Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
HorsePower, nakumbuka mpaka naulizwa kama nitamuoa mtu (nakuwa engaged) sikuwahi kuulizwa kama nina uwezo wa kuzaa ama la! let alone kupelekwa hosp kuchekiwa uwezo wa kuzaa. Namshukuru Mungu nina watoto lakini mpaka sasa nina uhakika kuwa hata nisingekuwa na watoto bado ningekuwa mke wake.FP nakubaliana na wewe, hii dunia ina mambo mengi, wengine wanaoa ili wapate watoto, wengine wanakwambia wazi kuwa wanaoa ili wapate mtu wa kuwalelea watoto walioachwa na marehemu mke wake au mtalaka wake, wengine wanaoa ili wapate mtu wa kumpikia, kufua na kutunza nyumba. Wengine pengine wanaoa hata kuwa na mtu wa kupokea wageni wake, lol!
Sasa ndoa za namna hii, zinanoposhindwa kufikia lengo la labda kupata watoto au kulea watoto au kutunza nyumba nk mara nyingi huishia kuvunjika. Bahati mbaya kwa sisi wa miaka ile ambayo kigezo kilikuwa ni kumpenda mtu jinsi alivyo, tunaonekana tumepitwa na wakati!
Kila siku huwa tunakumbushana kuwa watoto hawahusiki katika mapenzi yetu, ni matunda tu ambayo Mungu ametujalia. Nakumbuka kuna wakati tunapotaka kufanya vitu fulani kwa ajili yetu (unajua tena sisi wamama tunawazia sana watoto) huwa nakumbushwa sana kuwa hawa watoto siyo part ya mapenzi. Tulianza wenyewe na mwisho wa siku tutabaki wenyewe, watoto wasituingilie
Last edited by a moderator: