Naogopa Majibu Ya DNA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naogopa Majibu Ya DNA.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jazmine, Nov 29, 2011.

 1. Jazmine

  Jazmine Member

  #1
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umri wangu ni miaka ishirini na mmoja. Wazazi wangu hawakuwahi kuoana wala kuishi pamoja kwani nilipokuwa conceived (wazazi) wangu walikuwa bado kwenye late teens, wakati huo wanafunzi. Katika mazingira hayo, umri wangu wote nimelelewa na familia ya mama yangu kisiwani zanzibar katika maadili ya kiislamu.

  Kwa ung'ang'anizi wangu, Mwaka jana nimefanikiwa kumshawishi mama yangu mpaka akanikutanisha na baba yangu.
  Yeye Mkristo na maisha yake yote ni Tanzania Bara, sababu familia ya mama'ngu hawakutaka aibu ya familia wala mahusiano na mawasiliano yeyote na baba'ngu. Nililelewa nao na kusomeshwa mpaka umri huu, ingawa mama'ngu amekiri mbele ya baba'ngu kwamba kwa takriban miaka kumi na moja wamekuwa wanawasiliana (kwa siri) na baba'ngu iwapo palikuwapo na mapungufu ya pesa na ambazo mama alishindwa jazilia.

  Hivi sasa na mawasiliano ya mara na baba'ngu na kiukweli ananipenda sana, nami nampenda sana. Tatizo ni kwamba
  limepitishwa azimio la kwenda kupima DNA kutokana na shinikizo la ndugu wa baba, japo mwenyewe baba ananambia kiukweli naye hajiskii kufanya hilo.

  Woga wangu ni kwamba majibu yakiwa ni kinyume na ninavyoyatarajia, nami sitaki kumpoteza huyu baba ambaye kwa miaka mingi nimekuwa natamani nifahamiane nae, leo hii mwenyezi mungu katukutanisha halafu majibu yawe negative, kwamba sio baba yangu? Nisaidieni wanajamii forums, nijiandae vipi kulipokea hili. Natauficha wapi uso wangu majibu yakiwa kinyume na ninavyoyatarajia, kwa maana tayari tushazoeana sana na baba'ngu.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Majibu yakiwa kinyume na ulivyotarajia itabidi umuulize tena vizuri mama yako maana kosa litakuwa siyo lako au la huyo ambaye umeambiwa kuwa ni baba yako.
   
 3. Jazmine

  Jazmine Member

  #3
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Loh! Hapo pananitia uchungu zaidi kwani kwa miaka yote hii amekuwa ananionyesha kwa picha baba'ngu ni huyu, halafu baada ya majibu negative, nianze kumhoji tena aniambie ukweli?
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mrembo pole sana,ila kubaliana na matokeo yoyote sababu huna kosa hata kama sie baba yako muombe tu umuheshimu kama mzee wako...
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Majibu yakiwa Neg naamini huyo baba hatakutupa.
  Wewe uta'bank on the fact that huyo mtu ni rafiki wa mama yako, na ni mtu ambaye so far wanaheshimiana, basi inatosha!
  Lakini kwanini usiangalie upande wa pili wa shilingi, yaani ikijulikana kuwa ni baba wa ukwel;i?
   
 6. Jazmine

  Jazmine Member

  #6
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana, nimekuwa natamani na mimi niwe na baba yangu. Nimevumilia mengi kuwaona wenzao na baba zao. Baada ya mwaka
  na kufaidi raha na mapenzi ya baba niambiwe kumbe si baba'ngu kwakweli tayari ishaanza kuniuma kabla hata hatujapima. Natamani nikatae kupima Jamani. Sijui nimekosea nini Mwenyezi Mungu mie.

  Kuna raha gani sasa ya kumuomba awe baba'ngu? mimi namtaka baba'ngu mzazi.
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Jazmine huu ushauri wa PakaJimmy ni mzuri naamini utakusaidia, sidhani kama mama yako atakuwa amekudanganya ukweli kuhusiana na baba yako well inawezekana ikatokea ingawa nisingependa ikatokea hivyo sababu i know italeta mtarafuku mkubwa between both families na mbaya zaidi kwa mama yako but piga moyo konde na muombe Mungu kila kitu kiende sawa sawia
   
 8. Jazmine

  Jazmine Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani yatokana na hisia za unwanted kid tangia mdogo, Kujiona baba'ngu kanitelekeza na yu wapi miaka yote hii.
  Naogopa kuumizwa tena na hayo majibu baada ya kuonana na baba na ndoto zangu kutimizwa.
   
 9. Jazmine

  Jazmine Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasali nikiomba madua kutwa kucha, sina raha nikiombea basi hata hicho kipimo kisifanyike,
  yaani wajiridhishe tu kwamba mimi ni damu yao, lakini yaonyesha hata baba'ngu
  anakosa raha sasa. Ni shinikizo la nguguze.

  Yarabi stara.
   
 10. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Cheki maisha ya mama yako kama alikuwa kicheche usikubali.
   
 11. Jazmine

  Jazmine Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je, weye waweza mchungua mzazi wako juu ya hili?
  Ili iweje yarabi, au mkuki kwa nguruwe?
  Busara kaka.
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  uamuzi wa kupima ni kati yako wewe na baba yako ndugu unawahusu nini? mbona sie wabongo tunpenda kushadadia maisha ya ndugu zetu?

  huna haja ya kuhofu, wanasema amjuae baba wa mwana ni mama, mradi mama alikwambia huyo ndo baba yako ondoa hofu nenda mkapime .......

  vilevile kama na yeye anakupenda, anakuthamini na kukujali haijalishi majibu yatakua negative au positive ataendelea kukupenda na kukujali....
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kama baba na mama wanakubaliana kuwa wewe ni 'mtoto wao' suala la kipimo cha DNA lina umuhimu gani? Hao ndugu wanashinikiza kupima ili iweje?
   
 14. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muulize kwanza mama ukweli maana wanasema mama asin giziwi mtoto
   
 15. Jazmine

  Jazmine Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nashangaa, naomba dua tusifikie huko lakini mimi ni mtoto sina kauli ya kulisimamisha zoezi hilo.
  Inaniuma sana. Natamani mjiweke kwenye nafsi yangu, mwenzenu najiona nisiye na thamani kiasi kwamba ati DNA tu ndiyo itayonikubalisha kwamba mie ni damu yao upande wa ubabani.

   
 16. s

  sawabho JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Jasmine, kupima DNA ndio kitu pekee kitakachokuondolea wasi wasi na kukuwezesha kujiamini kuwa huyo kweli ni Baba yako na sio mbuzi kwenye gunia. Kama ndugu wa Baba'ko wanang'ang'ania kupima DNA na wewe na unakataa, itawapa nafasi ya kuendelea kukutenga na kutokukudhamini kwa sababu watadhani kuna namna hapo na wewe ni king'ang'anizi tu, na hata ikitokea kwa bahati mbaya Baba'ko hayupo duniani itakuwia vigumu kukubalika miongoni mwa warithi wake kijamii, ingawa kisheria inawezekana. kwa maana hiyo ni vizuri ukafahamu ukweli. Kwa ushauri wangu, piga moyo konde pima hiyo kitu halafu utaishi kifua mbele ukijua kuwa huyo ndiye Dad wako. Tatizo ninalo liona kwa ni kwamba umeomba ushauri, lakini hauko tayari kupokea huo ushauri.
   
 17. Jazmine

  Jazmine Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama keshanambia huyu ndiye baba'ngu, na baba keshanipokea kwa mikono miwili na mapenzi yote.
  Shida ni ndugu wa baba ambao wao hawajajiridhisha mpaka pafanywe kipimo cha DNA.
  Majibu yakija vizuri alhamdulillah. Uchungu wangu majibu yakirudi kinyume na matarajio yangu jamani.
  Ndio maana natamani hii ndoto (furaha na mapenzi baina yetu) iendelee hivi hivi bila kufikia huko kwenye DNA.
   
 18. Jazmine

  Jazmine Member

  #18
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana, niwie radhi unisomapo vibaya. Uchungu umenitawala ndo maana waona kama sitaki kupokea ushauri. Sawabho. Ninaloliongelea hapa ni post traumatic stress baada ya majibu ya DNA. Tayari najiona mdhaifu kuyapokea majibu yatayokuwa tofauti na ninavyoyategemea.

   
 19. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  kwani...kwanza ilianzaje anzaje mpaka likaibuka hili swala la kupima DNA....kuna tatizo gani lililokuepo maana mpaka uamuzi wa kupima DNA uje si kwamba umeletwa tu ki mchezo mchezo....kulikuwa na tatizo gani!!?
   
 20. Jazmine

  Jazmine Member

  #20
  Nov 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kipimo cha DNA ni uthibitisho kwa wana ndugu kwamba mimi ni damu yao.

  Muda wangu umeniishia hapa, ila najifikiria iwapo ungekuwa wewe kwenye umri huo unaambiwa lazima ufanye DNA
  testing kuthibitisha uhalali wako kwa baba yako, kisha majibu yawe kinyume na unavyoyatarajia.
  Nitakuja wasoma kesho, Inshaallah.
   
Loading...