Nani zaidi Aljazeera, CNN, BBC, DW, Press TV, ABC

Nani zaidi Aljazeera, CNN, BBC, DW, Press TV, ABC

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,393
Mimi ni mpenzi wa kufuatilia habari za kimataifa kupitia vyombo hivyo,lakini nimegundua kuwa kituo cha aljazeera cha mashhatiki ya kati ni kiboko kwa vyombo vya habari vya kimataifa katika habari hasa za kipekee(exlussive) na za breaking news .

hata hivyo inaonesha kuwa waandishi wa aljazeera ni wataalamu zaidi katika habari za vita,majanga na mambo kama hayo mfano kama waandishi JAMESB BAYS,MOHAMED ADO,KAMAU HAIDA ,KAMAU SANTAMARIA na wengine wengi.

Kwa kweli aljazeera wako juu,au wenzangu mnasemaje
 
Wengi wa waandishi wa aljazeera walikuwa cnn na bbc km akina riz khan. well hata mie nimependa jinsi aljazeera wanavyoripoti habari zao, mambo mengi ambayo tv za magharibi hawapendi habarisha kuhusu wao, aljazeera hutoa hewani.
 
Aljazeera ndio kuna uhuru wa habari bila kujali maslahi ya wakubwa
 
hata mimi naikubali Aljazeera kwa breaking news na uhalisia wa habari ingawa ni kweli reporters wake wengi walikua CNN na BBC. Mmenikubusha Rage Omar wa WITNESS. lakini hawa jamaa wa PRESS TV ya Irani wanakuja juu!!!
 
Al jazeera, Press TV ni PRO ARABS, PRO MUSLIMS AND ISLAM, ANTI WEST, ANTI ISRAEL!
 
Press TV ukiangalia habari zao kubwa ni Kupinga Israel kwa sana. Mara Israel kapiga Gaza, kauwa watoto, kabomoa nyumba lkn zile rockets wanazorusha Fatah na Hizbollah hawa ripoti.
 
napenda aljazeera but sometimes
wana kiuka misingi ya maadili ili tu kuwafurahisha waarabu.....
mfano mauaji ya gaza aljazeera walionyesha mauaji live
bila kujali athari anazopata mtazamaji ili tu watu waone unyama wa israel......
 
Al Jazeera of course! Walianza kwa matatizo makubwa pale walipokuwa wanakataliwa kupata anchors katk nchi za magharibi, hasa USA. Walikuwa nik tishio kwa network zao na hakika ni tishio hadi leo.
 
Press Tv ni wajinga kwa sababu wanaendekeza uarabu na kupinga chochote cha magharibi hata kama ni kizuri.
 
Uzaidi unategemea mwelekeo na nini hasa unakitaka. Ukiwa mtu wa habari za kushabikia mambo flani al jazeera poa sana ukiwa na shida ya kujua mawazo ya wamarekani kuhusu dunia na ajenda zao CNN iko bomba sana, ukitaka kujua waingereza na juhudi zao za keundelea na kuwa na nafasi na watu aliowatawala na hasa maeneo waliyojikita sana BBC iko imetulia lakini ukitaka kujua msimamo wa mataifa ya kiislamu na wale wenye itikadi kali ile Press TV ni kitu muhimu na ukitaka vururu vururu za kmichinini ABC itakua saidia. Kimsingi katika news analysis kila mmoja anavuta kwake kwa sababu zake na wewe unapopewa habari kumbuka kuna dozi inamwagwa kwako inaweza kuwa asali au inaweza kuwa kwinini na inaweza kuwa poison
 
Lini Nanyi Waafrika Mtakuwa na Televisheni Yenu yenye Hadhi ya Kimataifa na Ionekanayo kila Kona ya Dunia HII??????
 
Kwa CN nampenda Quest na Amnpour kwa makala zao nzuri sana. kwa BBC napenda sana makala zinazohusu jamii. na kwa aljazeera nadhani wanatoa coverage nzuri kwa mambo ya middle east
 
Back
Top Bottom