Naomba kufahamu mamlaka ya Afisa mtendaji kata na Afisa Tarafa

mzee Chibai

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
980
242
Wakuu naomba kujua mamlaka ya Afisa mtendaji kata na Afisa Tarafa maana hawa watu wana nguvu sana kwenye maeneo yao kuna sehemu unakuta mtu anakubali kupelekwa polisi lakini sio kwa Afisa mtendaji kata au Afisa Tatafa.
 
Anahusika na kusimamia miradi ya maendeleo katika vijiji vinavyounda Kata husika
 
Hawa watu majukumu yao yametofautiana kidogo sana,afisa tarafa yeye no mwajiriwa wa serikali kuu na anakuwepo ktk mamlaka ya DC na ana report kwa dc,yeye ni msimamia Sera ktk level ya tarafa,afisa mtendaji wa kata yeye ni mwajiriwa was serikali za mitaa na anakuwa chini ya mkurugenzi mtendaji,na kazi zake nikutekeleza sera,na ana report mojakwa moja kwa mkurugenzi mtendaji,
 
Jaribu kugoogle. Kuna kitabu nilikuwa nacho miaka ya nyuma kinaeleza majukum yao, nadhan kilifadhiliwa na Germany embassy kama sikosei
 
KAZI NA WAJIBU WA AFISA MTENDAJI WA KATA
Kutokana na Waraka Wa Maendeleo ya Utumishi wa Serikali za Mitaa namba 29 wa Mwaka 2003, pamoja na sheria iliyofanyia marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006 kazi za Afisa Mtendaji wa Kata ni:_

•Kumwakilisha na kumsaidia Mkurugenzi wa Halmashauri katika kusimamia shughuli za maendeleo katika kata;

•Kuandaa mpango kazi kuhusu kazi na wajibu wake na kuuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmshauri; •Kuwasimamia maafisa watendaji wa Vijiji katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo;

•Kushiriki na kushauri wakati wa uandaaji wa mipango ya maendeleo ya kata, kuratibu mipango kazi na taarifa za utekelezaji za Watendaji wa Vijiji katika kata na kuiwasilisha kwa Afisa Tarafa na kwa Mkurugenzi wa Halmashauri;

•Kushiriki, kushauri na kuwasilisha kwenye kamati ya maendeleo ya kata taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli ndani ya Kata;

•Kuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya kata;

•Kusimamia sheria ndogo zote katika kata;

•Kuhimiza uanzishaji na uendelezaji wa vyama vya ushirika na ujasiriamali na shughuli za ndani ya kata;

•Kupanga na kuratibu shughuli na kutoa msaada na ushauri kwa wakazi katika kata;

•Kuandaa na kuwasilisha kwa Halmashauri ya kijiji na Halmashauri ya wilaya mapendekezo ya kutunga sheria ndogo kuhusiana na shughuli za Kata;

•Kusimamia ukusanyaji wa mapato;

•Kuanzisha na kuimarisha maendeleo shirikishi katika kata;

•Kudhibiti majanga ndani ya kata;

•Kuimarisha masuala ya jinsia ndani ya kata;

•Kuwasimamia maafisa watendaji wa Mitaa katika kutekeleza majukumu yao;

•Kuwa mjumbe wa kamati ya maendeleo ya wilaya (DCC);

•Atakuwa kiungo cha uongozi wa Idara zote katika Kata na atashughulikia masuala yote ya uendeshaji katika Kata chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji;

•Mlinzi wa Amani katika Kata yake;

•Mratibu na Msimamizi, Mpangaji wa utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kata;

•Msimamizi wa utekelezaji wa sheria ndogo za Halmashauri katika Kata yake;

•Atafanya kazi zingine zote kama atakavyoagizwa na Mkurugenzi wa Halmashauri.



KAZI ZA AFISA TARAFA
Katika kurahisisha mawasiliano Afisa Tarafa ni kiungo kati ya ngazi ya Kata na Halmashauri kwa upande mmoja na Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa upande mwingine, majukumu ya Afisa Tarafa yameainishwa katika Mwongozo wa Uwajibikaji wa Maafisa Tarafa katika Wilaya na Halmashauri za Serikali za Mitaa wa tarehe 18 Desemba, 2003 pamoja na Sheria iliyofanyia marekebisho Sheria za Serikali za Mitaa namba 13 ya mwaka 2006 Majukumu ya Afisa Tarafa ni kama ifuatavyo:-

•Kumwakilisha Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza shughuli za serikali katika Tarafa;

•Kuandaa na kusimamia taarifa au habari kuhusu ulinzi na usalama katika kata zilizomo ndani ya

•Tarafa na kuziwasilisha kwa Mkuu wa wilaya na kwa Mkurugenzi;

•Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na Sera za Serikali kuu ndani ya Tarafa;

•Kuelimisha na kuwahimiza wakazi ndani ya Tarafa kushiriki katika shughuli za maendeleo;

•Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na wakazi ndani ya Tarafa;

•Kushughulikia malalamiko ya wakazi ndani ya Tarafa;

•Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya Tarafa na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya;

•Kuratibu shughuli zote zinazohusu majanga na dharura ndani ya Tarafa;

•Kushiriki kama mjumbe kwenye vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Wilaya DCC;

•Kumwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri na Katibu Tawala wa Wilaya katika kusimamia maendeleo ya eneo lake;

•Kuandaa ratiba ya kazi yake ili kuonyesha majukumu na muda wa utekelezaji ili kuondoa mgongano wa majukumu unaoweza kutokea kutokana na maagizo mbalimbali ya ngazi za juu na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji;

•Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji katika eneo lake;

•Kushiriki na kutoa ushauri kuhusu Upangaji wa Mipango ya Maendeleo katika eneo lake;

•Kuratibu ratiba ya kazi za Maafisa Watendaji Kata wa eneo lake na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji na kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya; •Kuhudhuria Mikutano ya Baraza la Madiwani la Halmashauri na kutoa ushauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa shughuli zilizofanyika katika eneo lake;

•Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata na Vijiji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na nakala kwa Mkuu wa Wilaya/Katibu Tawala wa Wilaya;

•Kuwa Katibu wa vikao vitakavyowahusisha Watendaji Kata, Madiwani na Wataalam waliopo katika eneo lake;

•Kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo za Halmashauri;

•Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na Mkuu wa Wilaya.
 
Back
Top Bottom