Nani Zaidi: Mwanakijiji Vs John Mashaka

Status
Not open for further replies.
John Mashaka na Shao wapewe nchi hii kwa sababu wanaandika na kuongea sana kimombo kwenye blog ya michuzi au kwa sababu ipi ingine mpya?

Watu wengi nadhani wanatishika na kimombo cha John Mashaka,lkn ukigeuza hoja zake hizo za kizungu na ukaleta kwa kiswahili utagundua kabisa kuwa uchambuzi wake wa uchumi wa tz ni sawa na wa mtoto wa darasa la saba au sana sana form 2!

- Mkuu with all due respect, angalau hao wanajiweka wazi mbele ya taifa na mawazo yao, kuliko wengine ambao kazi ni kuponda tu huku wakiwa hawana hoja hata za kimombo.

- No matter what the case, misimamo yao iko wazi kwamba wana nia njema na taifa letu, na wanazo hoja nzito za kukosoa serikali dhaifu tuliyonayo sasa, na huwezi sema eti Tanzania we are better off na viongozi kama Kusila na Guninita, just because wanasema hoja zao kwa kiswahili kuliko Mashaka na Shayo kwa sababu hoja zao ni za kiingereza, wakuu sometimes tulionee huruma sana hili taifa.

- Ninaamini kwamba Mwanakijiji, Mashaka na Shayo wakipewa nafasi za uongozi wa juu wa taifa hili, watatusaidia better than kina Kusila, Guninita, na kina Kingunge.

Ahsante.

William.
 
- Katiba inayofaa kwa taifa letu inaweza kutengenezwa hata kwa siku moja tu, kwa sababu matatizo yake hayahitaji kuwa professor kuyajua, la kwanza ni kupunguza madaraka ya rais tu na huenda hata huhitaji kwenda kwingine zaidi ya hapo tu kulisaidia hili taifa, la kurekebisha madaraka ya ajabu aliyonayo rais wetu hayahitaji karne kuyarekebisha, ni suala la siku moja unarudisha madaraka kwa wananchi kupitia bunge lao la jamhuri.

- Ujeuri wote wa mafisadi huko CCM, unaletwa na madaraka ya ajabu aliyonayo rais wa jamhuri, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Ahsante.

William.
Mkuu unajua unachokisema, katiba si kitu cha mchezo na si assignment za chuo kikuu na wala si maandishi ya articles kwenye JF hauwezi andika katiba siku moja....waambie hao akina Mwanakijiji waende kutangaza sera zao kwa wananchi na sio kwenye Blogs mkuu..maana naona mnataka kukimbia ukweli kwa kwa sasa hawana sifa wala uwezo wa kuongoza nchi mpaka tujue sera. sio unashangilia kila kitu, jua kuchuja...
 
Mkuu, nimependa mapendekezo yako, ila hapo kwenye kipengele "a" umezungumzia mabadiliko ya katiba kwa uhakika utadhani ukishaamua wewe basi wengine wote "Watasema zidumu fikra za Mwanakijiji" na kuafiki yote kama yalivyo..!!

Hapana; nimejenga kanuni ambazo kiongozi anatakiwa awe nazo; kwamba tutafanyia mabadiliko katiba na baadhi ya mambo ni hayo ndio mwanzo wa mjadala; at the end tutafika mahali baada ya michango ya watu mbalimbali na wadau mbalimbali tutapata kile ambacho kinaakisi kweli hamu, na matamanio yetu.

hatuwezi kuwa na uongozi usiojua unataka nini na kuweka miguu yake chini na kusema hiki ndicho tunakitaka.
 
Mkuu unajua unachokisema, katiba si kitu cha mchezo na si assignment za chuo kikuu na wala si maandishi ya articles kwenye JF hauwezi andika katiba siku moja....waambie hao akina Mwanakijiji waende kutangaza sera zao kwa wananchi na sio kwenye Blogs mkuu..maana naona mnataka kukimbia ukweli kwa kwa sasa hawana sifa wala uwezo wa kuongoza nchi mpaka tujue sera. sio unashangilia kila kitu, jua kuchuja...

yaani ukijua sera ndio umejua uwezo wa mtu kuongoza? Mbona CCM ina sera nzuri labda kuliko chama chochote kile? sera ni maneno yaliyopangwa vizuri ili kupata kura! Uwezo wa mtu kuongoza hausiani kwa namna yoyote ile na uwezo wa kuelezea sera; vinginevyo, mngempa Uwaziri Tambwe Hizza!
 
