JIGOKU IKAYA
Member
- Apr 29, 2017
- 38
- 46
Mimi ni Mwl, mwaka Jana nilisimamia mtihani drs la nne. Baada ya semina mkurugenzi alitulipa elfu 35, akasema tudai elfu kumi. Baada ya hapo tukapangiwa shule za kusimamia. Tulitakiwa kusimamia Siku tatu. Kila Siku elfu 30, kwa hiyo 30000*3=90000+10000 ya semina ni 100000. Aisee toka mtihani huo wa taifa ufanyike na matokeo baraza likatoa, hakuna malipo wala majibu au ufafanuzi wa stahiki za wasimamizi hao. Naomba serikali na wadau wa ELIMU mtolee maelezo japo mafupi ya maswali haya; 1.Pesa hii inalipwa na nani? 2. Je, halmashauri hazijalipa? 3. Na kama wengine wamelipwa nn kifanyike kwa halmashauri ambazo hazijalipa?. Kutoka halmashauri ya BARIADI VIJIJINI. Nawasilishaa karibuni kwa maoni wadau.