Naomba kujua sheria inasemaje manispaa inapokataa kutekeleza hukumu ya mahakama kuu?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
955
1,000
Wadau nilikuwa na Kesi ya Ardhi iliyoanzia Baraza la Ardhi la Wilaya hadi Mahakama Kuu kati yangu nikiwa Mmiliki wa Kiwanja kwa Hati Milki ya Miaka 66 na Mdai fidia wa Ardhi iliyopimwa hicho Kiwanja Ardhi ambayo yalikuwa Mashamba ya Wananchi ambayo Manispaa iliyachukuwa na kuwalipa fidia.

Hukumu ya Kesi hiyo Baraza la Ardhi Lilinipa Ushindi na kuagiza Vijumba vilivyojengwa kwenye Hicho Kiwanja Vibomolewa na Dalali wa Mahakama na Vilibomolewa na Mdai fidia Adai fidia ndio Haki yake. Mdai fidia alikata Rufaa Mahakama kuu na Uamuzi ukawa Huo Huo.

Tatizo lililopo ni Manispaa haitaki kumlipa fidia mhusika badala yake imempa Barua ya kuruhusu Akiendeleze Hicho Kiwanja.

Ombi langu kwenu ni hatua zipi nizifuate ili niweze Kukiendeleza Kiwanja Changu?
 

Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,750
2,000
Hapa Kuna mgogoro kati ya Mahakama na manispaa🤔🤔,Sasa sijui nan ana nguvu kuliko mwingine,ngoja waje wanasheria watutatulie hili!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom