Naomba kufahamu kuhusu Saadani National Park

Naomba kufahamu kuhusu Saadani National Park

kijani11

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
8,393
Reaction score
9,242
Habari za pilika pilika wadua.

Baada ya kupita pita sehemu zingine nikitafuta taarifa hizi, nimepata ambazo bado hazijakidhi kiu yangu hivyo ningependa kupata msaada wa haya.

Nilikuwa naomba kufahamu yafuatayo kuhusu hifadhi ya Saadani, kwa kuwa mimi na wenzangu tuna lengo la kutembelea hifadhi hiyo kipindi cha mwezi December

1. Malazi nafasi zake na gharama.

2. Gharama za kutembezwa kwa gari na boat pia.

3. Kuhusu chakula na upatikanaji wake.

4. Iwapo kuna jambo lingine muhimu la kuzingatia.

Je kuna ulazima wa kufanya booking ya huduma hizo kabla ya kufika kwenye hifadhi?

NB: ni kwa kikundi cha watu wa kipato cha kati wasiozidi kumi.
 
Nilifanya field huko wanyamapori walio wengi ni tembo haina wanyamapori wengi sana kinachofurahisha ni hifadhi inayounganishwa na bahari kwa hiyo unaweza uka fanya utalii hadi majini kwa kutumia boat
 
Nilifanya field huko wanyamapori walio wengi ni tembo haina wanyamapori wengi sana kinachofurahisha ni hifadhi inayounganishwa na bahari kwa hiyo unaweza uka fanya utalii hadi majini kwa kutumia boat

Vipi issues za malazi na gharama kama ulifuatilia.
 
Kuhusu gharama sikufuatilia jaribio kuingia kwenye website ya tanapa huenda viwango vya gharama za huduma vikawa Sawa
 
nimefika saadani mara kibao tu
malazi na usafiri nashauri mfanye booking kabisa
kuna gesti za kiwango duni kabisa, nzuri za kawaida, na nzuri zaidi za kitalii
so wewe tu na bajeti yako
 
Tanapa wana hostel pale Saadani nilikwenda muda sana ilikuwa elfu50 ila kuna wakati watu walilalamika cost zipo juu sasa sina hakika kama zilipungua cost za hostel za tanapa.
Ila usiende bila kuweka appointment mana unaweza kuta papo ful
 
asnte mkuu. Nitalifanyi kazi.
 
nimefika saadani mara kibao tu
malazi na usafiri nashauri mfanye booking kabisa
kuna gesti za kiwango duni kabisa, nzuri za kawaida, na nzuri zaidi za kitalii
so wewe tu na bajeti yako

Nimekuelewa mkuu
 
Jamani mi nauliza tu. Nataka kufahamishwa tofauti kati ya mbuga na hifadhi ya taifa. Natanguliza shukrani.
 
Nakushauri usiende ,mana mbuga ya saadan hutaona hata sungura pori ..me nilienda lakn kiukweli niliona ngiri peke yake
 
wanyama wapo bana huyo asikuzingue
Aseme kama aliende eneo linaitwa serengeti ndogo akakosa wanyama
 
Kaundime me saadan naijuwa vzr tu ..c mbaya mwache aende then atatupa report
 
Ni
Mkuu ulienda hiyo safari naomba share experience hapa
Ni hifadhi nzuri sana kwa anayependa mapumziko yenye utulivu na kupata wasaa wa kuzunguka kutazama wanyama (ila wanyama wanaooneka zaidi ni Twiga,Tembo, Ngiri bila kusahau viboko na Mamba kama utafika mtoni)

Kuna utalii wa kwenye maji pia (kuna boat mnalipia na kuzunguka mtoni kiasi na mpaka mto unapoingia baharini)

Kwa anayeenda azingatie haya (labda kama kuna mabadikiko kwa sasa)

1. Ni vyema uwe na usafiri binafsi kama utataka kuzunguka katika hifadhi

2. Malazi yanapatikana (gharama kwa sasa sijui ila wakati naenda ilikuwa 30000Tsh kwa Mtanzania mmoja mmoja) (hii ni muhimu kufanya booking mapema)

3. Barabara za kufikia hifadhini (kutokea njia ya bagamaoyo) kwa kipindi kile haikuwa rafika kwa msimu wa mvua hivyo kama ni msimu wa mvua njia ya Mandera itafaa zaidi.

4. Kwa siku hizi hifadhi za TANAPA malipo hufanywa kupitia bank ya CRDB (yaweza kuwa kumekuwa na mabadiliko karibuni) hivyo ni vyema kama utakuwa na Card yao au uuluze utaratibu kabla hujaanza safari.

Safari njema mkuu
 
Back
Top Bottom