Naomba kujua wakuu wa kurugenzi zote za CHADEMA

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,459
17,268
Habari wakuu
Naomba kuweka kumbukumbu zangu sawa, naomba kujua wakuu wa kurugenzi zote za chama cha demokrasia na maendeleo.

Kuna kitu naona hakiko sawa katika kumbukumbu zangu au katika taarifa zangu, naomba niwajue, ni kwa nia njema tu ya kupata taarifa na kuweka kumbukumbu zangu vizuri.

Naomba kuwajua hao wakuu wa idara na pia kujua wanatoka wapi, yaani kila mkuu wa idara anatoka mkoa gani.

Natanguliza shukrani.
 
Ungetaka kujua qualification zao ningekueleza ila hili la mikoa naona limekaa ndivyo sivyo.
 
Acha uk
Habari wakuu
Naomba kuweka kumbukumbu zangu sawa, naomba kujua wakuu wa kurugenzi zote za chama cha demokrasia na maendeleo.

Kuna kitu naona hakiko sawa katika kumbukumbu zangu au katika taarifa zangu, naomba niwajue, ni kwa nia njema tu ya kupata taarifa na kuweka kumbukumbu zangu vizuri.

Naomba kuwajua hao wakuu wa idara na pia kujua wanatoka wapi, yaani kila mkuu wa idara anatoka mkoa gani.

Natanguliza shukrani.
Bado tinaulizana Kanda na ukabila mpaka leo? Mbona wachina, wahindi na waarabu wamejaa kariakoo kwani ni kwao pale??
 
Kwani kuna shida gani kujua mtu anatoka mkoa gani, kuna ubaya gani katika hilo?

Hata wamarekani hua wanataja asili ya kiongozi wao, kama ni mmarekani mweusi au mlatini nk, mbona hua hawasemi ni mmarekani tu ikaishia hapo, kujua asili ya mtu hakuna ubaya wowote, wewe usietaka mtu ajulikane asili yake unataka kuficha nini?
 
Wanabodi nijuzeni kuhusu Afisa Habari wa CDM hivi sasa maana kwenye Msafari wa Kanda ya Kusini anayeripoti Taarifa ni MwanaHabari Huru wa JF. Muda mrefu sasa Mzee Tupatupa wa Lumumba ndiye mtoaji wa Taarifa mbalimbali.

Sijui ile Nafasi ya Afisa Habari imefutwa na kama ndivyo, itangazwe tupate kazi. Peopleeeeeeees!
 
Yaani lengo lako ni kujua mikoa wanakotoka wakurugenzi wa kurugenzi za chadema, ok ukishajua mikoa yao itakusaidia nini?. Hizi propaganda bora mziache maana sioni kama zinawapa faida yoyote.
 
Nanyie CHADEMA mmezidi unafiki na ukanda badilikeni
 
Yaani lengo lako ni kujua mikoa wanakotoka wakurugenzi wa kurugenzi za chadema, ok ukishajua mikoa yao itakusaidia nini?. Hizi propaganda bora mziache maana sioni kama zinawapa faida yoyote.
Kwani kuna shida mtu kujua wakuu wa kurugenzi za Chadema?

Kupata taarifa ni haki ya mtu
 
Kuwajua si kosa, na wewe hutaki tu kuwajua bali kujua mikoa wanayotoka. Mimi siangalii unachokisema bali unachokimaanisha au kukifikiria. Umejawa na mawazo ya kikabila, ukanda nadhani hata kwenye udini uko vzr
 
Back
Top Bottom