Naomba kufahamu kuhusu driving Course pale NIT

Kaveli

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
5,118
8,137
Wasalaam wanaJF...

Naomba kufahamu... hivi nikitaka kusomea Driving pale chuo cha NIT ili niweze kufikia ngazi ya 'Senior Advanced Driver' (nadhani ndiyo VIP/Executive level), itanichukua muda gani? na gharama kiasi gani kwa makadirio?

Na je wana-offer short courses on Motor Vehicle Mechanics?

Awali nilishasoma Basic Driving pale VETA na kupata Cheti & Leseni class A, D. Kwa hii Leseni class D... ni ngumu sana (almost impossible) kupata ajira kada ya udereva. Nimeona driver vacancy calls nyingi wanataka wenye Leseni kuanzia Class C and/or above. Pia nimegundua ukiwa na some basics in Motor Vehicle Mechanics... ni more advantageous kwenye ushindani wa ajira ya Driver.

Ndiyo nimefikiria nianze kujichanga ili niende pale NIT kusomea Senior/VIP/Executive Driving.

-Kaveli-
 
Nafkiri unatakiwa usomee Class E kwanza itumike mwaka mmoja then usomee PSV au Advanced Drivers Course Grade II (VIP Driving Course).

Ukisoma PSV utapata C1 ila ukisoma ADCG II utapata C123. Itumike mwaka mmoja halaf usomee C-Plain itumike mwaka mmoja then ndio usome hiyo course unayotaka kusoma.
 
Kumbe ni kasafari karefu kufikia level ya Senior/VIP Driving... si chini ya 3 YEARS! Thanks mkuu, umenipa mwanga.

Je vipi kuhusu Motor Vehicle Mechanics... huwa kuna short courses? just a basic level.

-Kaveli-
 
nasikia kwmb kozi za driving muda wake huwa sio zaidi ya week 8

Kama C-Plain ni siku 10 tu.

Duration fupi kabisa. Safi.

Wakati nasoma Basic Driving course pale VETA, tulitumia miezi miwili ... if my memory serves me well.
So nikadhani kwamba labda hizo course za juu zina duration ndefu zaidi.

Ahsanteni kwa taarifa.

-Kaveli-
 
Nafkiri unatakiwa usomee Class E kwanza itumike mwaka mmoja then usomee PSV au Advanced Drivers Course Grade II (VIP Driving Course).

Ukisoma PSV utapata C1 ila ukisoma ADCG II utapata C123. Itumike mwaka mmoja halaf usomee C-Plain itumike mwaka mmoja then ndio usome hiyo course unayotaka kusoma.
Kuna madereva wengne wana lesen had class E ila walizpta kwa njia shortcut:,hawakusomea wala kwenda course ya aina yoyote!!! Na lesen hyo ina miaka 2 na miez kadhaa..

Je, mtu huyu anaruhusiwa kwenda NIT na kuomba kusomea PSV ????
Na je,, class C plain anaruhusiwa kuisomea????
 
Kama leseni ipo kwenye system na inatambulika kisheria hamna tatizo coz kabla ya masomo au wakati mnasoma I hope leseni zinachukuliwa kwa ajili ya uhakiki therefore kama itaonekana kwenye system hamna tatizo unasoma PSV.

Na je,, class C plain anaruhusiwa kuisomea????

C Plain ni mpaka uwe na C123 ambapo hizo C123 unazipata baada ya kusoma Advanced Drivers Course Grade II (VIP Driving Course).

Ukishapata hizo unaruhusiwa kusoma C-Plain kiongozi.
 
Nimesoma nikapata leseni daraja LA b na d he naweza kwenda not kwa course ya tracks?

Ndio, ukiwa na B na D ambayo imetumika mwaka mmoja unaruhusiwa kusomea E ambayo inakurusu kuendesha magari makubwa mkuu.
 
Kumbe ni kasafari karefu kufikia level ya Senior/VIP Driving... si chini ya 3 YEARS! Thanks mkuu, umenipa mwanga.

Je vipi kuhusu Motor Vehicle Mechanics... huwa kuna short courses? just a basic level.

-Kaveli-

Yah, short courses zipo kiongozi.
 
Siku

Sikuwahi kusomea udereva , nataka niendeshe gari kubwa, mafunzo na sheria zake zikoje? Itanichukua muda gan?

Kwa kawaida ukitaka mafunzo ya kuendesha gari kubwa unatakiwa kuwa na leseni inayokuonesha kuwa umesoma mafunzo ya kuendesha magari madogo iliyotumika mwaka au walau miezi nane ndio watakupoke.

Na pia hujasema ni gari kubwa lori au basi la abiria. Kama ni lori unaweza ukafanya mpango wa kupata kwanza leseni ya B na D kwa njia ya uwani baada ya hapo unajiunga na kozi ya magari makubwa. Aidha, Kama ni gari kubwa za abiria huwezi kuruka ni lazma upitie hatua kadhaa kuweza kufika hapo.

Sheria ndio hizo na muda kwa gari kubwa ni siku 10 HGV kozi yake mara ya mwisho ilikuwa ni 515,000/10days.

Sjui ntakuwa nimekujibu.
 
Samahani ninaomba kuuliza utaratibu wa kujiunga chuo cha udereva unakuwaje?, coz kuna mtu alienda chuoni akaambiwa aende kulipia benk kabla hata ajapewa fomu ya kujiunga, na hata alipoomba fomu aliambiwa hawezi kupewa fomu kabla hajaenda kulipia benk hela ya mafunzo ya udereva, sasa sjui kuwa ndiyo inavyokuwa, ninaomba mnisaidie kunielewesha, na huwa ni shilingi kwa kozi ya miezi miwili.
 
kakujibu vizuri sana
 
Sorry kwa kuchelewa kujibu, ila utaratibu uliopo ni kuwa unapewa account number ya chuo then unaenda kulipia bank halaf unarudi chuoni.

Inategemea na course unayotaka kusoma coz kila course ina malipo tofauti na nyingine. Mimi kwa sasa sipo chuo ila ukifika pale uwaombe karatasi ya course zilizopo ambapo hiyo karatasi inakuwa na course pamoja na ada husika ya course na account number, pia wanakupa na karatasi ya vigezo kwa kila course utayotaka kusomea.

Thanks a lot.

Wlcm.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom