Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,592
- 81,575
Nimeishia hapo uliposema hamjawahi kufua, kufanya usafi n.kNatumai wazima wote,.
Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae( Mungu anisaidie niondokane na hii hofuππ₯Ήπ), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi..
Huyu mwanamke sielewi hua anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale., Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri ( anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja)..
Haitaishia hapo, Bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time⦠, Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani,. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa ( Napo ni mara chache sana ).. Sijui hua anapumzika mda gani
Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki , kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka,,..
Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati.. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinungβunika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja,..
Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni., Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishiπππ ( Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)
Hakuna mtu anafanya kila kitu mwenyewe mkuu, lazima wewe ukiwa mama utagawa kazi kwa wote wanaoishi ndani kwako. Lazima uwe na skills za management ya nyumba yako, kulea sio mzigo kihivyo.Sisi sio wavivu mkuu, kwasababu hata akisafiri hua tunafanya kila kitu wenyewe na nyumba inakua vizuri sana.. Tatizo ni kwamba hataki kusaidiwa na ameshamark kwamba kila kitu anatakiwa afanye mwenyewe..
Hicho ndo kinaniwazisha nitakapokuja kuwa mama itabidi niwe nafanya kila kitu mwenyewe
Ni vile kazi yangu inanikeep busy sana, lakini ninapopata nafasi mama hua hapendi kusaidiwaNimeishia hapo uliposema hamjawahi kufua, kufanya usafi n.k
Inaonekana nyie ni wazembe watu wazima msiojiongeza. Mpaka mtu unafikia kuwa una ajira maana yake umeshajitambua labda kwa hao wanaosoma.
Kwaupande wangu sijafurahia wewe kuona ufahari kuwa mpaka sasa mama anakufanyia kila kazi. Sijapenda kabisa. Nakushauri uanze kujiongeza rafki yangu angalau mama nae apate ahueni.
Hongera kwa kuwa na mama bora.
Yeah labda pia hivi,ila kuangalia watoto ni kazi sana kwa dunia hii ya sasa.Huenda waakati ukifika nitaona kawaida
Kuingia leba sijawahi kuwazia hata, najua nitaweza ila haya mengine jamani uwiiiπ©Hakuna mtu anafanya kila kitu mwenyewe mkuu, lazima wewe ukiwa mama utagawa kazi kwa wote wanaoishi ndani kwako. Lazima uwe na skills za management ya nyumba yako, kulea sio mzigo kihivyo.
Nilidhani hofu ni kuingia leba, kumbe ni management ya nyumba.
πππUmenifuraisha sanaDuh sema kwa jinsi vijana tulivyo manyang'au , nakawazia kabinti kangu kadogo kakikua itakuaje kipindi hichoπ€
Maajabu ya musa, hujui unachowish mrembo. Mama zetu wa zamani walijua jinsi ya ku treat waume zao na hata siku moja hawalalamiki lakini wadada wa siku hizi pruuuuu mrudi unyago mkasome upya.Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu
Amina kubwa.Mungu atafanya wepesi naamini
Kuingia leba labda Mungu asiwe amekupa uchungu wa EvaπππππKuingia leba sijawahi kuwazia hata, najua nitaweza ila haya mengine jamani uwiiiπ©
Kwa umri kama wa kwako hiyo hofu ni jambo la kawaida.Bado niko early 20s
Bado yuko in her middle 40s, ni vile tu kazi yangu inanikeeep busy sana, Lakini hata nikipata nafasi ya kushinda nyumbani hiwa hapendi nimsaidie ananiambia nipumzikeDuh! Balaa.. mnamchosha mama unless awe under 50.
Kama hufanyi kitu utakuwa unajua kazi zinavyofanyika?
Huenda ni kweli unayoyasema aiseeπ€π€π€Huyu mama house chore ndo refuge yake.
Nikwambie hatari iliyopo mbele,
Mkiolewa na kuoa mkamalizika hapo nyumbani,
GHAFLA anawaambia anahama nyumbani!
Hamtamuelewa , ila anaweza awajibu MMEKUA SASA!
nILIKUWA NASUBIRI KWA HAMU SIKU YA MDOGO WENU WA MWISHO KUONDOKA HUMU NDANI!
Mim nilikua kama ww.Umeanza kunitisha sasaπ₯Ίππππ
Hapana usiseme hapendi kusaidiwa. Wewe jiongeze na usimuombe kumsaidia. Mfano unawahi kuamka kabla yake anaamka anakuta umrfanya usafi angalau labda.Ni vile kazi yangu inanikeep busy sana, lakini ninapopata nafasi mama hua hapendi kusaidiwa