Unatumia mbinu gani kudai watu unaowada? Nafikiria kutokopesha watu ovyo ovyo ila roho inanisuta

Tamati

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,085
1,956
Nimekuwa muhanga wa kukopesha watu hela ila silipwi kwa wakati na wengine hawalipi na kuamua kukaa kimya, nachoka kuwadai kwani wanakaa kimya ninapowadai, wengine wanamua kubadili namba.

Mwaka 2016, nilikopesha mtu hela na akaahidi kunilipa baada ya muda fulani, alinilipa kidogo halafu nyingine akagoma na akabadili namba maana yupo mkoani, nikafanya juhudi za kumtafuta nikashindwa.

Mwaka 2017, mwishoni nikamkopesha mtu mwingine tena aliniahidi kunilipa baada ya muda fulani, alinilipa nusu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumdai kwa nguvu sana, sasa imebaki nusu namdai hataki kunijibu sms zangu, wala kupokea simu.

Nafikiria kutokopesha watu ovyo ovyo ila roho inanisuta, mbinu gani mnazotumia kudai watu wa namna hii? Tupeane uzoefu wa kukabiliana na jambo.
 
Next time aje na bond (kitu cha thamani kuweka). Kwa sasa kijinga funga moyo ukisubiri lipwa, yakikushinda jiwe kasema tuvute jani kisirisiri then tuvamie uwanja!..
Mshana Jr. anasema "samehe ukishindwa lipa kisasi".
Jasho la mtu haliendi bure!.
 
Dah...tafuta juisi ya ukwaju....au Kvant...gonga ya kutosha...Kisha mfuate mdeni wako....nakuhakikishia masaa 24 Ni mengi

Sent using Beretta ARX 160
Tatizo wapo mbali na mimi nilipo, niliwaamini sana ila ndio hivyo wamebadilika
 
Next time aje na bond (kitu cha thamani kuweka). Kwa sasa kijinga funga moyo ukisubiri lipwa, yakikushinda jiwe kasema tuvute jani kisirisiri then tuvamie uwanja!..
Mshana Jr. anasema "samehe ukishindwa lipa kisasi".
Jasho la mtu haliendi bure!.
Tatizo mtu ambaye alikuwa muaminifu ila anageuka hapo ndio panachanganya
 
Nimekuwa muhanga wa kukopesha watu hela ila silipwi kwa wakati na wengine hawalipi na kuamua kukaa kimya, nachoka kuwadai kwani wanakaa kimya ninapowadai, wengine wanamua kubadili namba.

Mwaka 2016, nilikopesha mtu hela na akaahidi kunilipa baada ya muda fulani, alinilipa kidogo halafu nyingine akagoma na akabadili namba maana yupo mkoani, nikafanya juhudi za kumtafuta nikashindwa.

Mwaka 2017, mwishoni nikamkopesha mtu mwingine tena aliniahidi kunilipa baada ya muda fulani, alinilipa nusu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumdai kwa nguvu sana, sasa imebaki nusu namdai hataki kunijibu sms zangu, wala kupokea simu.

Nafikiria kutokopesha watu ovyo ovyo ila roho inanisuta, mbinu gani mnazotumia kudai watu wa namna hii? Tupeane uzoefu wa kukabiliana na jambo.
Wewe kama Mimi,popote ninapoishi watu uniona ni MTU rahisi wa kuweza kuwapa msaada wa kipesa,na nimekuwa nasaidia sana,Tatizo wengine awarudishi mpaka mkumbushane,na Mimi kudai huwa sipendi.
Yaani kama Nina hela mfukoni,MTU akinililia shida,huwa inaniwia vigumu kusema sina.
Sasa nimeanza kuhisi baadhi ya jamaa zangu wa karibu wana take advantage,Nina mpango wa kuacha,maana kuna mmoja,nilimpa pesa,mwezi umepita ananipa story zisizo na kichwa wala miguu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa naenda njombe kuwaroga
Nimekuwa muhanga wa kukopesha watu hela ila silipwi kwa wakati na wengine hawalipi na kuamua kukaa kimya, nachoka kuwadai kwani wanakaa kimya ninapowadai, wengine wanamua kubadili namba.

Mwaka 2016, nilikopesha mtu hela na akaahidi kunilipa baada ya muda fulani, alinilipa kidogo halafu nyingine akagoma na akabadili namba maana yupo mkoani, nikafanya juhudi za kumtafuta nikashindwa.

Mwaka 2017, mwishoni nikamkopesha mtu mwingine tena aliniahidi kunilipa baada ya muda fulani, alinilipa nusu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kumdai kwa nguvu sana, sasa imebaki nusu namdai hataki kunijibu sms zangu, wala kupokea simu.

Nafikiria kutokopesha watu ovyo ovyo ila roho inanisuta, mbinu gani mnazotumia kudai watu wa namna hii? Tupeane uzoefu wa kukabiliana na jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wana jamvi.

Mwanzoni mwa huu mwaka niliamua kuanza biashara ndogo ndogo. Nauza nguo, pochi na urembo wa kike. Nashukuru mungu reception imekua nzuri japo mwanzo nilikua na kauoga kidogo. Now mambo yanaenda. Nina uzia Instagram na kwa watu ninaowafahamu na wafanyakazi wenzangu.

Changamoto ninayokutana nayo ni kudai pesa yangu. Mtu anachukua bidhaa na kuahidi pesa atalipa baada ya wiki mbili (2) huo muda utatimimia lakini pesa hatoi. Mimi ni mdai mzuri sana, nawasumbua hadi wanalipa. Wakilipa tu ni kama wamesusa hata WhatsApp wanani block hii inapelekea kupoteza wateja. Hili linaniuma sana.

Nipo kwenye nchi moja Chini ya Jangwa la Sahara, sarafu ya hii nchi haipo stable kabisa hivyo mtu anavyozidi kukaa na pesa yangu ndo inavyozidi kushuka thamani. Mathalani nimemkopesha kitu cha $7 kwa thamani ya sarafu ya nchi husika baada ya mwezi hiyo pesa inapungua thamani hivyo wakati wa kunilipa inakua $5. Hii kitu inani-frustrate sana!

Nisaidieni mawazo. Ni jinsi gani naweza kumdai mtu na anilipe bila kumkwaza?

Sent From Galaxy S9
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom