Naomba kufahamishwa gharama za kodi kuleta gari toka Zanzibar

Salamu Wakuu.

Gari ni sh million saba, aina ya gari ni toyota rumion Z736 JY. Itanigharimu Tsh. ngapi hadi kuiweka barabaran Dar. Pia, kwa hizo namba hapa Bara itasoma Namb C au D?

Karibuni kwa mawazo.
 
Kwa experience yangu utalipia Registration fee. Na pia itaingizwa kwenye system kuangalia kama ililipa kodi kamili, kama ilibaki kiasi fulan basi hyo ndo utalipa.!
 
Pia kw hizo namba hapa bara itasom Namb C au D?
kwenye usajiri huku bara, utapata namba mpya kabisa D...

Zaidi soma hii thread

Ukiagiza gari Zenji sasa hivi jiandae kupigwa tu hiyo gari kama ni milioni saba
Bandarini ushuru utapigwa milioni nne
That means unatakiwa uwe na 10M+
Sasa tabu hiyo si bora uchukue showroom za hapahapa Bongo tu.
Pia na hii link: Msaada wenu juu ya masuala haya kuingiza gari toka Zanzibar to dar es salaam

Ajiandae na gharama zifuatazo;
  • ATALIPIA KODI YOOOTE KULE KULE IKIJA BONGO ANASAJILI TU.
  • ATALIPIA KIBALI CHA KUSAFIRISHA GARI KUTOKA ZNZ KUJA BONGO.
  • ATALIPIA GHARAMA ZA KUSAFIRISHA GARI KAMA ITALETWA NA SEA LINK.
  • VILE VILE KUTAKUWA NA GHARAMA YA CLEARING AGENT BUT HII MTA NEGOTIATE,
 
Kama ni kusajili utapewa namba mpya itakayokuwepo Bara, kama nikulinganisha J inawezakuwa B Kwa bara, Kwa sababu namba mpya Znz Kwa muda huu L ili Hali Kwa Dar ni D.
Kuhusu ushuru nenda ZRB au TRA Znz upapewa maelekezo yote, hesabu itapigwa Kwa kuangalia muda ambao gari inetumika Zanzibar, kama inavibali vyoote wao wanaita kupasishwa, nk.
Kwa gari za namba L inehesabika kuwa mpya hivo itapigiwa Kodi ya bara, manake ni nini? Watachukuwa Kodi ulipaswa kulipa bara wanatoa Kodi uliolipa znz, Baki ndo Kodi unayopaswa kulipa. Usafiri kwenye meli kwa Toyota Rumion ni kama laki 3. Ila Kwa hiyo namba Kodi utayochajiwa ni ndogo Sana, sijui Kwa utaratibu wa sasa wa TBS kukagua ubora kama utapitishwa tena huko
 
Nlkua na copy ya Tra nltaka kutoa raum zanzbar asee huu muungano hauna maana kat yetu na znzbr kwanza wao wanaruhusiwa kulpa nusu ya kod na kuendelea kutumia chombo kwaio ukipgiwa hesabu unajkuta kwa umeilpia kama ml 5 kama gar umeinunua znzbr ml 7 weka ml 5 za bongo uku unakuta n kama umeagza japan nikiipata iyo pepa ntakuwea apa
 
Kama ni gari lako itz ok ila kama unanunua huko ulete huku bara big no coz hesabu utakayopigiwa ni bora ununue bara sbb usumbufu ni mkubwa sana
 
Fafanunua kuhusu hizo gharama,
Huwa wanalipa kodi 30% hiyo 70 utalipa wewe kama ukinunua so, kwenye hiyo milioni 7 unaweza ukajikuta unalipa milioni 4 hapo hujasafirisha bado plus usumbufu wa kwenda bandarini na TRA unakuta inakuja kwenye 12m ss hapo ni bora ununue bara au uongeze pesa kidogo uagize Japan
 
Back
Top Bottom