Malecela,
Unachekesha kweli..waliomfanya mwanakijiji semi- god ni nani..jisemee nafsi yako mimi namuona mlalamisha hana issue
Vinginevyo tunamsubiri kwenye field...Jukwaani na vijijini akimwaga sera..

- Unamuona Mwanakijiji ni mlalamishi na hana ishu, wakati kule chini ni wewe ndiye umeanzisha thread ya kumsifia kwamba anafanya kazi njema sana kwa taifa, ndio ninaita unafiki unaoturudisha nyuma taifa hili, you can't have it both ways mkuu! na tunaoingia humu JF sio wajinga kama unavyofikiri na kujidanganya, kuna wengi unawadanganya ila sio mimi. Halafu hili neno unachekesha hivi huwezi kutafuta lingine maana huwa huwezi ku-help yourself na hili neno na ndipo huwa unaharibu na hizo childish games zako, it is about time sasa uka grow up japo kidogo mkuu!

Ahsante.

William.
 
Mkuu unajua unachokisema, katiba si kitu cha mchezo na si assignment za chuo kikuu na wala si maandishi ya articles kwenye JF hauwezi andika katiba siku moja....waambie hao akina Mwanakijiji waende kutangaza sera zao kwa wananchi na sio kwenye Blogs mkuu..maana naona mnataka kukimbia ukweli kwa kwa sasa hawana sifa wala uwezo wa kuongoza nchi mpaka tujue sera. sio unashangilia kila kitu, jua kuchuja...

- Anayerukia ishus bila kuchuja ni wewe usiye na new ideas wala positive thinking, licha ya ushauri unaofaa kwa taifa lako zaidi tu ya kuponda watu wenye sifa na uwezo wa kufikiri kuliko wako, viongozi huweka njia tena mahali popote walipo regardless wako wapi iwe kwenye blog, iwe jela kama kina Mandela, iwe barabarani wanaendesha trucks kama kina Walecha kule Poland, au kwenye dini kama kina Pengo.

- Kwa maandishi yao tu mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kuona mbali, unaweza kuwaelewa kina Mwanakijiji, Mashaka na shayo kwamba wanaweza kulisaidia taifa letu, unazungumzia time as a factor katika kutengeneza katiba, kwamba ni lazima iwe ni muda mrefu ndio itakuwa a sound katiba na unatetea kwa nguvu zote kwamba you are right na hii nonsense thinking, kwamba ukiwaweka pamoja Tambwe, Guninita, Mzindakaya, Kusila, Rostam kwa muda mrefu sana basi watatengenza katiba saafi sana kwa taifa, no wonder hili taifa limekwama sana na this kind of thinking!

mu ndo mana nasema waende kuweka sera zao kwa watanzania mil 25/40 ambao ni wapiga kura..nachoweza kusema ni kwamba wanauwezo wa kuchambua mambo ila uongozi sijajua kwani watupe CV zao tujue...me leo nampendekeza mtu kama Migiro na Dr Salim Ahmed Salim je hao watu unaowataka wanaweza kusimama na akina Salim....Katiba haijengwi siku mmoja hapo tu tayari Mwanakijiji kaonyeshha udhaifu wa kukurupuka..katiba inakitu kinaitwa national forum ambao kila mwananchi anatakiwa atoe mawazo yake..bado pia kufwatilia international experience za katiba za nchi nyingine, pia inabidi wafwatilie requirements za variuos international conventions ili ziwe incorporated kwenye katiba...ni shughuli mzee na si lelemama

haya bwana nyie ndo mnao ingia mkenge ...tena nahisi hata haupo TZ hujui kinachoendelea unasoma tu kwenye ma JF na blogs mbalimbali ndo mana mwisho wasiku Chaaaaliiiiii
kaaazi kwelikweli teh teh teh teh
 
Ni mengi tu ambayo yanawezekana. Baadhi ya mambo ya kufanya baada ya mafanikio ya project-X:2010 ni haya:

a. Kuanzisha mchakato wa uandishi wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano na kuikamilisha ndani ya miaka miwili. Katiba hiyo:

- Itagawa madaraka kati ya Utendaji kati ya Rais na Waziri Mkuu
- Waziri Mkuu ataunda Baraza la Mawaziri litakalokubaliwa na Rais
- Tutatatua kero za Muungano kwa kurudi kwenye makubaliano ya Muungano ya 1964 (Articles of the Union) na kufanya mazungumzo mapya ya kuhakikisha serikali ya Tanganyika nayo inarudi (Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaongozwa na Mawaziri Viongozi na serikali zao- Tanzania itakuwa na Rais Mmoja tu!)
- Tutapunguza wingi wa Wabunge na kuligawa Bunge sehemu mbili zinazosimamiana na hivyo kuwa na bicameral parliament (Seneti na Baraza la Wawakilishi)
- Tutaweka mipaka ya matumizi ya kinga ya Rais ili iwe rahisi kuivua kinga hiyo katika mazingira fulani fulani.
- Mawaziri hawatalazimishwa kutoka miongoni mwa wabunge.

b. Tutasitisha mikataba yote mikubwa ya madini na kuipitia upya na kukubaliana na wawekezaji upya. Mwekezaji ambaye hataki kukaa chini upya tutamsaidia kufunga virago vyake bila ya kumuomba msamaha! Tutaanza na Barricks na wenzake!

Tutahakikisha mikataba yote inayohusisha raslimali za taifa letu (madini, ardhi, mbuga n.k) inatajirisha kwanza kabisa (siyo pili au tatu) wana na mabinti wa taifa hili. Mwekezaji yoyote ambaye atataka yeye atajirike kwanza tutamtimua siku ya pili ya kutoa kauli hiyo! Hatuna kubembeleza mtu yeyote yule.

And you ask: "sasa wawekezaji wakikimbia si ndio nchi itakwama"? Hayo ni mawazo ya Kikwete ambayo hayamo katika fikra zangu!

c. Tutarudisha baadhi ya mashirika mikononi mwa serikali katika mtindo wa private-public management. Miongoni mwao ni pamoja na NBC, Simu, Umeme, n.k Details nyingine hapa ninaziweka kapuni.

d. Tutaiokoa TRL na kuirudisha kuwa TRC na kuhakikisha ndani ya mwaka mmoja shirika hili linajiendesha lenyewe likiwa na menejimenti ya Watanzania na likiwa ni shirika lenye huduma na uwezo wa hali ya juu kabisa ya kusafirisha abiria na mizigo. Blueprint ya mpango huu tayari imeshakimilika.

Hayo ni machache tu; mengine subiri the "Real Deal: Contract with Tanzanians" kama sehemu ya P-X:2010.

Change is coming.. be part of it au kaa pembeni!

Nakupata mkuu, tuko pamoja. Tatizo la watanzania tumezoea kuwa wafuasi na sio waendaji. Wengi wanapenda kufuata yaleyale yaliyofanyika jana yake.

hii nchi inahitaji fikra mpya. Wanaoulizia uzoefu wanataka uzoefu gani? Wa kuiba!!! au wa kugawa rasilimali za watanzania kwa wageni bure il mradi wamepewa 10%

Mmesahau kuwa Mwl Nyerere alikabidhiwa nchi akiwa na miaka chini ya 40, je alikua na uzoefu gani.

Kinachotakiwa ni uzalendo, elimu ya kutosha kuanalyse and make decision na ujasiri.
 
,,uongozi wa nchi ni mzigo mkubwa,unahitaji uzalendo,kujitolea kwa kiasi kikubwa,,haya ni maneno ya mwl.nyerere........sio kila anaye weza kubwabwaja anaweza kupewa nchi..................
Ndugu Wadau, Nadhani muda unavyokwenda, nchi yetu inazidi kudidimia katika wimbi la ufukara. Nchi imekwisha na hali inazidi kutisha, hasa tukizingatia hali ya kisiasa na ya kiuchumi.
 
huu undumila kuwili mpaka lini????????????
- Unamuona Mwanakijiji ni mlalamishi na hana ishu, wakati kule chini ni wewe ndiye umeanzisha thread ya kumsifia kwamba anafanya kazi njema sana kwa taifa, ndio ninaita unafiki unaoturudisha nyuma taifa hili, you can't have it both ways mkuu! na tunaoingia humu JF sio wajinga kama unavyofikiri na kujidanganya, kuna wengi unawadanganya ila sio mimi. Halafu hili neno unachekesha hivi huwezi kutafuta lingine maana huwa huwezi ku-help yourself na hili neno na ndipo huwa unaharibu na hizo childish games zako, it is about time sasa uka grow up japo kidogo mkuu!

Ahsante.

William.
 
John Mashaka na Shao wapewe nchi hii kwa sababu wanaandika na kuongea sana kimombo kwenye blog ya michuzi au kwa sababu ipi ingine mpya?

Pamoja na kwamba sija-endorse wapewe uraisi ila hoja zao zinaonyesha kuwa wana fikra za kulitakia taifa hili mema kuliko viongozi wanaodaiwa kuwa na uzoefu.

Ni nani asiyejua kuwa tz maskini kwa sababu za madhara ya ukoloni mkongwe,au kwa sababu ya rushwa,au kwa sababu ya elimu duni ambapo bado tunatumia njia za kale kuendeleza resources zetu ,au kwa sababu ya utawala mbovu usizingatia maslahi ya walio wengi?
Ni kweli kabisa mkuu. Sasa unafikiri tutapataje viongozi wenye mtizamo tofauti bila kuangalia nje ya system iliyopo? Sio lazima awe MM lakini lazima tuanzie mahali na tuondoe mawazo kuwa kama mtu hajawahi kuwa kada wa CCM basi hawezi kuwa kiongozi.
 
mu ndo mana nasema waende kuweka sera zao kwa watanzania mil 25/40 ambao ni wapiga kura..nachoweza kusema ni kwamba wanauwezo wa kuchambua mambo ila uongozi sijajua kwani watupe CV zao tujue...me leo nampendekeza mtu kama Migiro na Dr Salim Ahmed Salim je hao watu unaowataka wanaweza kusimama na akina Salim....Katiba haijengwi siku mmoja hapo tu tayari Mwanakijiji kaonyeshha udhaifu wa kukurupuka..katiba inakitu kinaitwa national forum ambao kila mwananchi anatakiwa atoe mawazo yake..bado pia kufwatilia international experience za katiba za nchi nyingine, pia inabidi wafwatilie requirements za variuos international conventions ili ziwe incorporated kwenye katiba...ni shughuli mzee na si lelemama

haya bwana nyie ndo mnao ingia mkenge ...tena nahisi hata haupo TZ hujui kinachoendelea unasoma tu kwenye ma JF na blogs mbalimbali ndo mana mwisho wasiku Chaaaaliiiiii
kaaazi kwelikweli teh teh teh teh

Mkuu nawaheshimu sana Migiro na Salim. Pamoja na kwamba wamekuwa na mafanikio sana katika siasa, je unaweza kutupa jambo moja au mbili waliyofanyia nchi hii likaleta mabadiliko ya kuonekana katika maisha ya watanzania. Kama hakuna, CV zao nzuri zinatusaidia nini?
 
Mkuuniliweka majina hayo kwa mtego, na wewe hauja unasa ila tu umenisaidia kuforce my point home na point yangu ilikua hiviiiiiiii

Je John Mashaka, Mwanakijiji na Dr Shayo wamefanya nini kwa taifa mpaka wawe na vigezo ambavyo watu wanawapitisha kuwa wanafaa kuwa viongozi? au ni uwezo wao wa kuandika? kama ni uwezo wa kuandika wapo watu wengi tu? nilichokua nataka watu waelewe ni kwamba uongozi ni zaidi ya kujua kuchambua mambo..mfano prof lipumba hamna mtu anaemfikia katika wanaogombeaga u prez da kwa kuchambua mambo, ila i am not sure kama ni kiongozi mzuri...me naamini kiongozi mzuri ni yiule ambae anaweza kuwa na mipango mizuri kwenye afya, elim. azingira, technology, utawala bora na chamuhim zaidi kuwa na team thabiti itakayo waezesha kuingia madarakani na si tu kuingia madarakani bali pia kuongoza watu milioni 40...mfano tena vyama vyetu vya upinzani vinakosa team kamili yaani watu waliokamilika zaidi kukijenga na kujenga uwaminifu kwenye chama ambao wanafaa kuongoza nchi...tubahitaji mlolongo wa vitu vingi na si nakuwa na uwezo tu wakuandika na kuchambua mabo...ni sawa na usemi kuwa mchezaji soka bora atakua kocha bora, ambapo saa nyingine siyo

ahsanteeeee
 
Nakubaliana na wewe mkuu kuwa uongozi ni zaidi ya kuchambua mambo lakini vilevile kuna uwezakana wa mwenye uwezo wa kuchambua mambo akawa kiongozi mzuri. Vilevile nakubaliana na vigezo ulivyotoa vya kiongozi mzuri.

Ninachokataa ni huo mtizamo wa watu kuwa kiongozi mzuri anaweza kupatikana kwenye group la wanasiasa tuliowazoea tu na nje ya hapo hawana uzoefu. Uwezo wa mtu utaujuaje, kama sio kwa kuanzia na hoja zake ambazo zitakupa mwanga wa kujua fikra zake na kwenye utendaji wake wa kazi anayofanya kwa wakati huo, sio lazima iwe uongozi.

Badala ya kuwakandia John Mashaka, Mwanakijiji na Dr Shayo, tungewauliza kama wakipewa hiyo nafasi watafanya nini? Halafu tuwachallenge na hizo fikra zao.

Vinginevyo kama tunajiita great thinkers na hatujiamini kuwa anaweza kutoka kiongozi wa kaya humu JF basi ni kichekesho.
 
mimi nimeshadokeza kuwa timu yetu ikifanikiwa kuingia madarakani itafanya mabadiliko makubwa kwa taifa letu na ndani ya miaka 20 tu tunaweza kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati. Tuna maono ya kutosha na hadi sasa tuna watu wa kutosha wenye kushiriki maono hayo. Tunatambua wazi kuwa jukumu la kuongoza watu siyo sawa na kuchunga mbuzi au kondoo. Hivyo, kunahitajika hekima, busara, uthabiti, uthubutu, na uongozi wa kweli.

Tanzania hivi sasa haina tatizo la wasomi au watu wenye "CVs" wapo wengi na wengi wamejaa CCM na kwenye serikail yake. Kwa miaka zaidi ya 45 watu hawa ndio wameshika hatamu ya uongozi wa taifa letu na tumeaangalia wakilipeleka taifa letu katika uombaomba wa milele, utegemezi hadi wa kiakili na ambao leo hii kuanzia raia wao hadi mfagizi wanaangalia kamapuni ya kitapeli ya dowans kuwa ni mwokozi wa tatizo la nishati nchini!

Hawa siyo watu wa kujadiliana nao au kuwashawishi wafanye kitu tofauti kwani hawawezi kufanya tofauti na mazoea yao. Hawana maono ya mbali na hawana ujasiri wa kiuongozi. Ni watu ambao wamefilisika kimaono na mwelekeo wao ni ushahidi wa kudumaa kiakili. Bahati mbaya sana wanaowaongoza nao huzugika kirahisi wakipewa fulani, vikofia na wakikaribishwa mipalau na minuso ya hapa na pale.

Tanzania inahitaji viongozi radicals, wenye maono yanayowezekana na wenye uwezo wa kujenga ndani ya watu wao moyo wa kujiamini, kuweza na kujituma. Viongozi ambao maslahi yao ya kwanza siyo chama (kama ilivyo wa CCM) bali ni taifa. Viongozi ambao watafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kuwa Tanzania inajengwa tena.

Binafsi sijaomba wala sitarajii kugombea uongozi wowote ule. Lakini endapo historia itaniita kulitumikia taifa langu katika nafasi yoyote ile, nakuhakikishia kuwa Tanzania itaona fahari.

Na ukitaka kujua kama nimewahi kulifanyia nini taifa.. historia yangu iko wazi. Sijaanza kuandika kwenye mitandao... nimefanya mambo tangu nikiwa na miaka 14 ambayo watoto wengi leo hii na vijana wengine wangetamani kuwa na nafasi hizo. Kiu na matamanio yangu ya kutaka kuliinua taifa langu haitokani na kukaa mbele ya kompyuta! Inatokana na misingi ya malezi na uelewa wa wazi wa watu wetu na kiu yao ya maisha yenye afueni, manufaa na nafasi kwa kila mtu kufanikiwa.
 
solution nzuri kwa taifa navyo ona mimi ni kuunda chama kipya ambacho kitawakilisha watanzania wote...vyama vya upinzani tulivyo navyo vinamatatizo makubwa mfano kuwa ni mfano wa NGO na kuwakilisha baadhi ya group la watu...hapo ccm ndo inatofautiana na wengine..lakini ccm imesha shindwa kutuongoza na inamaovu mengi..chakufanya ni kipi?
vyama tulivyo navyo havina hadhi ya kuchukua nchi, tukisema tuvibadilisha=e na CCM watadai nao wabadilike..so mimi naona watu tujikusanye tutengeneze chama thabiti ambacho hakina dini wala kabila na kina adress matatizo yote ya mtanzania yakiwemo afya, elim, umaskini na ufisadi.
 
ina maana unataka kuunda chama ambacho watu hawatoruhusiwa kuwa na dini au makabila fulani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom