Naomba kujua ratiba za masoko ya mnada

Dec 20, 2016
98
109
Habari mimi ni mfanyabiashara mdogo wa nguo za mtumba hapa Dar es Salaam nilikuwa nataka kuongeza wigo wa wateja kwenda minadani kuuza biashara.

Nilikuwa naomba kujua ratiba mbalimbali za minada kwa hapa Dar na utaratibu wa kuuza biashara mnadani

Msaada wenu tafadhali napatikana Mtongani
 
Msaada wenu tafadhari napatikana mtongani
Siku ya Jumatatu nenda Mbopo.....kuanzia hapo utapata msaada.....
 
Jumatatu (Bagamoyo Mbande Kinyerezi)

Jumanne (Kivule Tabata Barakuda na Boko)

Jumatano (Kibamba Chanika na Tabata Kimanga)

Alhamisi (Bunju Moshi Bar na Tungi Kigamboni)

Ijumaaa (Kitunda Majohe Viwege na Kunduchi)

Jumamosi (Kibaha Loliondo Pugu Kajiungeni Kinondo I Biafra)

Jumapili (Machimbo Salasala Geza Kigamboni)
 
1000788518.png

Unajiuliza ukauze BIDHAA zako wapi?

Sio lazima ukae kwenye frem yako kila siku kusubiri wateja, unaweza kutafuta siku ambazo kuna Gulio maeneo mbalimbali ukaenda kuuza bidhaa zako.
.
Pia hii ni sehemu nzuri kwa wasio na frem. Fuata wateja walipo.
.
Uzuri wa siku za gulio kunakua na watu wengi hivyo uwezekano wa kuuza ni mkubwa.
.
Aya unaweza kuhudhuria haya masoko kwa watu wa Dar es Salaam na Pwani

Kunduchi Mtongani - IJUMAA.

Tegeta Mkanada _Jumamosi

Boko Chama _Jumanne

Bunju B _ Alhamisi .

Tabata Segerea (Barakuda) - Jumanne

Kimanga - Jumatano

Goba _Jumatano AU Jumapili .

Bagamoyo _ Jumatatu

Kibamba -jumatano
Pugu kona/ Kajiungeni _ jumamosi
Viwege kwa Mpemba_ ijumaa
Ubungo mawasiliano _ Ijumaa.
.
Chanika _Jumatano.
Tegeta_Ijumaa.
Kinondoni B_ jumamosi
Madale mwisho _jmosi.
.
Mbande - Jumanne.
Kinyerezi_ Jumatatu
Kinondoni Biafra_ Jumamosi
Kitunda _ ijumaa
lugoba_Jumatatu
Msata _Jumanne
Chalinze - Jumatano
Mbande _Jumatatu
Kivule _Jumamosi
Kigamboni geza _Jumapili
Kigambonimnadani _ Alhamisi.
Kigamboni_Ungindoni Jumanne.
.
Kibaha kwa Mathias_ Ijumaa.
Kibaha Loliondo _Jumamosi
Kibamba_Jumatano
.
Gulio ni sehemu maarufu kwaio ukifika huko unaweza kuulizia hasa ukaonyeshwa sehemu.
.
Kwenye magulio huwa kunakua na ushuru kidogo utalipia ikiwepo.
.
Kama wewe ni Mjasiriamali au mfanyabiashara usikae sehemu moja, unaweza kuzungukia magulio (masoko) kuuza bidhaa zako.
.
Tuambie, Sehemu gani nyingine kuna gulio? Una uzoefu gani na haya magulio kwenye kuuza bidhaa?

Magulio zaidi angalia comments za hii post na magulio nje ya Dar es Salaam pia follow IG @kelvinkibenje
 
Habari mimi ni mfanyabiashara mdogo wa nguo za mtumba hapa Dar es Salaam nilikuwa nataka kuongeza wigo wa wateja kwenda minadani kuuza biashara.

Nilikuwa naomba kujua ratiba mbalimbali za minada kwa hapa Dar na utaratibu wa kuuza biashara mnadani

Msaada wenu tafadhali napatikana Mtongani
Wilaya ya Kiteto: ni x 14 au 15(minada yenye mifugo) kwa mwezi na Magulio ni kila siku. Karibu sana mkuu. Kuna Kata 23 na Tarafa 7. Kazi kwako usishupalie Dar tu, njoo hata huku pia. Barabara/Njia zinapitika mwaka mzima.
 
saitaa
 
Back
Top Bottom