Naomba kujua kuhusu déjà vu

naomba unielekeze jinsi ya kufanya meditation au kuna sehem watu wana fanya meditation mkuu
 
sijaelewa mkuu
 
mkuu kama umeajiriwa, na unakatwa ile 18%

acha kazi maana njia yako umeshaiona

uwe mtabiri utapiga pesa mingi sana,

trust me, maana na mimi nilishakuonea hii ninayokwambia
naanzaje kua mtabiri? nifafanulie vizuri nielewe
 
Hii story yako pia ianzishie uzi mkuu, jamaa alikuwa nani? na ulijuaje? alikuwa mwema au mbaya kwako?
Karibu
 
Hii story yako pia ianzishie uzi mkuu, jamaa alikuwa nani? na ulijuaje? alikuwa mwema au mbaya kwako?
Karibu

Jamaa alikuwa ni mwema tu japo aliwahi kuniambia kuwa ametumwa na wakubwa wake aje kunichukua anipeleke ujinini ila anashindwa coz kuna nguvu zinanilinda hivyo anashindwa kunichukua.

Ikamlazimu yeye kushindwa kutimiza hilo jambo na akawa anaogopa kurudi ujinini bila ya kurudi na kile alichoagizwa (MIMI).

Mpaka kulala nae nlikuwa nalala nae usiku mambo nliyokuwa nikiyaona acha tu. Majini bwana wana vituko sana.
 
Basi ni sawa wakuu ntalifanyia kazi hili wazo wandugu.

Ila kiukweli hawa viumbe tunapishana nao sana mitaani na haya mambo yapo wakuu.

Tuko pamoja wandugu.

Thanks.
Na mimi unitag mkuu.
 
Mkuu naomba utupe japo kahistoria flan hiv kuhusu huyo jamaa yako wa ajabu kwan mlikutana katika mazingira gani na ilikuwaje ukajua kama sio binadamu?
 
inaonekana ni story nuri sana embu mkuu fikiria namna ya kuiandika tupate faida kidogo

mana kusoma icho kipande tuu nimekuw na maswali kama buku ivi kichwani mwangu

fanya ivyo mkuu
 
Mkuu naomba utupe japo kahistoria flan hiv kuhusu huyo jamaa yako wa ajabu kwan mlikutana katika mazingira gani na ilikuwaje ukajua kama sio binadamu?

Mkuu jinsi nilivyokutana nae mbona nimeeleza hapo nyuma na pia jinsi nlivyokuwa nikiishi nae yale matukio na vituko alivyokuwa akivifanya ndio vilinifanya nijue kuwa sio binadam.

Soma post #51 ameni-quote themanhimself nimeeleza jinsi nilivyokutana nae mkuu.

Thanks.
 
Ndio yenyewe.
 
Basi ni sawa wakuu ntalifanyia kazi hili wazo wandugu.

Ila kiukweli hawa viumbe tunapishana nao sana mitaani na haya mambo yapo wakuu.

Tuko pamoja wandugu.

Thanks.
Ukifungua uzi fanya kunitag mkuu
 
Hii ni hali inayo mtokea mtu pale ubongo unapofeli kutafsiri muda halisi wa tukio. i.e; present event is interpreted as past event

Cc: Jimena
 
kuna mambo mnayazungumza naona kama yanaukweli ndani yake kwaupande wangu kuna mambo nimesha yazoea sana sasa mfano kila nikipata tatizo lolote liwe kujibizana au hata ugonvi lazima jana yake nitakuwa naota nafukuzwa na simba au namfukuza paka nimesha zoea kujua kesho yangu kama kutakua na tatizo sasa kibaya zaidi mtu nikimuwaza sana au kumkumbuka lazima siku hiyo nimuone japo historia yangu ina utata kidigo kuna wakati sasa hata tukiwa wawili tukiwa umenyamaza ikitokea tu nimewaza wimbo flani basi wewe utaimba kwawakati huo kwakifupi nimekua ni mtu wamachale machale mfano kila ninapo ota ndoto za kutisha mfano kuona baazi ya ngugu ambao wamesha tangulia mbele za haki mfano hasa babu yangu lazima kesho nipate pesa kwa njia yoyote ila sasa huyu babu alitokea kunipenda utotoni na alinitabilia mambo kuhusu maisha yangu ambayo 80% nikweli yanatimia ila alikuwa ni mtemi huko kijijini unyamwezini hebu nisaidieni au kunamambo alinifanyia au ni karama niliyo pewa namungu
 
Mkuu hali hiyo ni bahati sana na inawatokea wachache sana, pia wala hauhusiani na uchawi kama wengi wanavyofikiri ila ni namna ambavyo mwenyezi Mungu anawasiliana nawewe kwa kukuonesha ya mbeleni.

Biblia inasema wazee wenu wataoteshwa ndoto na vijana wenu wataona maono.

Halafu kuhusu hiyo ndoto ni ndoto zenye maana na inahitaji tafsiri tu...na kwa waombaji hasa wanajua maana zake.

Mfano ndoto ambayo ni common kwa watu wengi ni hizi:-

1) Kuota kufukuzwa na ng'ombe mkubwa mwenye mapembe

2) Kuota kudumbukia katika shimo refuuu ila hufiki chini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…