Naomba kujua zaidi kuhusu 'Serum'

Titia

Senior Member
Jul 3, 2013
155
113
Habarini waungwana humu ndani.

Ninaomba kujua zaidi kuhusu serum na matumizi yake. Je, hazina madhara? Na ipi ni serum nzuri kwa matumizi ya usoni tu?

Nataka nitafute serum kwa ajili ya usoni tu, kupaka usiku, ili niwe na uso unaong'aa. Kwa sasa sina chunusi wala vipele ila kama uso wangu upo rafu hivi.

Asanteni.
 
Minazijua TU Serum.za kuchanganya na cream...Kwanini usitembelee maduka makubwa ya Urembo Kama SH.Amon na Mengine huenda wakawa na ushauri mzuri.
 
Sijui sana kuhusu Serum
Ila pia fanya scrub walau kwa wiki mara mbili pia

inasaidia kutoa ngozi ya zamani na kuleta mpya/that glow
 
Utumiaji wa serum na tundu za uso zimeziba ni sawa na bure.

Ukitaka serum hasa ya usiku ifanye kazi kwa ufasaha na upate hiyo glow n radiant skin fuata routine inayoeleweka.

Mfano waweza Tumia cleanser kila jioni..kwa ajili ya kuondoa vumbi na taka unazokutana nazo siku nzima..

Kisha waweza Tumia toner ya ngozi yako ..au hata alovera gel zile za dukani.

Sasa hapo waweza pakaa serum yako inayoendana na ngozi yako.

Kwa uso rafu tumia serum zenye kurepair ngozi ya uso

Ni vizuri pia Kufanya scrub walau Mara 2-3 kwa week hii inasaidia kuzibua tundu na kuondoa ngozi zilizokufa na kukuletea ngozi mpya.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom