Naomba kujua kuhusu déjà vu

Naomba kujua kuhusu déjà vu

Sijui aisee kama ndio deja vu au laa. Ila niliwahi kusoma humu uzi wa @Pasco kuhusu Psychic Powers ambazo kila mtu anazo tangu utoto ila huwa zinapungua/zinazidiana kadri ubongo unavyozidi kujaa mambo mengi ya nje. Tafuta huo uzi utaelewa zaidi.

Hilo suala la kumkumbuka mtu then ukamuona siku hiyo pia ni uwezo wa akili sjui niite ni connection kati ya mtu na mtu ila kwa mimi ilikuwa inanitokea kwa jamaa yangu mmoja tu ambaye nimekaa nae kwa muda wa miaka mitatu ila sikuwahi kujua anapokaa na ilikuwa nikimuuliza hataki kusema.

Huyu jamaa ilikuwa siku nikimuwaza au kumkumbuka ni lazma siku hiyo nionane nae. Lakini baadae nikaja kujua kuwa hakuwa binadam.

By the way tafuta huo uzi wa @Pasco.

Shukran.
😁
 
Habari zenu .....
Wanajamvi naomba kujua sababu ya kuona vitu au siku zinajirudia yani naweza kukaa siku nikaona kama matukio yanajirudia Yan nikaona kama hiyo siku nilishawahi kuiona na kufanya hayo mambo yanayotendeka kwa muda huo....

Pia naweza kuwa nimemkumbuka mtu halafu namuona hata kama hatujaonana siku au muda mrefu au naweza kuhisi mtu fulani atanipigia simu na anapiga simu siku hiyo .Je hii ndo de javu au kuna kitu kingine.

Umewahi kuwa na hisia za kufanya jambo fulani, kutamka maneno, kufika sehemu fulani au kupitia hali mpya ambayo unadhani tayari umewahi kuwa nayo hapo awali? Huwa una hisia kwamba baadhi ya mambo yanayokwenda kutoea huko mbele tayari unayafahamu?

Hisia hizo mara nyingi hufafanuliwa kama Déjà Vu, maneno ambayo kwa lugha ya kifaransa humaanisha “Jambo ambalo tayari umewahi kuliona”

Takwimu

Utafiti wa Marija Bošnjak Pašić et al (2018) wenye kichwa cha habari “Many Faces of Déjà Vu: a Narrative Review” unafafanua kuwa takriban 97% ya binadamu wote wamewahi kupatwa na hali hii walau mara moja kwenye kipindi fulani kwenye maisha yao na 67% wakipatwa na hali hii mara kwa mara.

Déjà Vu hutokea zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 15-25 na huendelea kupungua kadri umri unavyozidi kuongezeka. Pia, watu wanaokumbuka ndoto, wanaosafiri mara kwa mara, wenye mkazo (stress) pamoja na wale wanaofanya kazi ngumu sana zinazowaweka kwenye mazingira ya kuwa na uchovu mkubwa mara kwa mara huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupatwa na hali hii.

Chanzo cha Déjà Vu
Sababu za kutokea kwa Déjà Vu huwa hazipo wazi sana. Lakini, tafiti nyingi za afya zinataja uwepo wa changamoto za kimawasiliano kwenye mfumo wa taarifa za fahamu za ubongo kuwa ni chanzo cha kutokea kwa hali hii hasa ikiwa degedege/Kifafa kinachoanzia kwenye eneo la ubongo ambalo kitaalam hufahamika kama temporal lobe (Temporal lobe seizures/epilepsy) kitatokea.

Pia, wanasayansi wengine huamini kuwa hali hii husababishwa na changamoto za kiutendaji zinazotokea kwenye ubongo wakati wa kutekeleza majukumu yake.
 
Back
Top Bottom