Naomba kujua namna sahihi ya matumizi ya maneno 'sorry' na 'excuse me'

Hii kwa mujibu wa kamusi ya TUKI kuwa "sorry" ni "samahani"
View attachment 1256098



Mimi ninasema kuna mapungufu, ukizingatia kiswahili ni lugha finyu kwa maneno kulinganisha na kiingereza.

Samahani ni Excuse, na Sorry ni pole au -sikitika. Sorry ni neno la kuonyesha masikitiko baada ya kutokea jambo la baya.

Na Excuse ni neno la kusema/ kuomba kabla ya mtu hajafanya usumbufu kwa watu au mtu mwingine.

Nasema katika hiyo tafsiri ya TUKI kuna mapungufu na Wanatakiwa wafanye maongezeko na mabadiliko katika editions zingine.
 
Vile vile kwa mujibu wa google translate neno "sorry" ni "samahani"
View attachment 1256100


Hivi mfano, unaposema:- I am sorry to announce the death of Mr Simon.

Hapo utasema maana yake ni; Samahani kwa kutangaza kifo cha Bwana Simon? au maana yake ni; Ninasikitika kutangaza kifo cha Bwana Simon?

Shida iliyopo ni kushikilia maneno yanayotumika (informally /loosely ) na kuyafanya kuwa formal na mbaya zaidi watu hawafanyi utafiti wao binafsi na wanashindwa kugundua makosa.
 
Mokaze,
Nilichokuwa nakieleza nimerejea tafsiri ya kimazingira na sio tafsiri ya neno kwa neno na ndio maana nikaeleza kuwa neno "sorry" linaweza kuwa na maana ya samahani au pole vile vile ukiangalia samahani(nomino) na samahani(kitenzi) haibaki vile vile kuwa "sorry" na pia tukumbuke urasmi wa lugha hauzuii usahihi wa lugha mwisho pia nakubaliana na wewe kuwa inawezekana Kiswahili kikawa na msamiati michache na ndio maana tafsiri ya kimazingira huwa naitumia zaidi.
 
Nilichokuwa nakieleza nimerejea tafsiri ya kimazingira na sio tafsiri ya neno kwa neno na ndio maana nikaeleza kuwa neno "sorry" linaweza kuwa na maana ya samahani au pole vile vile ukiangalia samahani(nomino) na samahani(kitenzi) haibaki vile vile kuwa "sorry" na pia tukumbuke urasmi wa lugha hauzuii usahihi wa lugha mwisho pia nakubaliana na wewe kuwa inawezekana kiswahili kikawa na msamiati michache na ndio maana tafsiri ya kimazingira huwa naitumia zaidi.


Msamaha= nomino, samehe= kitenzi, samahani= kielezi.

Bado Sorry haiwezi kuwa na maana ya samahani, kama ni hivyo Excuse ina maana gani? Je, mahali pa Excuse unaweza kuweka sorry?.

Tusishikilie makosa ya kimazoea na kuyahalalisha, (justification of common mistake in language.)🤣🤣
 
Msamaha= nomino, samehe= kitenzi, samahani= kielezi.

Bado Sorry haiwezi kuwa na maana ya samahani, kama ni hivyo Excuse ina maana gani??, je mahali pa Excuse unaweza kuweka sorry??.

Tusishikilie makosa ya kimazoea na kuyahalalisha, (justification of common mistake in language.)🤣🤣
Ni ukweli upo sahihi 😬
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom