Naomba kazi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba kazi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Apr 16, 2011.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Lengo la kuomba kazi ktk chama tawala ni baada ya kuona kwamba, chama hiki kikongwe hakijui tatizo lake. CCM hawajui matatizo yao kwa kukosa watu wenye ufahamu au kwa kukosa watu wenye kusema ukweli. Hebu angalia maamuzi ya hivi karibuni na tutafute sababu zake;

  CCM walisema na wanasema walishinda kwa asilimia 60 na zaidi kidogo. Je, hilo ni tatizo kiasi cha kuanza kuvuruga vyombo vyao vya utawala? Au tuamini maneno ya CHADEMA, kwamba CCM hawakushinda kwa kura? Yaonekana wanajua kilichotokea na wanaanza kutafuta mbinu za kurudisha imani ili washinde kihalali.

  CCM wamejivua gamba au niseme ndo wameanza kujivua gamba maana hawajafika kwenye tatizo, ingawa pia sijui kama wanafahamu maana ya hayo maneno. Lakini;
  1. Je, tatizo wanalijua?
  2. Je, nini lengo la hayo ‘manjonjo’ wanayoyaonyesha na kujidai eti kujivua gamba?

  Majibu ya maswali hayo ni kwamba;
  1. Naamini CCM hawalijui tatizo lao, hivyo hawawezi kujivua.
  2. Ktk kujivua wana lengo baya, ovu na la kinafiki.

  Hapo ndo naanza kuomba kazi ili niwasaidie kutatua yanayowasibu, kama watapenda.

  CCM hawajui ni kwa nini wa-Tz wamewaacha. Naomba niwambie CCM kwamba wa-Tz wamewaacha kwa sababu siyo chama chao. CCM kimekuwa chama cha koo fulani-fulani. Milango ya kuingia ktk chama ilishafungwa kwa wasiyokuwa na majina ya koo hizo.

  Vijana kwa kufahamu hilo na kwa kupenda kuchangia ktk siasa za nchi yetu, wameamua kujiunga na vyama vyenye milango iliyo wazi, kuingia na kutoka! Bahati nzuri vyama kama hivyo ni vingi.

  Kwa kutojua tatizo lao, bado CCM wanaunda upya uongozi wao kwa kuingiza majina yaleyale ya koo hizo-hizo. Akina Makamba akina Nape, akina Mukama na wengine wanatakaokuja. Naamini hata akina Kikwete mdogo wako njiani kuingia. Wao wanasema wanajivua gamba.

  Lakini hebu angalia nyuma kidogo uone sababu ya kufanya hivyo.

  Mpaka mwisho wa kampeni za uchaguzi wa 2010, CCM walijinadi na kusema wako imara na hawana tatizo. Wakituambia wote tunaowakosoa ni kwa kukosa ufahamu. Wakaendesha uongo wakidhani ndo propaganda mpaka ndani ya JF wakazuka wachangiaji wa kila siku ambao leo hii hawaonekani. Ninachokiona ktk maamuzi yote wanayotuonyesha sasa hivi ni unafiki kwamba eti wamegundua makosa yao. Eti ghafla wamechukia ufisadi. Miezi 6 iliyopita hata Kikwete alionywa juu ya tabia ya kuwatetea mafisadi ktk majukwaa ya kampeni lakini masikio yalikuwa yameziba. Iweje leo hii masikio yake yazibuke wakati kelele zimekwisha pita?

  CCM bado hawachukii mafisadi. Wanajidai kuchukia ufisadi ili tuwafurahie. Mbona hawafungui milango yao? Mbona wanarudisha watoto wao na babu zao ktk utawala?

  Kama CCM hawataki kutuajili ili chama kifufuke, basi hata CCM ya Mukama itakufa tu!
   
 2. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  huu ni ujumbe mzito sana, uliobeba ukweli wa hali halisi ya mambo yanavyokwenda nchi hii
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Sijui kama unajua unachokiandika au unataka kuwafariji wana CDM wenzako katika kijiwe chao, kama ni kuwafariji nadhani ni kazi nzuri ila jifunge mkanda maana utaendelea kuifanya mpaka unaingia kaburini. Nadhani kama unamawazo mengine mazuri ungeyaelekeza kwa Slaa maana yeye utendaji kazi wake ndio unatumia miongozo ya JF.
   
 4. N

  Najaribu Member

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Kuhusu kushinda kwa CCM, mambo yote yaliwekwa hadharini na ripoti ya Timu ya Nchi za Ulaya. Inapatikana kwenye mtandao. Waangalizi hawa wanasema wazi kuwa kura za urais ziligubikwa na sintofahamu pale Tume ilipohesabu peke yake bila kuruhusu wakala au waangalizi wo wote kushuhudia idadi hiyo.

  CCM inajua fika haikushinda kiti cha urais na ndiyo sababu mzimu huo bado unawaandama sana. Inabidi tu wafuate kila kile kitakachosemwa na CHADEMA kwa sababu wanajua hawana dira yo yote zaidi ya ahadi zao mamia kadhaa waliyotoa.

  Tushirikiane na wapenda maendeleo kujinasua katika utumwa wa kuendelea kukumbatia chama ambacho dira na maono yake ni ushindi katika uchaguzi, na si maendeleo ya wananchi
   
 5. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  pole mkuu mjepu
   
 6. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mjepu i fail to define and comprehend you ...................are you the ex-husband of Josephine?.........hebu tujuze ili tuanze kukuelewa.....................nakufananisha sana na "system at dirty-work"
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Hapo ndo kuna tatizo! Tangu mulipozaliwa.

  Mulishindwa sababu ilikuwa wapinzani wa Ujamaa. Ujamaa umekufa sasa kila kushindwa kwenu ni CDM! Hata vurugu za mjadala wa katiba ilikuwa CDM. Ilipofika Zenj mukakosa la kusema!

  Ninyi CCM, Hata adui huokoa! Kama hamtaki, vueni hata ngozi lakini rangi ya kijani na ile nyundo na jembe tutaviona tu!
   
 8. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjepu nadhani una macho lakini huoni,una masikio lakini husikii,endelea kutetea ujinga kwa maslahi ya mafisadi.
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kazi ushakosa.
   
 10. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mtanzani mwenye fikra huru, nimegundua kuwa Slaa ni hatari zaidi kwa ustawi na amani ya taifa hili kwa tamaa zake za madaraka, mimi si mume wa josephine kwa bahati mbaya sinaga ukaribu na wanawake wa jinsi yake.

  Sina habari kama CCM ilishindwa uchaguzi, nachofahamu ni kuwa kulikuwa kuna udhaifu uliosababisha chama kukosa ushindi kiliopanga, nadhani sasa ni wakati kwa CDM nao kutuambia matarajio yao katika uchaguzi uliopita na kama kuna marekebisho maeneo yenye udhaifu kama ilivyofanya CCM, after all CDM pia ni chama chetu kinaendeshwa kwa kodi zenu tuna haki ya kujua utendaji wake wa kazi

  Hizi ndizo akili za kushikiwa, wewe aliyekuambia kuwa kuna pande ya Slaa na ufisadi ni nani? umekalilishwa kama sio nyeupe ni nyeusi na si vinginevyo. Tafuta ukweli dogo, taifa limetumia gharama sana kukusomesha.
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Mjepu,

  Kwa nini humpendi Dr. Slaa?
   
 12. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Vipi! hiyo join date yenu ni moja na msimamo wenu mmoja, ofisi yenu Lumumba nini?

  Hebu jiulizeni. Ni wapi ktk mijadala ya wazi, redioni, Tv na kumbi za mikutano utakapowakuta watetezi wenye hoja wakiisifu CCM? Au wote ni CDM? Najua hapa JF munajitutumua kwa kuwa hatuonani la sivyo mungenyang'anywa mic.

  Tusigombane. Hapa tunapeana maono yetu na siasa za TZ. Kwa kuwa mumeweka msimamo, naomba musiondoke JF kama hao wengine ambao sasa wamepotea. Dumuni ili siku si nyingi mutajionea jinsi CCM ilivyopwaya.

  Hakuna Kiongozi wa CCM ambaye ni mfano mzuri kwa mwananchi wa kawaida. Wote hawana lugha moja nasi kwa miaka hii.

  UVCCM ndo kabisa! Nimesema mara nyingi, wamejaa watu tunaowaita 'mishen town'. Watawezaje kutuvutia!
   
 13. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu umenena ni ukweli mtupu hapo
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Wale wale....huna maana hapa JF..............
   
Loading...