Habari... kwa mara ya kwanza kama unasafiri na bus utashuka... NAMAIBA BUS STATION [emoji579].. kwa ndege utashuka ENTEBE...mjini kuna HOTELS, LODGE n.k price ni kuanzia shs 30,000/= 40,0000/= UGX (UG SHS).
Kama chuo kipo mjini KATI kuna sehemu inaitwa Kansanga, makindye.. huko kuna vyumba vya kupangisha kwa bei nafuu kuanzia shs 70,000/= za kiganda na watanzania wengi huishi huko.. lakini pia zipo hostel ambazo zina ubia na vyuo husika na Gharama zao huwa zina range kuanzia shs 450,000/= (UGX) mfano ipo inaitwa MACHAKOS pale Kansanga.. na malipo haya ni kwa semester nzima maji, umeme, ulinzi included pia wanaruhusu kupika... Hivyo inategemea na uwezo wako zipo mpaka hostel za 800,000/= kwa semester.
Ukiwa NAKAWA TOWN karibu na MUBS branch ya Makerere University pia zipo hostel za shs 250,000/= 350,000/= n.k (UGX).
fedha ya uganda na Tanzania zinapishana... ya uganda ipo chini kidogo... Na kiwango cha chini cha RATE huwa ni 1.5
10,000/= (TSHS) X 1.5 =15,000/= (UGX)
100,000/=(TSHS) X 1.5 =150,000/= (UGX)
unaweza ukaona kiwango cha mabadiliko ya fedha hapo.
KAMPALA mjini % kubwa wanaishi watu wa kabila waganda na huwa wanazungumza LUGANDA na ENGLISH... Ni mji ambao watanzania, wa sudan, wa kenya, Eritrean, Ethiopian, Rwandans, n.k wapo wengi sana hivyo hutohisikia mpweke daima.
Suala la maadili, tabia, na mwenendo ni Jukumu lako kutambua unaenda wapi kufanya nini... Kuna makanisa na misikiti kama TANZANIA, kuna walevi, wahuni, wezi, wanaojiuza, wanaofanya biashara haramu, na kila aina ya uchafu unaofikiri upo hapa DSM basi hata KAMPALA upo... NB: Rate ya maambukizi ya UKIMWI ni kubwa sana.
FREEDOM NI KUBWA SANA... tofauti na huku..La msingi Amini kuwa Mungu Ndio atakuwa mwenyeji wako huko ukifika mtegee yeye Atakulinda.
WELCOME TO KAMPALA. (UGANDA)