Naomba kueleweshwa ndugu zangú

baiser

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
1,456
2,181
Kuna ndugu yangu alikua na kesi inayodhaminíka na dhamana ilikua wazi ila kutokana na process ya kupata barua tulichelewa kama dk 10 hivi akawa kashapanda gari anaelekea segerea jee tunaweza endelea na taratibu za dhamana akatoka maana kesi itakuwa baada ya week mbili ndo wanaisikiliza tena.naomba msaada wa haraka kwa wanaojua hili
 
Muone karani wa Mahakama jambo dogo tu ila itakukosti gharama ya kumfata huko mahabusu
 
Muone mh Hakimu atakuandikia remove order utakayokwenda Kumtolea mahabusu huyo nduguyako
 
Muone mh Hakimu atakuandikia remove order utakayokwenda Kumtolea mahabusu huyo nduguyako
Ahsante bosi na je kuna malipo yeyote ya kuandika removal order kisheria kama nimekamilisha document zote za dhamana
 
Kiutaratibu hakuna gharama zozote utakazotakiwa kutoa ila watakuzungusha zungusha hadi utaona muda unakwendasana na nduguyako ndiyo hivyotena yupo mahabusu itabidi ujiongeze, lakini kama ni mbishi hata miamoja haitoki
 
Gharama ya kumfuta huko ni ya nn ?ya gari la polisi au naenda kumchukua tuu huko?
Utamfuata mahabusu kwa gharama zako kumpeleka mahakamani ili hakimu akamilishe taratibu za dhamama.
 
Hawawez niandikia memo nikipeleka kule wamtoe afu aje siku ya kesi kama dhamana ikikamilikaa?

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
Hapana haipo hivyo. Kama unaogopa gharama subiri siku ambayo ndugu yako atakapofikishwa mahakamani kwa gari la magereza ili umalizie taratibu za dhamana
 
Hawawez niandikia memo nikipeleka kule wamtoe afu aje siku ya kesi kama dhamana ikikamilikaa?

Sent from my GT-I9082 using JamiiForums mobile app
Kwamba utapewa askari polisi mahakamani, utafuatana naye kwa usafiri wako mpaka Gerezani, yeye polisi atamchukua mshtakiwa kwa amri ya mahakama mpaka mahakamani ili kukamilisha taratibu za dhamama. Nakumbuka iko hivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom