Naogopa Kumuoa

Naogopa Kumuoa

Tatizo gani kwanza... maana vipimo vya kitanzania tunavijua...
 
::
Ni rahisi kupoteza bahati si rahisi kuurudia wakati kuipata bahati.
::
Endelea mbele,inawezekana Mungu amewaita muwe mfano wa ndoa nyingi ambazo kilio cha watoto ni wimbo wa Taifa.
::
Najua si rahisi lakini kimbia tatizo upate tatizo zaidi.
Je ungekuwa wewe mwenye tatizo ungejisikiaje?
=
 
Hujapenda bado!
Af nimekuona namna gani na sentensi yako mwisho.!aaaaaaaaaargh acheni hizo bana kama kipato na elimu yako ndo vitu PEKEE vinavyokutafsiri wewe basi chukua vyeti ufunge navyo ndoa i see.
 
Kuna dada mmoja aliolewa alafu akaachwa, kisa alikuwa hazai. Miaka 6 kupika ghafla akashika mimba, sasa anawatoto 5. Na aliambiwa na dokta hawezi kuzaa.

Kuna policeman mmoja alimuacha mpenzi wake wa miaka 8 sababu hazai, basi walipoachana tu yule dada akapata mpenzi mwingine na mimba hapo hapo ikaingia. Watu wakasema police mungu kamlani, kumbe mwenye ndio alikuwa hawezi kutia mimba. Ingawa docta alisema mwenye tatizo ni mke.

Muoe alafu subiri miAka 5-6, pengine atazaa baadae.
Na kama hakuweza kuzaa basi yeye mwenyewe atakuonelea huruma na atakushauri ukazae nje au ukaoe mwingine, lakini husimuache kwa sababu hiyo.
 
Ndoa ni zaidi ya kupata watoto mkuu.

Kama huyo umridhika ndiyo wife material muoe,ila kama unatafuta wa kukuzalia watoto tafuta ambae unauhakika atazaa.

Nina ndg yangu mke wake alikaa miaka 15 bila kupata mtoto yakasemwa mengi sana kuhusu huyo mama,Tz hospital zote

walidhibitisha hawezi kupata mtoto.Mungu akawajaajilia wakafika marekani ilikuwa ni maajabu iligundulika mama alikuwa na

tatizo dogo sana lakulimaliza in a minute.Amepata mtoto 2011 waliona 1996.

Watoto ni zawadi tu kutoka kwa Mungu unaweza Mkuu,mi ninakushauri uoe tu huyo huyo kama Madokta

wameshindwa,hakuna linaloshindikana kwa Mungu ukimwamini!..
 
Bado hujaeleza tatizo..........funguka upate ushauri
 
Thanks wakuu kwa ushauri na mmenipa moyo wa kusonga mbele.
Kuhusiana na tatizo nitaliweka JF doctor sababu naamini hapa nitapata ushauri wa kijamii na kule nitapata ushauri wa kitabibu.
Thanks.
 
Thanks wakuu kwa ushauri na mmenipa moyo wa kusonga mbele.
Kuhusiana na tatizo nitaliweka JF doctor sababu naamini hapa nitapata ushauri wa kijamii na kule nitapata ushauri wa kitabibu.
Thanks.

Y're not serious.
 
huwa naonea huruma sana watu wanaooa ili wapate watoto....
watoto wakikosekana ndo mwisho wa mapenzi
 
Me mwenyewe niliwahi kuambiwa inawezekana nisipate mtoto kutokana na kuambiwa nina tatizo la moyo.nilikaa na diagnosis ya uongo for about 7 years nikijua nina tatizo sugu la moyo na kuachwa na mchumba.kwendaa kwa doctor mwingine nikaambiwa tatizo sio kubwa la kufanya nisizae hapo nikazaa mtoto wa kwanza.hapa nilipo nina mimba ya mtoto wa pili na nimeenda kwa cardiologist mwingine amesema sina tatizo it was just a temporary desease
Nashukuru mume wangu wa yeye alinipenda na matatizo yangu yote kumbe mungu kajalia sina matatizo kiivyo
 
Hujapenda bado!
Af nimekuona namna gani na sentensi yako mwisho.!aaaaaaaaaargh acheni hizo bana kama kipato na elimu yako ndo vitu PEKEE vinavyokutafsiri wewe basi chukua vyeti ufunge navyo ndoa i see.
Hahahaha
 
huwa naonea huruma sana watu wanaooa ili wapate watoto....
watoto wakikosekana ndo mwisho wa mapenzi
Wea acha tu sijui kwanini huwa hawana huruma juu ya wenzao. Hivi huwa nami sielewi je kipi kinaanza kutaka watoto au upendo kat ya wawili hao. Manake nadhani watoto ni majaliwa.
 
Wea acha tu sijui kwanini huwa hawana huruma juu ya wenzao. Hivi huwa nami sielewi je kipi kinaanza kutaka watoto au upendo kat ya wawili hao. Manake nadhani watoto ni majaliwa.
kuna siku niliwahi ambiwa ndo ni kwa ajili ya kuzaa, kitu ambacho sikubaliani nacho mpaka muda huu
 
Kuna watu wanaambiwa hawatazaa na wanazaa. Watoto wanakuwa ni baraka ya Mungu tu. Oa na Mungu atawatunuku tu naamini.
 
Hivi Tanzania watu huwa hawafanyi "ADOPTION" au kutunga mimba kupitia "SURROGATE MOTHER"???
 
kuna siku niliwahi ambiwa ndo ni kwa ajili ya kuzaa, kitu ambacho sikubaliani nacho mpaka muda huu
[MENTION]FP[/MENTION] nakubaliana na wewe, hii dunia ina mambo mengi, wengine wanaoa ili wapate watoto, wengine wanakwambia wazi kuwa wanaoa ili wapate mtu wa kuwalelea watoto walioachwa na marehemu mke wake au mtalaka wake, wengine wanaoa ili wapate mtu wa kumpikia, kufua na kutunza nyumba. Wengine pengine wanaoa hata kuwa na mtu wa kupokea wageni wake, lol!
Sasa ndoa za namna hii, zinanoposhindwa kufikia lengo la labda kupata watoto au kulea watoto au kutunza nyumba nk mara nyingi huishia kuvunjika. Bahati mbaya kwa sisi wa miaka ile ambayo kigezo kilikuwa ni kumpenda mtu jinsi alivyo, tunaonekana tumepitwa na wakati!
 
Back
Top Bottom