Nani yupo sahihi,Afande Sele au Mrisho Mpoto?

Msichoke

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
569
400
Maneno Makali ya AFANDE SELE kutoka Instagram Kwa MRISHO MPOTO na Majibu ya MPOTO kwa AFANDE SELE...

Afande Sele King - Rafiki yangu mkubwa mjomba mpoto kama ni kweli wewe ndio ulikua kinara ktk kusimamia utayarishaji wa wimbo maalumu wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa halafu ukashawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa ndani ya wimbo huo na badala yake ukampa nafasi rafiki yetu christian bella kushiriki ktk wimbo huo unaowahusu watanzania wkt ukijua wazi kuwa bella pamoja na ukweli ni rafiki yetu sana lkn bado yeye sio mtz bali ni mcongoman....ktk hili mjomba umetukosea sana watanzania wenzako na kwa hakika kama ingekua kitendo chako hicho umekifanya kwa nchi zilizoshiba uzalendo na zisizovaa joho la unafki mjomba ulistahili kukatwa nywele zako na kupigwa risasi angalau tano kichwani kwa uchache tena hadharani kwani ulichofanya ni usaliti kwa nchi yako na ni aina flani ya uhaini...

Majibu

Mrisho Mpoto Akijibu - Kaka yangu @afandeseleking Bado narudia kusema kwamba heshima nnayokupa inatoka Mbali sana kwenye chumba cha nne cha moyo Wangu... Sihitaji kupoteza wino Mwingi kukukumbusha tofauti iliyopo kati ya UZALENDO, UZAWA na URAIA kwasababu nina uhakika unazifahamu vyema isipokuwa huenda leo haujaamkia ule ubavu sahihi na ule wa ukarimu wako ulionao siku zote, mpaka ukakataa uwepo wangu hapa Duniani Kwa kunichagulia adhabu ya kupigwa risasi tano tena za kichwa... kwakua hukuniuliza hili jambo kabla Itoshe kusema hunitaki tena...hivyo basi kabla sijapigwa hizo risasi tano nitakachofanya ni kukupa maelezo machache yatakayokufanya uipate picha ya UZALENDO.. Hivi unajua kama John Okello alipigania uhuru wa Zanzibar!? Majeshi yetu yamepigania uhuru wa msumbiji na hata Chegu sio mcuba na alipigania uhuru wa Cuba na Congo pia.. Na je unajua kama kuna wazawa wanaoangamiza maslahi ya nchi na kuna wazalendo wasiobagua!? Kaka, Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zetu ( umajumui Afrika, tena ukichimba huko sana kwa hapa nchini utakuna na Prof Shivji) .. na ndio maana hata mwenge wa uhuru uliwekwa juu ya mlima kilimanjaro ili kumulikia nchi nyingine.. Kumbuka hiyo mitizamo ya KIUZAWA Mwalimu aliita mitizamo membamba.. kwa maana ya kwamba ipo kwa ajili ya Kuiangamiza afrika

Na mwisho ningependa kukuuliza--->Je umezisikia shangwe za wazalendo na wazawa leo hapa dodoma baada ya kusikia Babu Seya na familia yake wamepewa msamaha wa rais!!? Wewe ni RASTA kaka.. kumbuka siku zote CHUKI HUMUUMIZA ANAYEIHIFADHI.. [HASHTAG]#AfrikaUnite[/HASHTAG] ✊

Nani yupo sahihi kati ya hawa mafahari wawili?
Je kuwa Mzalendo ni lazima uwe mzawa wa nchi husika?
 
Uzalendo sio rangi au asili ya nchi unakotoka!Bali ni fikra na utayari kuipigania nchi kwa ajili ya maendeleo na ukombozi wa wanyonge!Alichoeleza mpoto kina maana na ndio fikra hasa za uzalendo!Kuna mijitu imezaliwa hapa na mijizi haina huruma na wanyonge,kisa mweusi utamwita mzalendo?lakini kuna mtu mfano prof shivji ni muasia kwa asilia lakini ana imani na yuko tayari kuipigania TZ mpaka kifo tutamwitaje??
Afande sele akue....
 
Watunge wimbo wabishanie kwenye wimbo... Ila nawaza, kuna msanii wa Tanzania anayeishi nje ya nchi ataruhusiwa kuimba wimbo wa kuhamasisha uzalendo kwenye nchi hiyo?

Let us assume bwana "Harmorapa" anaishi Kigali Rwanda, atashirikishwa kwenye wimbo wa uzalendo wa wanyarwanda?
 
Kama anaishi huko mbona hamna shida kabisa
 
Uzalendo sio rangi au asili ya nchi unakotoka!Bali ni fikra na utayari kuipigania nchi kwa ajili ya maendeleo na ukombozi wa wanyonge!Alichoeleza mpoto kina maana na ndio fikra hasa za uzalendo!Kuna mijitu imezaliwa hapa na mijizi haina huruma na wanyonge,kisa mweusi utamwita mzalendo?lakini kuna mtu mfano prof shivji ni muasia kwa asilia lakini ana imani na yuko tayari kuipigania TZ mpaka kifo tutamwitaje??
Afande sele akue....

Unamtambiaje huyu ni raia rangi au utaifa wake
 
Maneno Makali ya AFANDE SELE kutoka Instagram Kwa MRISHO MPOTO na Majibu ya MPOTO kwa AFANDE SELE...

Afande Sele King - Rafiki yangu mkubwa mjomba mpoto kama ni kweli wewe ndio ulikua kinara ktk kusimamia utayarishaji wa wimbo maalumu wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa halafu ukashawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa ndani ya wimbo huo na badala yake ukampa nafasi rafiki yetu christian bella kushiriki ktk wimbo huo unaowahusu watanzania wkt ukijua wazi kuwa bella pamoja na ukweli ni rafiki yetu sana lkn bado yeye sio mtz bali ni mcongoman....ktk hili mjomba umetukosea sana watanzania wenzako na kwa hakika kama ingekua kitendo chako hicho umekifanya kwa nchi zilizoshiba uzalendo na zisizovaa joho la unafki mjomba ulistahili kukatwa nywele zako na kupigwa risasi angalau tano kichwani kwa uchache tena hadharani kwani ulichofanya ni usaliti kwa nchi yako na ni aina flani ya uhaini...

Majibu

Mrisho Mpoto Akijibu - Kaka yangu @afandeseleking Bado narudia kusema kwamba heshima nnayokupa inatoka Mbali sana kwenye chumba cha nne cha moyo Wangu... Sihitaji kupoteza wino Mwingi kukukumbusha tofauti iliyopo kati ya UZALENDO, UZAWA na URAIA kwasababu nina uhakika unazifahamu vyema isipokuwa huenda leo haujaamkia ule ubavu sahihi na ule wa ukarimu wako ulionao siku zote, mpaka ukakataa uwepo wangu hapa Duniani Kwa kunichagulia adhabu ya kupigwa risasi tano tena za kichwa... kwakua hukuniuliza hili jambo kabla Itoshe kusema hunitaki tena...hivyo basi kabla sijapigwa hizo risasi tano nitakachofanya ni kukupa maelezo machache yatakayokufanya uipate picha ya UZALENDO.. Hivi unajua kama John Okello alipigania uhuru wa Zanzibar!? Majeshi yetu yamepigania uhuru wa msumbiji na hata Chegu sio mcuba na alipigania uhuru wa Cuba na Congo pia.. Na je unajua kama kuna wazawa wanaoangamiza maslahi ya nchi na kuna wazalendo wasiobagua!? Kaka, Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zetu ( umajumui Afrika, tena ukichimba huko sana kwa hapa nchini utakuna na Prof Shivji) .. na ndio maana hata mwenge wa uhuru uliwekwa juu ya mlima kilimanjaro ili kumulikia nchi nyingine.. Kumbuka hiyo mitizamo ya KIUZAWA Mwalimu aliita mitizamo membamba.. kwa maana ya kwamba ipo kwa ajili ya Kuiangamiza afrika

Na mwisho ningependa kukuuliza--->Je umezisikia shangwe za wazalendo na wazawa leo hapa dodoma baada ya kusikia Babu Seya na familia yake wamepewa msamaha wa rais!!? Wewe ni RASTA kaka.. kumbuka siku zote CHUKI HUMUUMIZA ANAYEIHIFADHI.. [HASHTAG]#AfrikaUnite[/HASHTAG] ✊

Nani yupo sahihi kati ya hawa mafahari wawili?
Je kuwa Mzalendo ni lazima uwe mzawa wa nchi husika?
Kama wimbo ulishatungwa na una maneno mazuri ya uzalendo kilichotakiwa ni watu wenye sauti nzuri kuutendea haki katika sauti na sio lazima mtu awe mtanzania tu hata kama hajui kuimba.Huyo naye akivuta majani kichwa chake hakifai.Wakina Dr Remmy Ongala watakuwa na uzalendo kuliko hata huyu manywele
 
Mpoto yuko sawa sana hii dhana ya uzawa iko kwa nchi maskini sana pia inachangiwa sana na ubinafsi uliokubuhu kama jambo linafanyika kwa maslah mapana ya nchi hakuna haja yakuangalia ni nan anayelifanya ndio maana kwenye jesh la marekan kunawapare kibao mpaka wamatengo tukija kwenye soka ufaransa ni mfano tosha na balaa lake wote tunalijua namaliza kwakusema afande mbinafsi kwa kiwango cha kawaida kabisa
 
Mpoto nimemwelewa hapa,
Ila hakusoma sayansikimu huyu jamaa, waziri wa bata akapime safura
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom