Naomba kufahamu ubora wa hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma

miss chuga

JF-Expert Member
Dec 25, 2019
303
651
Habari za mda huu wapendwa? Poleni na majukumu.

Mimi nipo Dodoma ni mama kijacho wa miezi 2.5 hivyo nimepanga nianze kliniki katika kuumiza akili nianze huduma hii hospital ipi Kuna mtu akanishauri nianze hospital ya Benjamin mkapa iliyopo UDOM pia akanishauri Mungu akinijalia nijifungulie huko huko Benjamin Wana huduma nzuri.

Mimi bado sijafikia muafaka coz sijawahi kwenda kufanya huduma hapo Benjamin.

Naombeni mnisaidie kwa anayeifahamu vizuri hii hospital au ambaye ameshawahi kutibiwa pale mnipe sifa zake Kama huduma ziko pouwa kweli nianzie kliniki pale pia nijifungulie pale na Kama haziko pouwa naomba pia mnishauri hospitali gani nyingine nzuri kwa Dodoma kuanza kliniki na kujifungua.

Asanteni sana na Mungu awabariki kwa ushirikiano wenu
 
Hongera Kufanikisha Jambo Hilo
Kwanini Uende Mbali? Unaishi Sehemu Gani Dodoma Hapo
Benjamin Mkapa Hospital Wanajitahidi Sana Pazuri
Nimefika HHapo Mara Kadhaa
 
Hongera Kufanikisha Jambo Hilo
Kwanini Uende Mbali? Unaishi Sehemu Gani Dodoma Hapo
Benjamin Mkapa Hospital Wanajitahidi Sana Pazuri
Nimefika HHapo Mara Kadhaa
Asante kwahiyo unanishauri niende huko Mimi naishi mnadani jirani na chuo Cha mipango
 
Asante kwahiyo unanishauri niende huko Mimi naishi mnadani jirani na chuo Cha mipango
Hapo Mnadani Kuna Kituo Cha Afya. Ukiona Haifai Njoo Hapa Wajenzi Kuna Kituo Pia Cha Afya Ama Makole. Clinic Huwa Huhitaji Kwenda Mbali Mpaka Mkapa labda Kama Una Jambo Special.

Mimi Ni Mjumbe Wa Serikali Ya Mtaa Dodoma. Benjamin Mkapa Iko Vema Sana Lakini Ni Mwendo.

Utoke Mnadani Sijui Wa Zamani Ama Mpya
 
Hapo Mnadani Kuna Kituo Cha Afya
Ukiona Haifai Njoo Hapa Wajenzi Kuna Kituo Pia Cha Afya Ama Makole. Clinic Huwa Huhitaji Kwenda Mbali Mpaka Mkapa
Labda Kama Una Jambo Special.

Mimi Ni Mjumbe Wa Serikali Ya Mtaa Dodoma
Benjamin Mkapa Iko Vema Sana Lakini Ni Mwendo
Utoke Mnadani Sijui Wa Zamani Ama Mpya
Asante sana kwahyo kliniki naweza kufanya popote na kuhusu kujifungua unanishaurije?
 
Asante sana kwahyo kliniki naweza kufanya popote na kuhusu kujifungua unanishaurije?
Ninachojua Kama Huna Tatizo Lolote
Clinic Unafanya HHuku Mipango, Wajenzi, Makole
Ila Wakati Ukikaribia Ndiyo Unakwenda Benjamin Mkapa
 
Mimi ningekushauri uende hospitali ya chuo kikuu cha DODOMA iko college of informatic.

Ni hospital maalumu kwa ajili wazazi.

Ni hospitali nzuri sana inahudumia wanafunzi wachache na raia.

Mke wangu alijifungulia pale. Hakuna foleni na kuna watoa huduma wa kutosha na wazoefu.
 
Asante kwahiyo unanishauri niende huko Mimi naishi mnadani jirani na chuo Cha mipango
Ebu panda dalada ya kutoka mipango, kisha shuka kituo cha Nam area C, kisha vuka barabara upande wa pili.

Hapo utapata Zahanati nzuri tu, na utahudumiwa vizuri kwa hitaji lako.
Mkapa hospital ni vyema ukaenda ukuwa na complicated issue.

Otherwise ukitaka uhudumiwe chap, ebu nipitie hapa Reef One twende kama Mr and Mrs
 
BMH wako vizuri. Wife alideliver pale recently. Changamoto kwako ni distance. chukua maoni ya mjumbe hapo juu clinic uende Kituo cha Afya cha Karibu. Vinginevyo kama una complication fulani fulani.
 
BMH wako vizuri. Wife alideliver pale recently. Changamoto kwako ni distance. chukua maoni ya mjumbe hapo juu clinic uende Kituo cha Afya cha Karibu. Vinginevyo kama una complication fulani fulani.
Asante sana, hivi na gharama zao zipoje maana wewe wife wako amejifungua hapo na uhakika utakuwa unazifahamu gharama zao
 
Asante sana kwahyo kliniki naweza kufanya popote na kuhusu kujifungua unanishaurije?
Klinik fanya Mary Imakulata wapo vema Kishakama unataka kujifungua kea upasuaji nenda Benjamin au Ntyuka DCMC.

Na Kama kawaida nenda General hospital Kama uzazi ni wa kwanza
 
Back
Top Bottom