Naomba Business Idea

Siasa

Member
May 18, 2009
29
7
Wakuu, ninao mtaji wa sh.milioni kumi. Nataka nianze biashara hapa Sinza. Naomba ushauri wenu tafadhali. Nimetafakari nifanye biashara gani nimeshindwa kujua ipi itanilipa kwa kiasi hicho kidogo nilichonacho. Asanteni.
 
naona sas hivi hili tatizo ni kubwa .... wengi humu yaonyesha wana mitaji midogo na ya kati lakini wanamapungufu ya kukosa wazo zuri la biashara ... nini kifanyike wana jf-entrepreneurs

je? kuna uwezekano kwa walio na mitaji lakini hawana wazo la biashara wakaungana na walio na wazo la biashara lakini hawana mitaji?

changamoto hii ni kubwa
 
Kaka suala la ku-team up na mtu msiofahamiana bila arrangement nzuri za kisheria na kijamii, ni gumu kidogo ndio maana inakuwa ngumu kuwakutanisha hawa watu kwenye makundi mawili.
Lakini wazo lako ni zuri na linatekelezeka kama watu wengi wangekuwa na uelewa mzuri wa Capital market. Soko letu la Mitaji halitumiki ipasavyo kwa sasa zaidi ya kuuza HISA, na Government Bonds na sijaona jitihada za kuwaelimisha watu juu ya hilo, ingawa sheria zinaruhusu watu kukusanya mitaji (na wengine kuwekeza) kwa arrangement hizo
 
Wakuu, ninao mtaji wa sh.milioni kumi. Nataka nianze biashara hapa Sinza. Naomba ushauri wenu tafadhali. Nimetafakari nifanye biashara gani nimeshindwa kujua ipi itanilipa kwa kiasi hicho kidogo nilichonacho. Asanteni.
Ukipekua pekua post zilizotangulia utakutana na haya unayoyahitaji kwani yameshajadiliwa sana hapa. Kila la heri mkuu
 
Wakuu, ninao mtaji wa sh.milioni kumi. Nataka nianze biashara hapa Sinza. Naomba ushauri wenu tafadhali. Nimetafakari nifanye biashara gani nimeshindwa kujua ipi itanilipa kwa kiasi hicho kidogo nilichonacho. Asanteni.

mimi nakuomba kama suluhu uwe na urafiki na mkenya utapata maarifa mengi sana ya biashara na utanawili
 
fanya biashara ambayo unaweza kuimeneji usikurupuke ukishapata idea fanya research ya hyo idea
 
Mkuu the best Business Aidea inatoka kwako wewe mwenyewe,na inashangaza kwamba unaishi hapa hapa duniani lakini huwezi kupata wazo labiashara, MKUU
1, UNAKULA
2,unakunywa
3,Unalala
4. Unatembea
5. Unaona/unatazama
6.Unasikia
7. Unasoma
Kama unafanya hivyo vyote huwezi kosa wazo la biashara hata siku mojamkuu na wazo bora linatoka kichwani mwako na kama huwezi kutafuta wazo zuri labiashara hutaweza kuendesha biashara yeyote ile
S0

1. soma magazeti yenye makala za biashara/uchumi

2. Tazama television hasa vipindi vya uchumi na biashara
3. soma vitabu vya biashara na machapisho ya biashara

4. Tembea/safiri from one place to another

5. Blog au website mbalimbali unaweza kuja na wazo la biashara. websitekama ya AFRCAN REPORT, ENABLIS NA WEBSITE ZINGINE ZA BUSINESS PLANINGCOMPETITION ZIKO KIBAO SEARCH.

UKIFANYA HAYO HUWEZI KOSA WAZO LA BIASHARA HATA SIKU MOJA

moaja ya kitu cha muhimu katk kumshauri mtu wazo la biashara lazima kujua vitu vifuatavyo, na kama utapenda nizidi kkushauri naomba unijibu maswali yafuatayo. 1. unainterest na vitu gani? 2.umewahi kufanya biashara b4?(uaozefu katika biashara ipi?) 3.elimu yako? 4.uta manage we mwenyewe au kunamtu ambae utamwachia? 5.unataka uifanyie wp? 6. unataka uingize minimum ya sh ngp kwa ck? 7.uko tayari kupata risk ya kias(hasara) gan? 8.uko radhi kufanya biashara kwa mda gan? 9.huo mtaji ni mkopo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom