Naomba kufahamishwa haya kuhusu Hati ya Mashtaka

Myhope

Senior Member
Jul 20, 2017
154
67
1. Hati ya Mashtaka inapoandaliwa na mamlaka isiyo halali kisheria hapo inakuaje?

2. Hati ya Mashtaka ambayo imerejea vipengele vya kisheria visivyo sahihi, hili nalo kisheria limekaaje?

Naomba kupewa msaada hapo.
 
1.Hati ya Mashtaka inapoandaliwa na mamlaka isiyo halali kisheria hapo inakuaje?

2.Hati ya Mashtaka ambayo imerejea vipengele vya kisheria visivyo sahihi, hili nalo kisheria limekaaje?
Naomba kupewa msaada hapo.
Ikiwa hati ya mashtaka haitakidhi vigezo itakuwa haifai, kwa lugha ya kigeni (defective charge) yaani hati yenye mapungufu. Mshtakiwa akiwasilisha/akiibua upungufu/mapungufu yaliyopo kwenye hati ya mashtaka na mahakama ikaridhia kuwa yanaukweli basi shtaka dhidi ya mtuhumiwa litafutwa.

Kumshtaki MTU kwa kifungu tofauti nimoja ya sababu za kuifanya hati ya mashtaka kuwa yenye makosa, pia hati ya mashtaka kuandaliwa na mamlaka isiyo halali.

Zitumie hizo kama point za kuweka pingamizi dhidi ya shtaka.
 
👉👉Naomba kujua tofauti ya hati ya mashitaka na nakala ya hukumu?

👉👉👉Ikiwa kesi imetolewa hukumu mahakamani na mlalamikiwa AKASHINDA kesi lkn mlalakaji AKACHELEWA KUKATA RUFAAA JE KiSHERIA hii imekaaje,je mlalakaji atatumia njia gani tena Ili akate rufaaa na nyaraka kama hati miliki ya madai yake Hana?
 
Naomba kujua tofauti ya hati ya mashitaka na nakala ya hukumu?

Ikiwa kesi imetolewa hukumu mahakamani na mlalamikiwa AKASHINDA kesi lkn mlalakaji AKACHELEWA KUKATA RUFAAA JE KiSHERIA hii imekaaje,je mlalakaji atatumia njia gani tena Ili akate rufaaa na nyaraka kama hati miliki ya madai yake Hana?
Hati ya mashtaka ni nyaraka inayobeba maandishi yenye makosa ambayo mtuhumiwa anatuhumiwa kuyatenda.

Nakala ya hukumu ni nakala inayoelezea na kutoa majibu juu ya makosa yaliyo andikwa kwenye hati ya mashtaka ambayo mtuhumiwa anatuhumiwa nayo au nyaraka ya madai.
 
1.Hati ya Mashtaka inapoandaliwa na mamlaka isiyo halali kisheria hapo inakuaje?

2.Hati ya Mashtaka ambayo imerejea vipengele vya kisheria visivyo sahihi, hili nalo kisheria limekaaje?
Naomba kupewa msaada hapo.
mamlaka gani isiyo halali inayoweza kuandaa hati ya mashtaka, kwa mfano.
 
Kwenye kesi ya kikazi, Afisa utumishi anasaini hati ya mashtaka badala ya mamlaka ya nidhamu.
Hati ya Mashitaka inaandaaliwa na DPP peke yake! Hata police hawana mamlaka hayo tena ya kuandaa Mashitaka kwa ajili ya kwenda Mahakamani, Police upelelezi wao wote unaishia kwa DPP! na DPP ndiyo ataamuwa Nani amuandalie hati ya Mashitaka kwa ajili ya kupelekwa Mahakamani!! Au Nani amauandalie barua ya kuachia Mashitaka bila ya kueleza sababu ya kufanya hivyo!!!
 
Back
Top Bottom