Naomba kujifunza kwa kuona na maelezo kuhusu kufuga Nguruwe

SHAIDI

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
291
141
Habari
Naomba mtu yeyote anaefuga nguruwe nimtembelee na kuona ili kujifunza zaidi
Naishi dar niko tayari kufika kokote pembezoni mwa dar kama mkuranga, rufiji, kibaha, mlandizi, morogoro na bagamoyo
No 0715034565 nitashukuru kupata ushirikiano wenu.
 
Habari
Naomba mtu yeyote anaefuga nguruwe nimtembelee na kuona ili kujifunza zaidi
Naishi dar niko tayari kufika kokote pembezoni mwa dar kama mkuranga, rufiji, kibaha, mlandizi, morogoro na bagamoyo
No 0715034565 nitashukuru kupata ushirikiano wenu.
Mkuu funga safari uende SUA ukajifunze kufuga nguruwe!!
 
Mimi sifugi nguruwe ila nimepata kuwa karibu na rafiki yangu mmoja yeye alifuga nguruwe wengi zaidi ya mia mbili lakini walimshinda kwani hawakuwa na faida.

Kutokana na kua nae karibu yapo mengi nimeweza kufahamu kutoka kwake na mengine nimeweza kuona kwa macho.

Huu ndio ushauri wangu kwako:
Changamoto kubwa ya nguruwe ni kivipi utaweza kumlisha chakula kiasi ila chenyevirutubisho lakini kwa gharama ndogo tangu akiwa mdogo mpaka atakapofikia kuuzwa.

Nguruwe si wamagonjwa mogonjwa ila usipokua makini utakua huna tofauti na mtu alieweka pesa yake bank.

Hivyo wakati unatafuta dondoo za fugo ya nguruwe jitahidi sana umpate mtu aliefanikiwa kwenye kutumia gharama ndogo za malisho ili kupata faida.

Lakini pia jografia ya mkoa husika nayo inaweza kusaidia kupata vyakula hata visivyo na gharama kabisa mfano mikoa yenye hali ya hewa oevu kama morogoro ambapo majani mara nyingi ni kijani kwa muda mrefu unaweza punguza gharama kubwa kwa wakati mwingine kuwalisha majani badala ya pumba ambayo ni ghali.

Sehemu kama Ifikara Morogoro mfano kijani hupatikana kwa muda mrefu lakini pia pumba ya mpunga(Poladi) hupatikana kwa gharama ndogo sana.

Nimekupa mfano wa rafiki yangu aliyeshindwa lengo si kukuvunja moyo bali kukupa makosa yake yakutotafuta namna yakuwalisha kwa gharama ndogo ili usije ukapata hasara.
Ni vema ukafika SUA kama ulivyoshauriwa na mkuu hapo juu.
Kila la heri!
 
Hello..... Karibuni Sana Katika group linalohusu ufugaji wa nguruwe

Karibu Sana wewe mtaalamu wa mifugo, mfugaji, mnunuzi, pamoja na Wale wenye kiu ya kujifunza zaidi kuhusu ufugaji huu wenye tija na kipato cha uhakika.....

Click link ifuatayo kujiunga......

Zingatia kujitambulisha pindi tu uingiapo katika group hili
ZINGATIA KUJITAMBULISHA PINDI TU UINGIAPO KATIKA GROUP HILI... JINA, MKOA, SHUGHULI

TSA- PIG FARMING
 
Back
Top Bottom