA CHUPI, SIDIRIA,SOKSI MPAKA MATAULO YA MTUMBA.Hulijui hili?
NINI VIFAA VYA MUZIKI Ikiwa wasanii wenyewe ni choka mbaya.
 
Ok mkuu
Nitajitahidi kuangalia hio Gatatone 50+, nataka kufahamu bei zake huko ili nisije kupata hasara, wewe utanunua kwa bei gani?
 
Mtu anataka kutumia fursa wewe unampotosha.

Uelewe, Kwa uchumi wetu Watanzania kumudu bei ya vifaa vya muziki vipya si kitu rahisi.
Sibishi, vipo ila ni kama mapambo huko madukani kutokana na bei kuwa kubwa sana kulinganisha na uwezo wa wateja ambao ni wasanii.

FAHAMU TU BONGO LICHA YA KUPIGWA MARUFUKU BADO TUNAUZIWA CHUPI, SIDIRIA,SOKSI MPAKA MATAULO YA MTUMBA.Hulijui hili?
NINI VIFAA VYA MUZIKI Ikiwa wasanii wenyewe ni choka mbaya.

Shukran kwa kumfahamisha huyu kijana, ndio maana waafrica hatuendelei kwa kuvunjana tamaa kama za huyu.
 
Mkuu mm nimesafirisha 1.26cubic meter stuffs zangu za nyumbani toka Tullemale Int A/port (australia) to Dar vitu kama home appliance, keyboard, guitar, home theatre, tv, toys, scooters, pram, strolley na nikalipa AUD 2695 (usd 2200) lakini sijaona tofauti kiviile kama ningenunua tu huku bongo ingawa vingine ofcoz havipo huku Tz.

Labda uko ulipo kuna alternative ya usafiri & tra pale cargo lounge sioni km galaton ni deal wkt veta moshi wanaunda very classic galatons..anyway sikukatishi tamaa but it may not be worthy
 
Usafirishaji kwangu sio deal kwani kila week tunasafirisha mizigo, tunachargiwa hela ndogo tu, mzigo kama wako huo hapa UK ni pounds 200 mpaka 300, wakati mwingine huwa na gari na kuitia kwenye gari, na huchargiwa bei ya gari tu.

Kama unataka kufanya biashara ya used UK usafiri wake rahisi kidogo kutokana na wasafirishaji ni wengi sana, kila siku watanzania wanapakia contena.
 
Mkuu wanakupotosha bei inategemeana na gitaa ....mfanp Dar Yamaha galatoni ni SH. laki tano kuna mengine ni 250,000/= , mpaka ya 150,000/= yapo ! ya umeme ni hivyo mengine hadi laki 600,000/- ....Niletee zawadi ya Galatone kwa kukupa facts!

Je hapa dar shule ya kupiga gitaa iko wapi ili tuwe wateja wa hizo gitaa???
 
Mkuu wanakupotosha bei inategemeana na gitaa ....mfanp Dar Yamaha galatoni ni SH. laki tano kuna mengine ni 250,000/= , mpaka ya 150,000/= yapo ! ya umeme ni hivyo mengine hadi laki 600,000/- ....Niletee zawadi ya Galatone kwa kukupa facts!

Hahaha powa ahsante
 
Acoustic ni laki mbili na nusu mpaka laki tatu.. Lakini kutokana na kampuni kama Yamaha huwa na bei zaidi.. Alafu umeme tupu huwa ni kuanzi laki tatu unusu na kuendelea... Ubora una matter pia na brand
 
Mkuu wanakupotosha bei inategemeana na gitaa ....mfanp Dar Yamaha galatoni ni SH. laki tano kuna mengine ni 250,000/= , mpaka ya 150,000/= yapo ! ya umeme ni hivyo mengine hadi laki 600,000/- ....Niletee zawadi ya Galatone kwa kukupa facts!
Huyu ndiye kajibu straight, wengine mnazunguka tuu
 
Gitaa nyingi bongo ni feki kuna brands wanaziingiza za kichina zinauzwa 250000-400,000 ila sio OG ikikutana na dhahma ya joto mfano Dar inabanduka na kupinda handle, kwa tunaoyaelewa magitaa tulikuwa tukinunua Nairobi au Padz shop alikuwa akiuza used guitars pale kkoo ila hayupo nowadays... Ukifungua duka la used guitars hasa za Europe utakuwa umetisha wateja wapo guitars za China japo wanaiga brand names zile kubwa kV fender bado ni counterfeit.... Leta biashara hiyo itakulipa.
SOME FACTS
°Makanisa ya Kilokole Ministries yameongezeka wanatumia sana guitars Hawa
° Night musical bands zinazogonga cover za oldies zipo za kutosha everywhere countrywide
°Congolese musicians hapa Dar ndio one stop city kwa ajili ya mahitaji yao ya affordable musical tools
°guitars za mchina zinakufa haraka kwa hiyo yakifa watakuja kwako kupata OG guitars
°brand new OG guitars zipo ila bei kali ukienda Morgan pale bass guitar OG hadi 800k
Leta mzigo huo biashara ipo zile siku za kwanzakwanza wekeza kuitangaza business yako wadau waijue,you win
 
Back
Top Bottom