Naomba kufahamishwa kuhusu mashine za kubetia

Tuo Tuo

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
669
1,194
Habar jf
Biashara ya kubeti imekua ikishamili Siku adi Siku ...watu wamekua wakibeti kupitia online au katka mashine vilevile kwa mitandao kama voda,tigo na mingineyo

Swali langu kuhusu kubeti kwa mashine
Biashara hii ikoje?
Faida kwa mwenye machine?
Je malipo yake yakoje?
Mtaji n shi ngap?
Na nikihitaji napataje hizi mashine na vigezo n vipi?
Kwa mwenye uelewa tafadhari tusaidiane mawazo
 
Like serious jamani kwa mwenye kufahamu kiundani kuhusu biashara hiyo aje kutuelekeza kwani hata mimi kwa mtazamo wangu nilikua naona ni biashara nzuri ukizingatia kwa sasa kazi zimekua ngumu hvo kupelekea vijana wengi kuwa addicted na michezo ya bahati nasibu. Hivo naona kama mtu ukiwekeza huko kuna pesa. Mjini kuna zile betting center zinazokua na screen zenye fixtures, screen zenye game zingine kama farasi na mbwa. Naomba kwa mwenye kujua mtaji na namna ya uendeshaji wa center zile anipe mwongozo. Huku niliko hakuna center zile so nahisi zikiwekwa vijana watavutika sana. Kwa mwenye mawasiliano na makampuni yanayotoa hzo screen anaweza akanipa tafadhali.
 
ingia kwenye mitandao yaoo.utaona namba ya simu, piga utapata maelezo. asante, ila kamali ni haramu
 
Nilienda m betting na premium betting mashine zile ndogo wanazitoa bure unatakiwa uwe na baraua za wazamini wawili zikiwa na muhuri wa selikari za mitaa. na barua moja ya utambulisho wako kutoka serikali ya mtaa. hawa jamaa wanatoa commision kwa kila laki moja utakayokatisha ticket wanakupa elfu nane hao mbetting kwa premium nimesahau ni sh ngapi waliniambia lakini kwa laki haizidi elfu kumi. kizuri kuhusu hizi mashine unapopewa wanakuwekea laki moja kwaajili ya kuanza kuchezeshea.
Mkuu km upo location nzuri tuwasiliane zaidi tufanye hii kitu haiitaji mtaji wala nguvu nyingi.
 
Back
Top Bottom