Naomba kufahamishwa hili kuhusu Blackberry!

SirBonge

JF-Expert Member
Jul 18, 2010
378
435
Jamani mimi nimekuwa nikitumia simu za kichina kwa muda mrefu sasa nimeamua kujivua gamba na kununua Blackberry! sielewi vitu hivi kwenye Blackberry-BB torch, BB curve, BB style, BB bold, BBM, Android.nime'google lakini bado cjaelewa vizuri.Tafadhali naomba kufahamishwa nini maana ya hizi zote? ni aina tu za blackberry au vipi? na je ipi ni nzuri kuliko zote?(kwa kufanya kazi sio sura)
Natanguliza shukrani, naomba msinicheke kwani naamini kupitia jukwaa hili ntakuwa nimesaidika, Ahsanteni
 
BlackBerry ni simu zinazotengenezwa na kampuni ya RIM zote zinatumia Blackberry Operating System, Android ni operating System nyengine kabisa hakuna BlackBerry ambayo inatumia Android. BBM ni program ya kutumiana message kwa kutumia mtandao kwenye simu za blackberry, inafanya kazi kati ya simu za blackberry tu, hivyo sio nzuri. Hizo curve, bold etc ni model tofauti za simu za bb, zinatofautiana muundo, bei etc.Ushauri wangu ni uachane na blackberry, sio simu nzuri kwa ujumla hasa kwenye upatikanaji wa apps na user friendliness yake. Tafuta simu inayotumia Android ambayo itakufaa.
 
true fact usichukue bb tafuta android.. mi imenlazimu kumsusia mtu bb9300 kwa laki moja tu.. cmply b'ze naona inasifiwa bure tu and i wasnt enjoying da phone.. applications kibao zilikuwa zinakataa na kudownload long video clips inagoma
 
Blackberry is the smartest phone ever! Uwe tayari kupay bills tu! Otherwise tafta simu nyingine! BBM 4 EVER
 
kijana mpango mzima ni adroid phones..hizo brackberry hazikidhi mahitaji ya mtanzania..mi ilikuwa inaniudhi kila application ni ya kununua af game zake mbayaaaaa....pia kila mwezi unalipia wakati mwanawane na adroid yangu naweka 2500 ya zain hadi application ya jamiiforum nimedownload
 
wadau samahan kwa kuingilia thread hzo adroid ndio simu gani? Mfano mimi natumia nokia x2- 01 je, hyo ni adroid?
 
Hapana kaka adroid ni operating system kwenye baadhi ya simu kama samsung,lg na nyengine kama ilivyokuwa nokia wanatumia symbion na window mobile...
 
Simu zote za Android ambazo ni official na zinatambuliwa na Google Android Device Gallery
pia kuna zengine ambazo zinatumia Android ila hazitambuliwi na Google, zinakuwa hazina Google Apps kama Play Store (Market) na Maps.
 
Mkuu Activister wewe unayetumia IDEOS inatumia Android OS E
edition ya Froyo 2.0.
 
hata mimi nilikua mpenzi wa Blackberry yani huwezi niambia kitu lakini nilivyopata android duh li BB langu limekua li alarm clock langu ...apps za android ni msala plus rooting and customizing hutakaa uichoke kamwe ..People join the future get Android
 
Hapana kaka adroid ni operating system kwenye baadhi ya simu kama samsung,lg na nyengine kama ilivyokuwa nokia wanatumia symbion na window mobile...

samahan mkuu,me natumia samsung g3410 je naweza kuwa na hyo android?
 
nawashukuru sana wadau kwa kunielewesha,nitaachana na BB na kutafuta Adroid!! Mbarikiwe sana
 
Back
Top Bottom